RANIA (19)

Zephiline F Ezekiel
JINA: RANIA
SEHEMU YA KUMI NA TISA
ILIPOISHIA...
Kama kawaida mganga alipeleka umbea kwa malikia suya wa Tharia...alimweleza yote waliyo panga..

Sawa...unaweza ondoka....alisema malikia baada ya kuambiwa mambo yote na Mganga.

Siku hiyo malikia hakutaka maongezi marefu na mdogo wake maana alikua na mawazo.

Akiwa amekaa alikumbuka jinsi alivyompata Fasha kinyemela enzi hizo na kumwacha mama mzazi wa Fasha akilia kwa uchungu mkubwa...

SASA ENDELEA..
Miaka mingi iliyopita suya akiwa msichana mrembo tena alieonekana mpole sana aliolewa na mfalme baada ya mke wake aliekuwepo kutokua na uwezo wa kuzaa..

Suya wakati anaingia ikulu alikua anatambua kua mfalme ndie tasa.

Suya alikua na mwanaume mwingine aliekua na mahusiano nae muda mrefu. Baada ya kupata nafasi ya kuolewa na mfalme aliamua kuelewa na kumwacha mwanaume huyo (habiri) kwenye mataa..

Habiri aliumia sana moyoni ila alijikaza.

Muda mfupi baada ya suya kuolewa alikuja kumwomba habiri warudiane akiwa hivyo hivyo malikia ila habiri alikataa.suya alikasirika sana baada ya habiri kukataa

Kabla suya hajawa malikia alikua akifanya kazi ikulu pamoha na habiri

Baada ya muda habiri alipata mwanamke mwingine akaoa na mwanamke huyo ndie Rai,

Walipendana sana na baada ya muda walioana na kuzaa mtoto mmoja Dom.

Wakati huo suya alipata mwanaume mwingine wa siri saba akawa anafanya nae mapenzi kwa kujificha ili abebe mimba asingizie ni ya Mfalme.

Alifanikisha kubeba mimba na akasingizia ni ya Mfalme.

Ufalme uligubukwa furaha kww malikia kushika mimba.
.
Hatimaye ufalme ulipata mrithi...alisema mfalme kwa furaha.

Muda huo Rai nae alikua na mimba ya umri sawa na wa malikia.

Wote walilea mimba hadi ukafika Wakati wa kujifungua.

Ilikua majira ya jioni ambapo malikia suya alikua akijifungua..muda huohuo kulikua na mwanamke mwingine akijifungua ambae ni Rai

Mwanamke yule alijifungua mtoto mzuri wa kiume..kwa bahati mbaya mwanamke yule alipoteza Fahamu pindi alipomaliza kujifungua kutokana na kupoteza damu nyingi.

Wakati huo malikia suya nae alijifungua..kwa bahati mbaya mtoto wake alikua amekufa tayari kipindi anazaliwa..

Malikia, kwa bahati mbaya umejifungua mtoto aliekufa..alisema mmoja wa mkunga aliekua akimsaidia malikia kujifungua...

Nini?..aliekufa?....Aliuliza malikia kwa mshangao.

Ndio malikia.. Alijibu mkunga...

Hii haiwezekani.... Nataka kwa gharama yoyote ile nipate mtoto alie hai tena wa kiume.... Alisema suya.

Malikia.. Kuna mama huko umezaa nae muda sawa...mtoto ni mzima na ni wa kiume Halafu mama yake amezirai...alisema mkunga mkuu.

Ni nani huyo mwanamke?..aliuliza malikia..

Ni Rai,msaidizi wa mganga... Alijibu mkunga.

Sasa mnafanya nini bado?.. Alifoka malikia.

Tunakwenda kumwiba mtoto wake sasa hivi mtukufu malikia... Alisema mkunga.

Maskini Rai akiwa amepoteza fahamu bado aliibiwa mtoto wake (Fasha wa sasa ) na kuwekewa maiti.

Wale wakunga wezi walimpelea malikia suya mtoto yule wa kiume (Fasha).

Rai alipozinduka aliuliza mtoto wake yuko wapi akaambiwa kua ameshakufa tayari.

Rai alilia sana..kama mtoto mdogo.

Rai alimchukua mtoto yule aliekua amekufa amkumbatie japo amekufa..hakuweza kumtambua maana alikua hajamkalili

Rai alizimia tena kwa mara ya pili... Alipewa huduma na baada ya muda akazinduka.

