RANIA (19)
JINA: RANIA Mtunzi: Teddy Mibaraka SEHEMU YA KUMI NA TISA ILIPOISHIA... Kama kawaida mganga alipeleka umbea kwa malikia suya wa Tharia...alimweleza yote waliyo panga.. Sawa...unaweza ondoka....alisema malikia baada ya kuambiwa mambo yote na Mganga. Siku hiyo malikia hakutaka maongezi marefu na mdogo wake maana alikua na mawazo. Akiwa amekaa alikumbuka jinsi alivyompata Fasha kinyemela enzi hizo na kumwacha mama mzazi wa Fasha akilia kwa uchungu mkubwa... SASA ENDELEA.. Miaka mingi iliyopita suya akiwa msichana mrembo tena alieonekana mpole sana aliolewa na mfalme baada ya mke wake aliekuwepo kutokua na uwezo wa kuzaa.. Suya wakati anaingia ikulu alikua anatambua kua mfalme ndie tasa. Suya alikua na mwanaume mwingine aliekua na mahusiano nae muda mrefu. Baada ya kupata nafasi ya kuolewa na mfalme aliamua kuelewa na kumwacha mwanaume huyo (habiri) kwenye mataa.. Habiri aliumia sana moyoni ila alijikaza. Muda mfupi baada ya suya kuolewa alikuja kumwomba habiri warudiane akiwa hivyo hivyo malikia ila …