
SEHEMU YA ISHIRINI NA MOJA
ILIPOISHIA...
Mganga hakuamini macho yake kwa alichokigundua..dawa zote kwenye chungu zilikua zile zile ila hazifanyi kazi...hii ina maana kwamba kuna mtu aliziharibu..tena kwa kutumia nguvu kubwa mno..Nini?..hii inawezekanaje?. Alijiuliza Mganga akiwa amechanganyikiwa..
SASA ENDELEA..
Nani atakua alifanya hii kazi?...na anauwezo gani wa kufanya hivi?... Alijiuliza mganga huku macho yakiwa yamemtoka..Mganga alihisi kuchanganyikiwa sana tu.. Hakutaka kukubali kama kuna Mtu wa kumzidi uwezo kiasi kile.
Haraka alitoka na kuelekea kwa malikia...
Malikia suya alishituka baada ya kuona mganga amerudu ghafla akiwa anahema.
Kuna nini?..aliuliza malikia suya.
Malikia... Zile dawa zote nilizoweka zimeshateguliwa halafu zikarudishwa kama zilivyo kwenye chungu...alisema mganga.
Nini?...kivipi?.. Kwanini hukulijua hilo?.. Aliuliza malikia.
Aliezitegua atakua na nguvu sana kiasi kwamba sikuweza kugundua...alisema mganga.
Malikia alibaki mdomo wazi..
Ni nani huyo?.. Alijiuliza malikia.
Nenda ukamtaarifu Mfalme haraka ajue cha kufanya... Alisema malikia.
Mganga bila kuchelewa aliondoka na kwenda kumtaarifu Mfalme.
Nini!!!????...aliuliza Mfalme kwa mshtuko baada ya kupata habari zile.
Ndio mtukufu Mfalme.. Himaya hii iko hatarini sana kama ameshatokea mtu kama huyo mwenye nguvu kiasi hicho.. Alisema Mganga..
Mfalme Vamani aliishiwa nguvu na kupoteza fahamu muda huohuo.
Mfalme alikua na tatizo hili kila anapopata habari za kushitua sana.
Mfalme... Aliita mganga kwa mshtuko baada ya Mfalme kupoteza fahamu .
Mganga bila kuchelewa alimwita Fasha na omandi pamoja na daktari binafsi wa mfalme..
Mfalme alichukuliwa na kupelekwa sehemu maalumu kwa ajili ya matibabu..
******
Rania.. Unataka kwenda Lazi kufanya nini?..aliuliza Namadi.
Nikienda Lazi nitajitahidi kukutana na mfalme...alisema Rania kisha akaweka kituo..
Halafu inakuaje?..aliuliza Namadi.
Nilipata habari nilipokua ikulu kua Mwanamfalme anataka kuozeshwa..halafu muolewaji atatoka Lazi.. Mwanamfalme hajui kuhusu taarifa hii... Alisema Rania.
Heeee...kwanini wanataka kumuozesha huko Mwanamfalme?... Aliuliza Namadi kwa mshangao.
Huu ni mpango wa malikia..Mfalme nae ameshakubaliana na hili.. Malikia anataka kumwozesha huko Mwanamfalme kwakua anampango wa kumpindua Mfalme..kwahyo anajipendekeza huko ili aje apate msaada wa kijeshi kwenye uasi wake...Mfalme halijui hili jambo....alisema Rania.
Wewe ulisikia wapi yote hayo?..aliuliza Namadi.
Nililiwasikia wafanyakazi wa mwanamfalme wakiongea pindi nilipokua ikulu ila wao hawakuniona...alisema Rania.
Kwahyo hiyo itasaidia nini?...aliuliza Namadi.
Nitakuja na msafara wa watumishi wa bintimfalme wa Lazi anaeolewa.. Nitaishi ikulu ya Tharia kama mfanyakazi wake.
mmmh...fasha akijua itakuaje?..aliuliza Namadi.
Hakuna kigeni kwake... Hiyo haina shida... Alisema Rania.