Habiri mme wa Rai aliumia sana moyoni.. Ilimbidi akae kumbembeleza mkewe.. Habiri na Rai walikua na mtoto mkubwa waliemzaa kabla ya Fasha.. Mtoto yule alitambulika kwa jina la Dom..

Habiri alikua mlinzi wa ikulu na Rai alikua msaidizi wa mganga

Mama... Chi ulichema unaenda kuleta katoto?..kako wapi mama?. Aliuliza Dom aliekua na umri wa miaka miwili tu.

Mwanangu.. Nilikuta watoto wameisha sokoni...nitakaleta siku nyingine sawa eee...alisema Rai akimwambia mwanae Dom

Na tumbo je limeenda wapi?.. Aliuliza Dom

Nimejamba likaisha...alijibu Rai..

Haya mama..utanunua chiku ingine ...alisema Dom.

Sawa mwanangu...alisema Rai

Baada ya usiku kadhaa kupita mganga wa ikulu aligundua kua kua Fasha si mtoto halali wa Mfalme wa Tharia.

Baada ya kuligundua hilo alimdokeza mwenzie mmoja ambae kumbe alikua shushushu wa malikia.

Malikia alipogundua kua mganga ameshajua alipanga njama na kumuua mganga..iliaminika kua mganga ameugua ghafla kumbe aliuawa.

Baada ya kumuua mganga alianza kumuwinda Rai na habiri awaue maana damu ni nzito kuliko maji kama ikitokea wakakaa pale huenda wakajuana na mtoto wao Fasha.

Habiri na Rai waligundua mapema na wakatoroka kuogopa kufa..

Na sasa mtoto wao ndie Mwanamfalme Fasha asiejua wazazi wake..malikia hakujua kama Fasha anaujua ukweli

Hizo ndio zilikua kumbukumbu za malikia suya

Habiri na Rai Walitoroka wakaenda nchi jirani ila baada ya miaka kumi walirudi Tharia ingawa sio ikulu..

Waliporudi Tharia waliendelea na maisha yao ingawa kwa kujificha..

Habiri alikua mfanya biashara baada ya kutoka ikulu na hakua akikaa nyumbani na mkewe na mwanae Dom mara kwa mara

Siku moja habiri alisafiri na katika safari yao walipata ajali wengi wakafa na wengine kutojulikana miili yao ilipo..

Siku zote Rai aliishi akijua mmewe habiri alikua amekufa kwenye ajali ile mbaya.

Moyo wake ulimuuma sana habiri kumwacha.. Mwanaume aliempenda sana.

Aliendelea kumlea mwanae Dom hadi muda huu.
****

Kwa upande wa Rania, baada ya maongezi na mwanamfalme aliondoka...

Fasha alibaki njia panda asijue nini cha kufanya.

Kabla Rania hajaondoka katika kasri Dom alimuwahi..

Rania.....imekuaje?. Aliuliza Dom.

Rania alimwelekeza Dom kwa ishara kua amfuate..

Dom alifanya hivyo. Rania alipohakikisha hakuna anawaona alimweleza Dom kila kitu..

Rania...hii ni kweli?. Aliuliza Dom kwa mshangao mkubwa.

Ni kweli Dom.. Alisema Rania.

Haa.. Dom alichoka.

Fasha hakubaliani na mimi katika hili anasema nimewahi sana.. sana..sina nguvu.. Kama tu wewe unavyosema .Amekataa hata kunisaidia kukaa hapa....alisema Rania.

Dom.. Kama na wewe hauko tayari basi mimi nitapambana mwenyewe ninavyojua...alisema Rania.

Lakini Rania... Alisema Dom ila Rania alimkatisha.

Sikubali ushauri wa yeyote yule... Nimeshaamua...alisema Rania.

Namadi... Nitakua nimekuchosha sana kukaa haoa muda mrefu.. Tuondoke.. Alisema Rania huku akianza kupiga hatua

Kabla hajaenda popote Dom alimshika mkono...

Unaenda wapi Rania?. Aliuliza Dom.

Popote tu...alijibu Rania na kujiondoa mikononi mwa Dom na kuanza kuondoka akiwa na Namadi.

Dom alibakia njia panda.. Alishindwa kujua la kufanya maana Rania alikua hakataziki kwa muda huo...

