
SEHEMU YA ISHIRINI NA TANO
ILIPOISHIA...
Rania alimwangalia Dom usoni kwa dakika kama tano hivi..Nini...aliuliza Dom kimasihara .
Dom nikwambie kitu... Alisema Rania.
Niambie....alisema Dom kwa hamu ya kuambiwa hicho kitu....
SASA ENDELEA..
Rania taratibu alianza kumsogelea Dom.. Dom macho yalikua yamemtoka kama chura mjamzito...Rania alimsogelea zaid Dom akamkazia macho kwa muda wa dakika kama tatu hivi kisha akainua mkono wake kuelekea usoni kwa Dom..Dom ndo alizidi kukodoa macho zaidi
Aiiiiii...we Raniaaaa!!!!... Dom alisikika akilalama baada ya Rania kumbonyeza kwa nguvu chunusi yake kubwa iliyokua usoni.
Anhaa....kumbe ni li chunusi..nilizani jipu...alisema Rania huku akimwachia Dom.
Nilizani umeshakua..kumbe bado una mambo yako ya kitoto..alisema Dom.
Hihiihii...alicheka Rania kisha akasema:
We ulitaka nifanyeje uone ni mambo ya kikubwa?....najua tu ulichokua unawaza kichwani kwako.. Hahaaa...alisema Rania.
Wewe subiri... Nitakukomesha na wewe siku nyingine.. Tuombe uzima tu...alisema Dom.
Utanifanyaje?..aliuliza Rania.
Hata sijui...alisema Dom.
****
Omandi alikua katika kazi yake ya kumchunguza malikia na mienendo yake.
Katika pita zake alimwona malikia akiongea na Amri jeshi.omandi alijiuliza sana ila aliona ni vyema Zaidi kama akitulia na kuwachunguza zaidi kabla ya kumwambia mfalme.
Siku iliyofuata tena aliwaona wakiwa wanaongea. Hapo hakutaka kuvunga..aliondoka moja kwa moja na kuelekea alipookua mfalme.
Kuna ulichokigundua omandi?.. Aliuliza Mfalme baada ya omandi kuingia ndani.
Mfalme... Malikia hua anakua na maongezi ya mara kwa mara na Amiri jeshi... Nahisi watakua na kitu wanapanga...alisema omandi.
Nini?...yaani ndugu yangu anawezaje kushirikiana na malikia na kuniasi mimi!!!...alisema Mfalme.
Mfalme... Kumbuka wewe na bakanga (amiri jeshi) mlikua mkishindania kiti hiki cha ufalme enzi za baba yenu....alisema omandi
Ni kweli... Lakini nilimpa cheo kikubwa tu mbona... Au anataka kunipindua awe Mfalme kabisa.. Alisema Mfalme.
Tufuatilie hili swala kiundani zaidi Mfalme.. Alisema omandi.
Haya nakupa kibali.. Fuatilia..alisema Mfalme
*****
Pame mwanangu.. Ni miaka mingi tangu tuondoke Lazi na kumwacha Rania huko..hatujui ananendeleaje wala anaishi vipi...mimi sina amani na hili... Alisema kaasha.
Ni kweli mama..ila kwa kua wewe umeshazeeka nakuomba ubaki hapa mimi nikaangalie hali ya Rania.
Sawa mwanangu.. Wewe nenda..ukifanikisha kumpata utamleta huku mwanangu... Alisema kaasha.
Sawa mama..alisema pame.
Kesho yake pame aliondoka na kuanza safari ya kuelekea Lazi..
Ilikua safari ndefu sana na ilimchukua muda mrefu sana kufika Lazi.
Baada ya siku kama tatu hivi alikua ameshafika lazi.
Aakiwa mtaani mara alikutana na kijana mmoja.
Wewe kijana samahani....alisema pame baada ya kuona kama anamfahamu kijana yule.
Yule kijana alisimama na pame alimsogelea.
