RANIA (18)

Zephiline F Ezekiel
RANIA (18)
JINA: RANIA Mtunzi: Teddy Mibaraka SEHEMU YA KUMI NA NANE ILIPOISHIA... Alifika hadi nyumba chenyewe anachoishi Dom na kubisha hodi kama vile kuna kazi amekuja kufanya kama mtumishi wa kasri. Dom alifungua mlango akizani ni mtumishi. Alipoangalia vizuri alishangaa kuona Rania yuko mbele yake!!!!.. SASA ENDELEA.. Rania!!..Alita Dom kwa mshtuko. Rania alikua amekunja sura tu kama kawaida.. Dom alimshika mkono na kumpeleka mbali kidogo. Mbona umerudi ghafla?..aliuliza Dom. Nataka kuishi ikulu.. Tena bila kujificha...alisema Rania. Nini?..kwanini?.. Aliuliza Dom. Kwa gharama yoyote lazima nipambane..alisema Rania. Sikuelewi Rania... Alisema Dom Nisaidie nionane na Fasha maana mimi kama mimi siwezi kukaribia anapoishi...alisema Rania. Rania.. Ongea basi ueleweke...nieleze vizuri..alisema Dom. Kabla watu hawajauawa zaidi nitalizibiti hili...watu wanakufa kwa sababu yangu. Alisema Rania kwa uchungu. Nani mwingine amekufa?..aliuliza Dom. Rania alimwelezea Dom kilochowakuta na jinsi alivyosema yule waliemkamata..…