Rania, nenda salama.. Siwezi kutoka ikulu kwa sasa. Natakiwa kukaa ikulu kwa ajili ya kukusaidia maana ndipo uwanja wako wa vita ulipo....nikikosa nguvu sitaweza kukusaudia...alijisemea Dom huku akimsindikiza kwa macho.

Huku Fasha alikua na mawazo sana.

Rania... Hujui unalolipanga. Hata kama umezaliwa kwa dhamira hii...sio kwa sasa...nahofia utapotea...alijisemea Fasha kimoyomoyo akiwa peke yake chumbani kwake.

Rania aliondoka akiwa na Namadi hadi walipoku wakiishi zamani...

Walishangaa kumkuta hanna ndani lakini akiwa amefungiwa nje na kufuli.

Walipomuuliza aliwapa jibu la kuchekesha .

Alisema kwamba ameona akikaa huko watamvamia tena.. Dawa ni kuingia huku ambako wanajua walishahama. Alisema pia aliingia kupitia upenyo wa dirisha yeye pamoja na Lau.

Namadi alicheka....

Rania alikua kimya tu.. Hakua tena Rania yule mwenye vimbwanga..wala hakucheka.

Baada ya kupata chakula cha jioni walikaa kuyajenga..

Rania alimweleza kila kitu hanna na jinsi alivyopanga kupambana..ingawa hakuwaweka wazi kuhusu Fasha kwamba sio mwanamfalme halali.

Kwahyo unataka kufanya nini muda huu? Aliuliza Namadi.

Cha kwanza natakiwa nipate nafasi ya kuishi ikulu bila kujificha....

Nikipata hiyo nafasi mengine yatafuata nyuma...alisema Rania.

Sasa utafanya nini uweze kwenda ikulu?. Aliuliza Namadi.

Rania alikaa kimya kwa muda mfupi kisha akasema:

Namadi....wewe ni mpiganaji mzuri sana...naomba unisaidie katika hili... Alisema Rania

Lipi hilo Rania?. Aliuliza Namadi.

Kwenye hii nchi ndege aina ya kolokolo (wengine wanaita domo refu) ni adimu sana kupatikana na akionekana basi hili ni janga la taifa ...

Kolokolo akionekana amekufa nje ya lango kuu la kasri hiyo ni hatari kubwa na inaashiria kuna uonevu wa kumwaga damu umetendeka na usipoachwa kutatokea kitu kibaya sana....alisema Rania.

Kwahiyo tunafanya nini?....aliuliza Namadi.

Tumtafute huyo ndege... Mimi nitavaa mavazi kama mtumishi wa ikulu na nitawapelekea walinzi chai yenye dawa ya usingizi mkali...wakilala wote utakuja na kumchinjia pale yule ndege na kuondoka haraka...alisema Rania.

Tutaingiaje ikulu?.....Aliuliza Namadi..

Mimi nazijua chocho zote za kasri.. Tutaingia tu... Alisema Rania..

Sawa... Na hao ndege je?...aliulza Namadi.

Kuna sehemu niliwahi kumwona mmoja.. Niatenda kufuatilia..alisema Rania.

Hizo habari za kolokolo Rania alizisikia kwa mama yake Dom siku ameenda kumtembelea.

Rania alikumbuka mambo yalivyokua.

Wewe Dom wewe... Msimkamate huyo ndege.. Amelaaniwa..akionekana kwako ni mkosi...alisema Rai akimwambia Dom.

Mmmh.. Kiaje sasa?..aliuliza Dom.

Hebu njooni hapa niwaeleze...alisema Rai.

Rai akiwaeleza yote ambayo Rania alimwambia Namadi kuhusu kolokolo.

Haaa...mama ni kweli?.. Aliuliza Dom.

Ni kweli.. Huyu ndege alishawahi kuanguka kwenye kasri mara tatu chini ya wafalme tofauti tofauti. Mara ya mwisho alianguka kipindi mfalme kelkuni ameondolewa madarakani kwa nguvu na umwagaji damu ukatokea...

Mfalme aliekuwepo ambae ni baba wa mfalme aliepo sasa aliogopa ila hata hivyo hakuacha kumwaga damu za wazawa wa kelkuni.

Hivyo hivyo hata mwanae aliepo madarakani sasa alipokua Mfalme aliendeleza tabia za baba yake..