Aaah..kumbe ni wewe...alisema yule kijana baada ya kumtambua pame..
Mbona uko hapa umevaa mavazi ya watumwa?..kulikoni?..aliuliza pame.
Faritha sio mtu mwema kabisa...yaani baada ya mimi na wenzangu wawili kujua mambo yake ya siri akatusingizia kesi tukaletwa utumwani....alisema kijana yule.
Mmmh..kumbe...alisema pame.
Kijana huyu alikua mmoja ya watu waliomteka pame na mama yake kipindi kile wakiwa lazi kwa amri ya Faritha.
Baada ya wao kujua siri za Faritha aliwasingizia kesi na sasa ni watumwa.
Vipi kuhusu mwanangu?.. Aliuliza pame.
Mwanao alishaondoka lazi muda mrefu uliopita baada ya kuwindwa sana na Faritha.
Mfalme aliona bora amtoroshre kwakua kazi aliyoitaka kwa yule binti ilikua imekamilika...alisema kijana yule.
Alielekea wapi?..aliuliza pame
Haijulikani alikoelekea...alisema kijana yule.
Asante sana nashukuru kwa msaada wako..alisema pame
Bila kuchelewa pame alianza tena safari ya kurudi kwa mama yake kumpa taaarifa ile ili waondokealipamoja kuelekea Tharia.
Baada ya siku kadhaa pame alifika alikokua anaishi na mama yake na kumweleza aliyoyasikia.
Enhee..kumbe hayuko Lazi... Alisema kaasha.
Ndio mama...alijibu pame.
Sasa pumzika na baada ya siku mbili tutaanza kwenda Tharia maana najua ndio alikoelekea....alisema kaasha.
Sawa mama...alisema pame
***
Malikia... Mbona hujanipa taarifa kuhusu Mganga?.. Ameelekea wapi?. Aliuliza Bakanga.
Mganga amekwenda kwenye ibaada ya kumtambua huyo alietengua dawa yetu na itachukua mwezi mzima.... Alisema malikia
Sawa malikia... Ila mbona hukunipa taarifa?.. Aliuliza Bakanga.
Aaah...nilisahau tu... Alisema malikia.
Sawa mtukufu malikia..huo mwezi unakamilika lini?.. Aliuliza Bakanga.
Kesho ndio Siku ya mwisho.. Alisema malikia.
Jambo jema sana....natarajia matokeo mazuri... Alisema Bakanga.
Ni kweli... Alisema malikia
Malikia suya... Kumbuka ahadi yako..mimi nakusaidia hapa kwenye mipango yako..ila hakikisha hauivunji ahadi tuliyowekeana mimi na wewe... Alisema Bakanga.
Hilo usijali..yaani hayo maeneo yenye utajiri katika nchi hii utayapata tu kama nilivyokuahidi...alisema malikia
Sawa malikia... Alisema bakanga kisha akaondoka.
Unajidanganya sana Bakanga... Ukimaliza kunisaidia nakuua bila kuchelewa.. Kama umeweza kumsaliti ndugu yako wa damu utashindwaje mimi?..siwezi kufuga msaliti kama wewe...alijisemea Malikia suya kimoyomoyo.
Kama alivyosema malikia suya.. Kesho yake ilikua siku ambapo mganga anakamilisha mwezi mzima wa ibaada yake.
Kila kitu alikua amekamilisha vizuri tu...na sasa alikua anasubiria majibu tu..
Akiwa amekaa anaangalia katika pazia lake la kiganga mara alianza kuona tarehe na siku ambapo dawa iliharibiwa..
Haraka haraka alianza kuchunguza kila kilichotokea Siku hiyo katika mazingira yaliyo karibu na dawa.
Mara aliona mtu mmoja anajificha akimsubiri yeye atokea hapo kwenye dawa..
