RANIA (21)

Zephiline F Ezekiel
RANIA (21)
JINA: RANIA Mtunzi: Teddy Mibaraka SEHEMU YA ISHIRINI NA MOJA ILIPOISHIA... Mganga hakuamini macho yake kwa alichokigundua..dawa zote kwenye chungu zilikua zile zile ila hazifanyi kazi...hii ina maana kwamba kuna mtu aliziharibu..tena kwa kutumia nguvu kubwa mno.. Nini?..hii inawezekanaje?. Alijiuliza Mganga akiwa amechanganyikiwa.. SASA ENDELEA.. Nani atakua alifanya hii kazi?...na anauwezo gani wa kufanya hivi?... Alijiuliza mganga huku macho yakiwa yamemtoka.. Mganga alihisi kuchanganyikiwa sana tu.. Hakutaka kukubali kama kuna Mtu wa kumzidi uwezo kiasi kile. Haraka alitoka na kuelekea kwa malikia... Malikia suya alishituka baada ya kuona mganga amerudu ghafla akiwa anahema. Kuna nini?..aliuliza malikia suya. Malikia... Zile dawa zote nilizoweka zimeshateguliwa halafu zikarudishwa kama zilivyo kwenye chungu...alisema mganga. Nini?...kivipi?.. Kwanini hukulijua hilo?.. Aliuliza malikia. Aliezitegua atakua na nguvu sana kiasi kwamba sikuweza kugundua...alisema mganga. Malikia alibaki mdomo wazi.. N…