Baada ya hapo ilitokea njaa kali sana ambayo haikuwahi kutokea. Ilibidi wazawa wa kelkuni waombwe msamaha na wasichinjwe ndo njaa ikaisha...alisema Rai.

Mmmh... Kumbe!!...sasa sisi tuna madhara gani tukimshika?..aliulza Dom.

Ni laana wanangu.. Msimshike na msithubutu kumuua maana akionekana amekufa sehem fulani watu wa hapo watatuhumiwa kuamwaga damu isio na hatia. Alisema Rai.

Sasa mbona anakuja hapa kila mara?.aliuliza Dom.

Rai alitabasam kisha akajisemea kimoyomoyo

Ni kwa sababu mimi na wewe Dom mwanangu ni maadui wa familia ya kifalme kwakua sisi ni uzao wa kelkuni ndo maana huyu ndege haishi kuja hapa maana asili yake ni adui wa ufalme wowote uliopo madarakani..

Hata mimi sifamahu kwakweli... Alidanganya Rai.

Muda sio yule ndege alitua kwenye bega la Rania...

Haaaa....mbona ametua kwangu jamani?..au niba mkosi?. Alisema Rania.

Hakika sijakosea. Wewe ndie NADISH mwenyewe hasa..huyu ndege ndio maana ametua kwako... Wewe ni adui mkubwa ww mfalme na ufalme wake.... Alijisemea Rai kimoyomoyo ingawa hakumwambia Rania.

Hizo zilikua kumbukumbu za Rania( ingawa sio kwamba alikumbuka hadi ambayo Rai alijisemea moyoni)

Sasa cha kufanya twende nilikomwona...alisema Rania akimaanisha kwao Dom.

Fasha akiwa peke yake aliwaza sana juu ya aliyoambiwa na Rania.

Utawezaje Rania kupambana?.. Alijiuliza Fasha akaishia kukosa majibu..alibaki na wasiwasi mkubwa

Usiku ulifika. Dom pia alikua na mawazo mengi sana..kila alichokua anakifanya alikua anakosea sababu ya kukosa amani...

Rania.. Uko salama huko?..utaweza kweli Rania??.. Alijiuliza Dom..

Hadi usiku wa manane Dom hakua amelala...alikua na wasiwasi mwingi sana juu ya usalama wa Rania...alitamani aondoke ikulu aambatane na Rania ila alijua kua si chaguo sahihi...

Alibakia akishuhudia usiku unavyogeuka kua asubuhi.

Ilipofika asubuhi tu Dom aliomba ruhusa kwenda kumwona mama Yake mzazi...Dom alipanga kumwambia mama yake juu ya uamuzi wa Rania.

Kesho yake mida ya mchana Rai alitoka na kwenda sehem moja...alifika huko akakaa mpweke sana maana alimkumbuka sana Dom.

Mwanangu Dom.. Njoo nyumbani mama yako nimekukumbuka sana..ni wewe tu mwanangu hayupo mwingine.

Laiti kama mdogo wako angekua hai basi angekua hapa akinifariji wewe ukiwa haupo..

Mwanangu mdogo. Pumzika kwa amani..hata sikupata bahati ya kukupa jina... Mama yako nakukumbuka sana..kaka yako Dom alikua anakungojea sana lakini hata leo haupo nae. Alijisemea Rai machozi yakimtoka.

Akiwa analia mara alishikwa kwa nyuma...

Alishangaa kuona ni mwane Dom amekuja kumsalimia..

Mama .mbona uko Hivi?. Aliuliza Dom Baada ya kumwona mama yake kwenye ile hali.

Nilikua nimekukumbuka sana Dom.. Bora umekuja..alisema Rai akimkumbatia mwanae

Waliongea muda mrefu sana na hatimaye wakakaa ili Dom amweleze mama yake shida halisi iliyomleta..

Sema mwanangu.... Alisema Rai.

Mama.. Ni kuhusi Rania... Alisema Dom

Amekuaje Rania?.. Aliuliza Rai...

Wakati huo Rania alikua amekaribia kwao Dom maana hapakua mbali sana....NINI KINAFUATA? ..

SIJAJUA BADO SIKU DOM NA FASHA WAKIJUANA ITAKUAJE.😺

USIKOSE SEHEMU YA ISHIRINI

TAZAMA VIDEO HII KISHA BONYEZA SUBSCRIBE CHINI YAKE WAKATI TUKIELEKEA KWENYE MUENDELEZO

Chapisha Maoni