Kama alivyo panga Rania alifunga safari akiwa Namadi kwenda Lazi.. Hanna walimwacha akiwa na katoto.
Baada ya siku kazaa waliwasili nchini Lazi.
Rania alikaa sehemu ya maficho kwanza na Namadi alitangulia.
Namadi alikwenda hadi lango kuu la kasri na kutaka kuingia lakini alizuiliwa na walinzi..
Akiwa anazozana nao mara mlinzi mkuu wa mfalme wa Lazi alipita...
Alishangaa sana kumwona Namadi akiwa hapo.. Hakuamnini macho yake. Alisogea ili ahakikishe zaidi na alikuta ni Namadi.
Mlinzi wa mfalme wa Lazi alikuja na kuwaamuru walinzi wale wamwache Namadi aingie ndani.
Mlinzi wa mfalme alimpeleka Namadi moja kwa moja hadi kwa Mfalme wa lazi.
Mfalme wa lazi alifurahi sana kumwona Namadi ambae hakua na hakika kama yu hai ama amekufa.
Walikumbatiana kwa muda mrefu na baada ya hapo walikaa kuongea.
Mlifika salama wewe na Rania?.. Aliuliza Mfalme
Tulifika salama ingawa kwa misukosuko...alisema Mfalme.
Hatimae umerudi nyumbani..Rania anaendeleaje huko?...aliuliza. Mfalme.
Rania yuko hapa lazi na anahitaji kuongea na wewe...alisema Namadi.
Haaa.. Yuko wapi?...aliuliza mfalme.
Nipe muda nikamlete...alisema Namadi.
Baada ya masaa machache Rania alikua ameshafikishwa mbele ya Mfalme.
Rania!!...aliita mfalme kwa mshangao.
Rania alitoa heshima kwa Mfalme na alifurahi kumwona
Rania alimweleza mfalme nia halisi ya yeye kuja pale ghafla kwamba anahitaji kua!batana na msafara wa binti Mfalme akiwa anaenda lazi..
Rania.. Kwanini unataka kuishi ikulu?..aliuliza Mfalme.
Mfalme... Kuna mchezo mhafu unafanyika ikulu... Nahitaji kupambana nao. Alisema Rania.
Mmmh...haya.. Mimi skuulizi zadi. Alisema Mfalme
Sina kipingamizi Rania.. Nitaakusaidia kama wewe ulivyonisaidia siku zile.. Alisema mfalme.
Nashukuru sana Mfalme.. Alisema Rania.
Walikubaliana Rania akae huko hadi pale posa itakapokuja.
Huku Dom alikua na mawazo sana kichwani... Aliwaza jinsi gani Rania atapita katika moto huu.
Muda wote alikua akiangalia pete ile iloyowakutanisha yeye na Rania na kumkumbuka sana Rania.
Akiwa anawaza sana alipata wazo aende kumsalimia Rania huko anakoishi..
Alianza safari bila hata kuaga na kwenda kumwona Rania.
Alipofika alimkuta hanna tu na mtoto yule.
Hanna Rania yuko wapi?.. Aliuliza Dom.
Dom..Rania ameenda Lazi... Alisema hanna.
Lazi!!!??....aliuliza Dom kwa mshangao.
Ndio Lazi... Alisema hanna.
Kufanya nini?..Dom.
Hanna alimweleza kila kitu Dom..
Dom alishangaa sana..
Ameacha ujumbe wako hapa....alisema hanna na kuingia ndani kisha akauleta ujumbe ule na kumkabidhi Dom.
Dom aliufungua haraka na kuanza kuusoma.
"Dom, najua hujafurahisswa na kitendo cha mimi kuondoka bika hata kukutaarifu..najua usingekubali niende kwa kuhofia usalama wangu.. Ndio maana nimeobdoka kimya kimya..
Nisamehe saba Dom ila nakuhakikishia nitarudi....ni mimi Rania.
Dom aliishiwa pozi baada ya kuusoma..alichoka kabisa.
