
SEHEMU YA ISHIRINI NA NNE
ILIPOISHIA...
Omandi walikua wako nje wanaongea..Rania aliona hiyo ndio nafasi nzuri ya kufanya uharifu wake..Taratibu aliitioa ile karatasi na kuanza kuipitishia dirishani..?
Ile anaiweka tu mara alishtuka kusikia.....
SASA ENDELEA..
Unafanya nini hapo?..Rania alishtuka sana...miguu iliishiwa nguvu na akajikuta anatetemeka...
Nakuuliza wewe ni nani na unafanya nini hapo?..aliuliza omandi..
Rania aliona hapa hakuna jinsi... Ni kutimua tu.🏃🏃🏃
Rania alikimbia kwa kasi ya ajabu huku omandi akimfuata nyuma kwa kasi..
Rania alikua vizuri sana kwenye mbio..alikimbia kama hana akili timamu.
Rania alijua fika kua omandi atamkamata...ilimbidi akimbie kwa juhudi..Rania alipata nguvu ghafla na kuruka ukuta pale ikulu na kukimbilia msituni usiku wa manane jamani daah!!..
Omandi nae hakua nyuma...aliruka ukuta na kumkimbiza Rania huko msituni.
Rania alikimbia hadi akajihisi kuchoka ingawa alikua amemwacha umbali kidogo omandi..
Alipoona anaanza kuishiwa nguvu alijitosa ndani ya korongo refu lenye giza nene bila kujua ndani hata kuna nini...bahati nzuri korongo lile lilikua na mawe yamechongoka kiasi kwamba Rania aliweza kuingia taratibu bila kuumia akitumia mawe yale kama ngazi..
Omandi alikuja nyuma kwa kasi...hadi akafika pale kwenye korongo..wala hakuwaza kama mhalifu anaemtafuta anaweza kua humo..kwa kasi alipitiliza na kuendelea kukimbia mbele kumtafuta mhalifu
Alikimbia hadi akachoka hakuna alichokipata..aliamua kurudi kwanza ikulu kujipanga upya.
Walinzi wengie walikua wakishangaa tu vurugu zile bila kujua tatizo ni nini... Muda sio mrefu omandi alirudi akiwa ameloa jasho..
Bila kupoteza muda alikusanya walinzi wa kutosha na kuanza kumsaka mhalifu yule.
Muda huo Rania alikua ndani ya korongo hofu imemjaa...hakua na namna ilibidi tu avumilie..
Habari zile zilisambaa ikulu na zilimfikia Dom pamoja na Fasha.
Dom alihisi kuchanganyikiwa... Kabla hajajua la kufanya mara omandi alifika na kumwamuru amfuate waambatane kwenye kumtafuta mhalifu.. Dom alizidi kuchanganyikiwa zaid
Rania....tafazali subiri kidogo tu nitakuja kwa ajili yako... Alijisemea Dom kimoyomoyo.
Dom hakua mbishi..aliambatana na omandi na kuelekea porini usiku huo..
Walipofika msituni omandi aliwaamuru watawanyike na kwenda huku na huko kumtafuta mhalifu.
Dom alijua kua Rania asingeweza kumwacha omandi..atakua kajificha sehemu tu wala hayuko mbali.. Haraka alianza kurudi nyuma..
Alipofika kwenye lile korongo alisimama huku ameshikilia taa ya moto..akiwa amesimama mara pembeni yake aliiona ile pete ndogo ya Rania...Dom alikumbuka kua ile pete aliwahi kuirudisha kwa Rania siku ile wamekutana tena baada ya siku nyingi za kufungiwa ndani na Fasha
Mbona hii pete iko hapa?..Rania yuko wapi?.. Alijiuliza Dom.
Kama bahati tu aliamua kumulika ndani ya korongo..
Dom hakuamini macho yake baada kumona Rania akiwa ndani ya korongo..
