RANIA (18)

Zephiline F Ezekiel
JINA: RANIA
SEHEMU YA KUMI NA NANE
ILIPOISHIA...
Alifika hadi nyumba chenyewe anachoishi Dom na kubisha hodi kama vile kuna kazi amekuja kufanya kama mtumishi wa kasri.

Dom alifungua mlango akizani ni mtumishi.

Alipoangalia vizuri alishangaa kuona Rania yuko mbele yake!!!!..

SASA ENDELEA..
Rania!!..Alita Dom kwa mshtuko.

Rania alikua amekunja sura tu kama kawaida..

Dom alimshika mkono na kumpeleka mbali kidogo.

Mbona umerudi ghafla?..aliuliza Dom.

Nataka kuishi ikulu.. Tena bila kujificha...alisema Rania.

Nini?..kwanini?.. Aliuliza Dom.

Kwa gharama yoyote lazima nipambane..alisema Rania.

Sikuelewi Rania... Alisema Dom

Nisaidie nionane na Fasha maana mimi kama mimi siwezi kukaribia anapoishi...alisema Rania.

Rania.. Ongea basi ueleweke...nieleze vizuri..alisema Dom.

Kabla watu hawajauawa zaidi nitalizibiti hili...watu wanakufa kwa sababu yangu. Alisema Rania kwa uchungu.

Nani mwingine amekufa?..aliuliza Dom.

Rania alimwelezea Dom kilochowakuta na jinsi alivyosema yule waliemkamata...

Kwahyo wanasema hata wewe ukifa bado watawaua?..alisema Dom.

Ndio hivyo.... Mimi siwezi kukaa kimya juu ya Hili..alisema Rania

Rania, mbona mapema sana unaweza kupambana vipi na hauna nguvu ya kutosha?..aliuliza Dom.

Ndo nitajua jinsi ya kupata nguvu kuanzia sasa...alisema Rania..

Dom alikua haamini kama Rania ndo kabadilika kiasi hicho yaani..

Sasa Fasha unataka umwambie nini?.. Aliuliza Dom.

Nataka anisaidie kupata nafasi ya kuishi ikulu... Alisema Rania.

Akikuuliza sababu... Aliuliza Dom.

Nitasema nimenusurika kifo huko na wavamizi ndo nikaona bora nirudi ikulu..ila sitamwambia nia yangu halisi...alisema Rania.

Unazani utaweza kumficha hadi lini?.. Aliuliza Dom.

Kwahyo nimwambie ukweli?.. Aliuliza Rania.

Itakua vyema zaidi....alisema Dom.

Siwezi kumwambia ukweli kabla yeye hajaniambia ukweli..alisema Rania.

Ukweli upi unaoutaka?..aliuliza Dom.

Inakuaje ashirikianena mimi wakati yeye ndo mrithi wa kiti cha ufalme na anatakiwa kuniua?..hapo ndo nataka jibu.

Atakwambia ni sababu anakupenda..alisema Dom.

Basi namimi sitamwambia ukweli kama yeye akiamua kunificha...alisema Rania.

Huenda hiyo ndo ikawa sababu ya kweli ya yeye kufanya hivyo....Alisema Dom.

We unazani inawezekana kweli hiyo ndio ikawa sababu?... Aliuliza Rania.

Inawezekana...alisema Dom.

Rania alimkazia Dom macho makavu kwa muda kisha akasema,
Mimi siamini kama hiyo ndo itakua sababu maana nilishawahi kumuuliza kwanini asiniue akasema

"wewe hujajua kitu fulani, ukijua hakika utaelewa kwanini nafanya hivi".. Alisema Rania

Mmmh.. Basi ngoja tuone...alisema Dom.

Wakiwa wanaongea mara Fasha aliwaona kwa mbali.. Fasha alitaka kupoteza akijua Dom anaongea na mtumishi wa kasri,lakini kwa mbali aliona kama ni Rania akasogea kumwangalia vizuri.

Rania!!!... Aliita Fasha kwa mshtuko baada ya kumwona Rania pale..

Mbona uko hapa ghafla?. Aliuliza Fasha.

Mwanamfalme, nimekuja hapa kuishi tena....nisaidie niishi bila kujificha... Alisema Rania akimwangalia Fasha.

Kwani nini kimetokea?..aliuliza Fasha.

Dom, nakuomba utupishe kidogo.. Alisema Rania..

Sawa...alisema Dom huku akiondoka

Haya niambie sasa...nini kimekusibu?.. Aliuliza Fasha.

Mwanamfalme.. Naombaa kabla sijakwambia kilichotokea unijibu swali moja.. Alisema Rania.