Taratibu aliinuka na kuanza kwenda ikulu.
*****
Huku hali ya Mfalme haikua nzuri baada ya kuzirai muda ule...hata alipozinduka alikua hayuko vizuri.
Aliagiza Fasha aje na ikafanyika hivyo.
Mwanangu... Unaona baba yako hali yangu mbaya...nataka nikukabidhi ufalme huu.. Alisema mfalme.
Wewe ndio mwanangu wa pekee...hauna budi kuchukua nafasi ya baba yako.. Alisema mfalme akiwa kitandani
Kabla ya yote unatakiwa uoe.. Mtoto kutoka ufalme wa lazi...hii ni kwa ajili ya kujenga mahusiano mema ili hata ukupata tatizo au hitaji unaweza kuwaomba msaada...Alisema Mfalme.
Fasha alishtuka sana kusikia habari za kuoa...moyo wake ulimuuma sana hasa akikumbuka kua ameshamuweka Rania moyoni mwake.
Mwanangu.. Hujafurahia maamuzi haya?. Aliuliza mfalme
Aaah..hapana baba...ni Sawa... Aliongopea Fasha
Kuna mtu unampenda?. Aliuliza mfalme..
Hata kama yupo anaempenda lazima aoe binti mfalme wa Lazi... Alidakia malikia suya baada ya kuingia.
Fasha aliishiwa pozi ila hakua na ujanja wala hakuwez kupinga.
Watu wote walitangaziwa kuhusu Fasha kwenda kuchumbia Lazi.. Ufalme uligubikwa na furaha kubwa.
Posa ilipelekwa lazi na ikakubaliwa.
Huku Fasha alikua hana raha hata dakika moja..muda wote alimuwaza Rania...alikumbuka mengi waliyoyafanya zamani..
Alikumbuka shairi la kusisimua alilotunga Rania kwa ajili ya siku ya kuzaliwa kwa Fasha.. Alihisi dinia nzito.
Akiwa anawaza huku anatembea huku na huko mara alikutana na Dom
Dom....usizani mimi kuoa ndo kwamba Rania amekua wako..nitamfanya hata mke wa pili na nitampenda kuliko yeyote... Alisema Fasha.
Dom hakujibu...alitoa heshima kwa mwanamfalme na kuondoka zake.
Hakika Fasha aliumia sana moyoni mwake.
Posa ilifanyika salama na siku ya bintimfalme kuja iliwadia..
Rania alijipanga kurudi Tharia.. Kwa muda huo tayari alikua ameshafanywa msaidizi wa binti mfalme bila yeyote kushirikishwa..
Mfalme alimpa hicho cheo cha kua msaidizi bila kumshirikisha mtu.
Rania alivaa sare zake vizuri na kuambatana na binti mfalme kama msaidizi mkuu wa binti mfalme.
Safari ilichukua Siku kazaa njiani na baadae walifika Tharia
Watu waliwapokea kwa shangwe..watumishi wa ikulu ya Tharia walikuja kuupokea msafara wa binti Mfalme ili akatunzwe kwa ajili ya harusi ambayo ilitakiwa kufanyika siku tano zijazo..
Msafara wa wapokeaji uliongozwa na Fasha mwenyewe..
Fasha alifika na watu wote wakashangilia kumwona...
Fasha alipogeuza macho yake alikutanisha macho ana kwa ana na Rania akiwa kama mmoja wapo wa watumishi wa binti mfalme...
Nini???...alijisemea Fasha kimoyomoyo kwa mshangao mkubwa...NINI KINAFUATA??
USIKOSE SEHEMU YA ISHIRINI NA MBILI
TAZAMA VIDEO HII KISHA BONYEZA SUBSCRIBE CHINI YAKE WAKATI TUKIELEKEA KWENYE MUENDELEZO
TAZAMA VIDEO HII KISHA BONYEZA SUBSCRIBE CHINI YAKE WAKATI TUKIELEKEA KWENYE MUENDELEZO