RANIA (24)
JINA: RANIA Mtunzi: Teddy Mibaraka SEHEMU YA ISHIRINI NA NNE ILIPOISHIA... Omandi walikua wako nje wanaongea..Rania aliona hiyo ndio nafasi nzuri ya kufanya uharifu wake.. Taratibu aliitioa ile karatasi na kuanza kuipitishia dirishani..? Ile anaiweka tu mara alishtuka kusikia..... SASA ENDELEA.. Unafanya nini hapo?.. Rania alishtuka sana...miguu iliishiwa nguvu na akajikuta anatetemeka... Nakuuliza wewe ni nani na unafanya nini hapo?..aliuliza omandi.. Rania aliona hapa hakuna jinsi... Ni kutimua tu.🏃🏃🏃 Rania alikimbia kwa kasi ya ajabu huku omandi akimfuata nyuma kwa kasi.. Rania alikua vizuri sana kwenye mbio..alikimbia kama hana akili timamu. Rania alijua fika kua omandi atamkamata...ilimbidi akimbie kwa juhudi..Rania alipata nguvu ghafla na kuruka ukuta pale ikulu na kukimbilia msituni usiku wa manane jamani daah!!.. Omandi nae hakua nyuma...aliruka ukuta na kumkimbiza Rania huko msituni. Rania alikimbia hadi akajihisi kuchoka ingawa alikua amemwacha umbali kidogo omandi.. Alipoona anaanza kuis…