Uliza.. Alisema Fasha.

Kwanini unanihifadhi badala ya kuniua wakati wewe ni mfalme ajae na unatakiwa kuulinda ufalme huu?... Aliuliza Rania.

Fasha alishtuka kusikia swali lile kutoka kwa Rania

Mmmh....kwanini kaniuliza hivyo?..alijiuliza Fasha kimoyomoyo.

Fasha alishusha pumzi na kusema:

Rania mimi nafanya hivi kwa sababu nakupenda tu.. Hamna jingine....alisema Fasha.

Rania alijua amedanganywa....mwonekano wa Fasha usoni kipindi anaongea ulidhihirisha kabisa kua anayoyasema sio ya kweli.

Sawa... Wewe ni mwanamfalme wa hii ardhi.. Huwezi kuniamini kiasi cha kuniambia mambo yako ya siri... Sikulaumu kwa kunificha....alisema Rania.

Fasha aliingia katika wakati mgumu sana..alijiuliza kama ni sahihi kumwambia Rania au la...

Rania... Aliita Fasha baada ya kuwaza muda mrefu

Abee...aliitika Rania

Simwamini Dom na ndio maana nashindwa kukwambia.. Alisema Fasha.

Sasa Dom anahusiana vipi na wewe kuniambia?..aliuliza Rania.

Najua nikikwambia hili jambo lazima utamwambia Dom iwe isiwe...alisema Fasha.

Dom ni mwaminifu...namwamini sana tu...ni salama hata akijua....alisema Rania.

Hata hivyo hii haitakua siri milele.. Acha na huyo Dom ajue tu..alisema Fasha.

Rania... Mimi si mtoto halali wa mfalme...alisema Fasha kisha akaweka kituo kikubwa.

Abee....aliropoka Rania kama alikua ameitwa.

Mimi si mwanamfalme halali,na wala malikia sio mama yangu... Alisema Fasha.

Rania alishitushwa na maneno yale..macho yalimtoka kama anaweka uzi kwenye sindano...

Mwanamfalme!!!!....aliita Rania kwa sauti ya chini tena ya chini sana.

Niite Fasha kuanzia sasa...mimi sio mwanamfalme ..alisema Fasha.

Rania alichoka... Tena sana...

Kwahiyo wazazi wako wako wapi?.. Aliuliza Rania.

Siwafahamu..alisema Fasha.

Ulijuaje...?aliuliza Rania

Nilimsikia malikia na mganga wakiongea siku moja...

Mfalme hana uwezo wa kupata mtoto na kwa sababu hiyo alikua akimfukuza kila mwanamke anae muoa kwa tuhuma kua hazai kumbe yeye ndo tatizo..

Alifukuza wanawake kama wanne hivi.. Malikia aliepo alikua anajua kua mfalme ni tasa..hivyo ili auteke moyo wa Mfalme aliamua kuiba mtoto na kusingizia ni wa mfalme.

Sasa kitu kimoja sielewi...kwani mimba yake ilikua haionekani?. ..aliwezaje kumdanganya Mfalme wakati mfalme alikua akilala nae nyumba moja?...kiukweli hapo sijui.. Alisema Fasha.

Umejua tangu lini?..aliuliza Rania..

Nikiwa na umri wa miaka 13...alisema Fasha

Daaah...haya ni majanga kwakweli... Utakua ulipitia wakati mgumu sana kuishi miaka yote hiyo ukijua fika si mtoto wa mfalme..pole sana..... Alisema Rania.

Najua siku moja itafahamika na mimi sitakua na changu hapa... Alisema Fasha.

Lakini Rania akiwa amekaa kawazo sijui nikaite kabaya sijui nikaite kazuri kakamwijia;

Kwahyo Fasha angelikua mwanamfalme halali asingenipenda..ananisaidi kwakua tu hapa si mali yake na siku moja atatolewa...aliwaza Rania ila aliamua kutomuuliza asije akamchanganya bure.

Haya sasa niambie kimekukuta nini?..aliuliza Fasha

Rania alikua alijiuliza aseme au asiseme..ila mwisho wa siku aliamua kukubali kusema

Rania alimweleza Fasha yaliyotokea walipovamiwa....

Fasha aliumia moyoni mwake maana alijua ni Mfalme tu iwe isiwe...

Mwanamfalme,najua kua mfalme lazima atakua anahusika hapa....sijui kama utayapenda haya maamuzi ninayoyachukua...utanisamehe sana mwanamfalme... Alisema Rania.

Maamuzi gani?..aliuliza Fasha.