Rania alishangaa kumwona Dom pale..angalau moyo wake ulipata amani akahisi kuna msaada.
Dom aliiingia korongoni na kumtoa Rania ndani ya muda mfupi.
Alimpandisha kwenye farasi na kumrudisha ikulu.. Walipofika karibu na ikulu Dom alimkabidhi Rania nguo za kike ambazo ni sare yake ya kazi maana kipindi anaenda kufanya uharifu alikua amevaa sare ya walinzi.
Kipindi Dom anakuja porini alibeba nguo za Rania za sale ili akimpata amvalishe
Dom alimpeleka Rania hadi sehemu ambayo hakuna walinzi na akamsaidia kuruka ukuta na kuingia ikulu.
Dom alirudi msituni haraka na kujidai anatafuta mhalifu
Rania akiwa ananyata ikulu mara alivutwa na Fasha kwenye uchochoro maana mbele yake kulikua na walinzi wanatembea tembea.
Rania alishusha pumzi kuona aliemvuta ni Fasha.
Rania... Vipi hali yako?..aliuliza Fasha kwa hofu.
Mimi niko salama tu mwanamfalme... Alisema Rania huku akihema
Mwanamfalme alimsaidia Rania kumfikisha uani na kumwambia akae humo hadi hali iwe shwari kisha arudi kwenye chumba chake cha kulala.
Rania alikaa uani hadi akapata upenyo wa kurudi chumbani kwake..
Wewe ingia haraka..hujasikia uvamizi uliotokea?..alifoka mlinzi mmoja baada ya kumwona Rania nje..
Rania aliingia haraka ndani na kufunga mlango..
Rania hakuamini macho yake kama amepona..alishusha pumzi nzito na kulala kama alikuwemo tangu zamani.
Omandi na watu wake walitafuta hadi wakachoka na hakuna walichoambulia.
Baada ya kuchoka walirudi ikulu mida ya asubuhi.. Omandi alienda moja kwa moja hadi kwa Mfalme..alipofika tu Hivi Mfalme alimdaka kwa maswali mengi.
Omandi... Mmemkamata mhalifu?...aliuliza Mfalme.
Hapana Mfalme.. Hatujafanikiwa...alisema omandi.
Kwani alikua anafanya nini?..aliuliza mfalme.
Alikua anaingiza mkono kwenye dirisha lako..sijui alikua anafanya nini..aliponiona akaanza kukimbia.
Kwahyo ndo kaweka huu ujumbe hapa!!!.. Alisema mfalme.
Umekuta ujumbe!?..atakua yeye bila shaka.. Unasemaje?..aliuliza omandi.
Mfalme alimkabidhi omandi karatasi ile akajisomea mwenyewe..
Haaa...ni nani huyu na anajuaje haya mambo?.. Alisema omandi
Hata mimi nashangaa... Alisema Mfalme
Walikaa chini na kuwaza juu ya hili jambo..
Omandi.. Sio kwamba kilichoandikwa hapa kia ukweli?. Aliuliza Mfalme.
Mfalme.. Huyu mtu ndo tunatakiwa kumjua kwanza kabla hatujaanza kufuatilia kilichoandikwa hapa... Alisema omandi.
Utamkamata wapi Kwa sasa?....tusipoteze muda..wakati tunaendelea kumtafuta ni bora tukachunguza hata kilichoandikwa hapa...tunaweza kupuuzia ukawa ni ukweli... Alisema Mfalme.
Hiyo ni kweli mfalme.. Na tufanye hivyo.. Alisema omandi.
Omandi.. Naomba uanze kumchunguza malikia kwa ukaribu na utafute kama kuna watu anapenda kua na maongezi nao mara kwa mara halafu ni viongozi wa juu..alisema mfalme.
Hakika nitafanya kama ulivyoamuru Mfalme...alisema omandi.
Omandi alianza rasmi kumfuatilia Malikia suya ili agundue kama kuna mtu anashirikiana nae.