Mara akaona mtu mwingine tena anajificha tofauti na yule wa kwanza
Anhaaa..kumbe walishilikiana wawili!!!..ila mbona sasa ni viivuli tu sioni sura?..alijiuliza mganga..
Aliendelea kuangalia vivuli vile..
Aliona hadi pale ambapo kivuli kimoja kikashika chungu kupasua...mganga alikodoa macho aone kilichotokea.
Mara kikatokea kivuli cha pili kikamzua kivuli wa kwanza kupasua chungu...
Mmh...inamaana hawa hawakua njama moja?..alijiuliza Mganga ila akaendelea kuangalia tu.
Baada ya mazungumzo ambayo Mganga hakuweza kuyasikia..kivuli wa kwanza akashusha chungu..
Baada ya hapo kivuli wa pili alikamata kijiti kile na kukukata kisha dawa zote zikayeyuka na kujirudia katika hali yake ya kawaida ila hazikua na uwezo tena.
Anhaaa...kumbe ndo maana sikugundua mapema.!!!!alijisemea Mganga..
Huyu kivuli wa pili atakua nani na ananguvu gani kiasi kwaba hata hapa sioni sura naona giza tu???alijiuliza Mganga.
Sasa nitafanya hivi..kwakua hawaonekani basi nitawatupia makombola ambayo yatawaathiri vibaya hasa maeneo ya paji la uso..
Hawatakufa wala hawatapona kabla sijaja na kuwagundua..alijisemea Mganga.
Naanza na huyu kivuli wa kwanza....alisema Mganga na kutuma kombola kwa kivuli yule (Fasha).
Safiii...limempata vilivyo...alijisemea mganga
Wakati huohuo mama yake Dom alikua ameshahisi kua kuna mtu anamfuatilia Dom.
Haraka aliingia kwenye chumba chake na kuanza kazi.
Baada ya muda mfupi alikua alishampata adui yake.
Bila kuchelewa aliweka kinga kiasi kwamba mganga akirusha kombola lolote kwa Dom lisifanye kazi..
Mganga baada ya kuona kua amefanikisha mara ya kwanza, aliandaa kombola kubwa zaid kumpiga alie kata kijiti..
Alilirusha kwa nguvu zake zote..
Baada ya sekunde kama arobaini hivi Mganga alishtukia kitu kama moshi kinakuja kumvagaa...
Mganga aliongopa..alitumia nguvu zake kuurudisha lakini haikuwezekana...ulimrarua vibaya sana kiasi cha kupoteza fahamu ingawa hakufa.
Hii ilitokea maana Dom alikua na ulinzi mkubwa aliowekewa na mama yake.. Vile vile Rai alimwekea ulinzi Dom kiasi kwamba akitaka kudhurika tu yeye anajua.
Lakini Fasha hakua na kinga zaidi ya ile tu aliyowekewa asidhurike pale anapokanyaga ikulu..kwahiyo kombola hakuweza kuliepuka
Wakati huo Mganga anatuma kombola, Fasha alikua amesimama sehemu akiwa peke yake.
Mara ghafla alihisi kitu kizito kikimpiga usoni.. Alihisi kizunguzungu na kuanguka chini..
Kipindi anaanguka Dom hakua mbali maana alikua anapita pale..
Dom apoona vile aliwahi alipokua Fasha.
Mwanamfalme... Mwanamfalme... Aliita Dom lakini Fasha hakuamka..Dom alihisi kuchanganyikiwa....
Hali ya Fasha ilikua mbaya sana....NINI KINAFUATA?..
USIKOSE SEHEMU YA ISHIRINI NA SITA
TAZAMA VIDEO HII KISHA BONYEZA SUBSCRIBE CHINI YAKE WAKATI TUKIELEKEA KWENYE MUENDELEZO
TAZAMA VIDEO HII KISHA BONYEZA SUBSCRIBE CHINI YAKE WAKATI TUKIELEKEA KWENYE MUENDELEZO