Mimi..nitaanzisha mapambano na utawala wa baba yako mlezi. Mfalme..alisema Rania.

Rania!!!!!!..aliita Fasha kwa sauti

Utanisamehe sana mwanamfalme... Ila sirudi nyuma...alisema Rania.

Hauna nguvu ya kupambana na ufalme wewe..huoni unajitafutia balaa?.alisema Fasha.

Najua sina nguvu.. Sasa niwaache watu waendelee kufa kwa sababu yangu?...najuta hata Kwanini niliwatoroka walipotaka kuniua ..ningekufa siku hiyo hawa watu wasingekua hatarini leo.. Alisema Rania kwa uchungu.

Rania.. Wewe sio sababu ya haya yote.... Hata kama ukifa wewe wataendelea kuuawa..alisema Fasha.

Kumbe ulikua unajua kila kitu kua hata mimi nikiuawa mauaji hayo hayatakoma..basi ni vizuri....sasa mbona unanizuia kupambana?.. Alisema Rania

Rania.. Kwa sasa huna uwezo wewe wa kupambana na ufalme.... Tafazali nakuomba tulia...alisema Fasha.

Siwezi kutulia..kama ni kufa acha nife....alisema Rania.

Siku zote Rania wewe mbishi na ukiamua jambo hi king'ang'anizi haswa...mimi nakwambia hauna....alisema Fasha kabla hajakatizwa na Rania.

Najua sina nguvu.. Na sihitaji hizo nguvu... Alisema Rania.

Sasa utatumia nini kama sio nguvu?.. Aliuliza Fasha.

Nitatumia mbinu..alisema Rania

Sasa mbinu bila nguvu utakua umefanya nini? Aliuliza Fasha.

Subiri utaona...alisema Rania..

Rania.. Najua kua wewe umezaliwa kwa ajili ya hii kazi..ila nakuomba tulia kwanza... Alisema Fasha.

Unazani hata nikisema nikusanye nguvu nitazapata kuuzidi ufalme?..itakua lini hiyo?.. Aliuliza Rania.

Mimi sitakitafutia nafasi ya kuishi hapa ikulu Rania... Alisema Fasha.

Sawa..nitaiingia kwa juhudi zangu mwenyewe..Alisema Rania kisha akasimama na kuondoka.

Rania!!!..Aliita Fasha ili Rania arudi lakini Rania aliendelea kuondoka.

Fasha alibaki amechanganyikiwa asijue cha kufanya.
*****

Mambo yanaendaje huko?. Aliuliza Mfalme akiwauliza omandi na Mganga

Wanauawa sehemu zingine vizuri tu ila kuna sehemu tumekwama...alisema omandi.

Mmekwama vipi?. Aliuliza mfalme.

Vijana wetu wamesema kwamba kuna familia waliwaua wazazi mtoto akabaki..

Waliendelea kumfuatilia mtoto yule hadi wakampata ila walipotaka kumuua walikumbana na upinzani mkali wakapigwa sana na mtu wasie mjua na mmoja wao alikamatwa na mtu yule... Alisema omandi.

Wao wengi kiasi kile wanashindwaje na mtu mmoja?..alifoka mfalme.

Wanadai ni mtu hatari sana kwenye upiganaji....alisema omandi.

Omandi.... Sasa namtaka huyo mtu haraka sana iwezekanavyo..ukishindwa kumkamata muue...hawezi kutukwamisha.. Alisema Mfalme.

Ndio mtukufu Mfalme .. alisema omandi.

Mganga yeye siku hiyo alikua haongei..alikua mpenzi msikilizaji😁.

Kama kawaida mganga alipeleka umbea kwa malikia suya wa Tharia...alimweleza yote waliyo panga..

Sawa...unaweza ondoka....alisema malikia baada ya kuambiwa mambo yote na Mganga.

Siku hiyo malikia hakutaka maongezi marefu na mdogo wake maana alikua na mawazo.

Akiwa amekaa alikumbuka jinsi alivyompata Fasha kinyemela enzi hizo na kumwacha mama mzazi wa Fasha akilia kwa uchungu mkubwa...

UNAZANI NINI KILICHOTOKEA ENZI HIZO HADI FASHA KULETWA IKULU?.. NI MBINU GANI HIZO AMBAZO RANIA ANADAI ATAZITUMIA?

USIKOSE SEHEMU YA KUMI NA TISA

TAZAMA VIDEO HII KISHA BONYEZA SUBSCRIBE CHINI YAKE WAKATI TUKIELEKEA KWENYE MUENDELEZO

Chapisha Maoni