Wakati huo Rania alikua peke yake ndani anajitibu maumivu aliyoyapata usiku...baada ya hapo alikwenda kusimama peke yake sehemu akiwa na mawazo mengi.
Akiwa hapo anawaza mara alikuja Mars mke wa Fasha.
Alimkuta Rania amesimama tu mawazo yakiwa mbali.
Kwahyo wewe ndio unajidai mrembo sana ee...unamfanya Fasha asiwe na habari na mimi mda wote... Si ndio wewe?..alisema Mars.
Rania alikaa kimya hakijibu kitu...
Nakuuliza wewe hapo...tena umekaa hapa bila kazi..unazani kua umetoka Lazi kuja kutalii?..alijiuliza Mars kwa ukali.
Rania alikua kimya tu amejiamini mdada...
Wewe ni bubu?..aliulza Mars baada ya kuona Rania yuko kimya sana.
Unataka nijibu nini basi?..niseme kua ndio nilikuja kutalii?..au niseme ndio mimi ni mzuri sana?.. Aliuliza Rania kwa kujiamini.
Unanijibi hivyo wewe kama nani hapa?...aliulza Mars kwa ukali.
Rania alikaa kimya wala hakuongea kitu..
Wewe malaya!!!!!...aliita Mars.
Nani?..malaya?....ilisikika sauti kutoka nyuma ya Mars.
Mars aligeuka na kukuta ni Fasha.
Mars..wewe sio ni bintimfalme hapa.. Hapa tafazali heshimu kauli zako...alisema Fasha.
Nisamehe sana lakini huyu Rania ana kiburi sana...alisema Mars.
Basi unaweza kuendelea kwenda ulikokua unaenda Mars.
Mars aliondoka huku amekasirika kwa kitendo cha Fasha kumtetea Rania.
Nashukuru sana mwanamfalme.. Alisema Rania baada ya fasha kumsaidia.
Kwakua Mars alikua hapo basi Fasha hakutaka kuleta kesi zaidi..akionde na kumwacha Rania pale.
Rania aliendelea na shughuli yake ya kupunga upepo mwanana.
Baada ya muda Dom alikuja pale alipokua Rania na kuungana nae kupunga upepo.
Rania aligeuka na kumkuta Dom pembeni yake.
Unaendeleaje Rania?.. Aliuliza Dom.
Naendelea vizuri sana..nashukuru sana Dom... Alisema Rania.
Nilikuja hapa kwa ajili yako Rania... Hii ndio kazi yangu.. Alisema Dom
Kwa ajili yangu wewe na Fasha mnapata shinda ambazo haziwahusu...roho inaniuma sana...alisema Rania.
Dom.. Aliita Rania..
Naam...
Unapata shida sana hapa.. Umehatarisha maisha yako mara nyingi kwa ajili yangu...najiskia vibaya sana.. Sasa hivi ungekua na mama yako anaishi kwa amani..
Sijawahi kukulipa hata jambo moja kati ya uliyonifanyia Dom.. Alisema Rania.
Rania....hakuna furaha kama kukuona ukiwa mzima na salama.. Ni sawa tu linikute lolote ila uwe salama.. Alisema Dom.
Rania alimwangalia Dom usoni kwa dakika kama tano hivi..
Nini...aliuliza Dom kimasihara .
Dom nikwambie kitu... Alisema Rania.
Niambie....alisema Dom kwa hamu ya kuambiwa hicho kitu....RANIA ANATAKA KUSEMA NINI?..?
USIKOSE SEHEMU YA ISHIRINI NA TANO
TAZAMA VIDEO HII KISHA BONYEZA SUBSCRIBE CHINI YAKE WAKATI TUKIELEKEA KWENYE MUENDELEZO
TAZAMA VIDEO HII KISHA BONYEZA SUBSCRIBE CHINI YAKE WAKATI TUKIELEKEA KWENYE MUENDELEZO