
SEHEMU YA ISHIRINI NA SITA
ILIPOISHIA...
Dom apoona vile aliwahi alipokua Fasha.Mwanamfalme... Mwanamfalme... Aliita Dom lakini Fasha hakuamka..Dom alihisi kuchanganyikiwa....
Hali ya Fasha ilikua mbaya sana....
SASA ENDELEA..
Dom alihisi kuchanganyikiwa.. Hakujua nini hasa chanzo cha Fasha kua vile na hakujua afanye nini...Ndani ya muda mfupi tayari matabibu wa ikulu walikua wameshafika.. Haraka walimchukua Fasha na kuondoka nae..Dom aliwafuata kwa nyuma.
Walipofika tu kwenye chumba cha tabibu mkuu walimwingiza Fasha haraka..Dom nae pia alitaka kuingia lakini alizuiliwa.
Kwa huzuni alirudi alikotoka...
Akiwa amekaa mara Rania alikuja huku anahema.
Dom... Eti nini kimemkuta Fasha?.. Aliuliza Rania.
Sifahamu...mwenyewe nimemwona ameanguka tu hata sielewi...alisema Dom..
Mmmmh..sasa atakua amefanyaje..alisema Rania huku akikaa.
Mara ghafla Dom alishtuka.
Nini?...mbona umeshtuka hivyo?.. Aliuliza Rania.
Dom aizidi kukodoa macho...
Dom..tatizo nini?...aliuliza Rania.
Dom akiwa pale alikumbuka siku ile mama yake alipompa kisu cha kukatia kile kijiti alimwambia hivi:
""Mganga alieko ikulu hana uwezo wa kupambana na mimi maana Mganga aliepita aliacha amenipa kitu muhimu sana ambacho ndo kilikua kitovu cha nguvu zake...Mganga wa sasa na malikia suya hua wanakitafuta sana ila hawajui kama ninacho mimi.. Kwahyo Dom wewe wala usiogope..nenda kakate hiko kijiti.. Najua ipo siku watakutafuta wakujue ila hawataweza kamwe.""
Baada ya kukumbuka maneno hayo pia alikumbuka Fasha alivyowaambia kua mganga alikwenda kusali mwezi mzima kumpata alitegua dawa.
Hapo hapo Dom alijua kua mganga kamtumia Fasha kombola maana kwa Dom haiwezekani..kwakua Fasha hana kinga basi atakua kafanikisha kumdhuru.
Rania...aliita Dom huku amekodoa macho bado.
Fasha... Fasha....atakua.. Alisema Dom kwa kusita.
Sema basi... Alisisitiza Rania.
Mganga atakua amefanya hili jambo.. Alisema Dom.
Rania alizunduka kutoka usingizini..
Ni kweli.. Itakua kazi ya Mganga..huenda amekujaribu wewe ikashindikana...alisema Rania.
Lakini sasa atamdhuru kiasi hiki wakati ni mwanamfalme!!!... Alisema Rania.
Hapo hata mimi napata wasiwasi... Alisema Dom
****
Wakati huo pame na mama yake nao walikua wanakuja Tharia.. Baada ya muda mrefu hatimaye walifika Tharia.
Walikwenda moja kwa moja hadi waliokua wakiishi zamani..
Nyumba yao haikuwepo tena maana iliharibiwa kipindi cha vita.. Wakati huo kulikua na makazi mapya kabisa.
Wakiwa wanashangaa mara alikuja mama mmoja aliekua jirani yao enzi hizo.
Aaah...kaasha ni wewe!!!...alisema jirani kwa mshangao.
Mmmh...jamani miaka amepita.. Hadi umezeeka!!!...alisema kaasha.
Walisalimiana na kuongea mawili matatu...hatimaye kaasha aliulizia kuhusu habari za Rania.
Rania!??.. Habari za Rania nenda kawaulize rafiki zake wanaishi kule hivi..alisema jirani.
Tupeleke...alisema kaasha na jirani yule akawapeleka alipokua anaishi Namadi na Hanna pamoja na yule mtoto.
Jirani aliwatambulisha kaasha na pame kwa Namadi na Hanna.
Wanangu..Rania yuko wapi?..aliuliza kaasha baada ya maongezi ya muda mrefu.
Bibi.. Rania yupo anaishi ikulu... Alisema Namadi.
Nini?....ikulu?.. Aliuliza kaasha kwa mshtuko mkubwa..
******
Wakati huo maongezi kati ya Dom na Rania yaliendelea.
Kwahyo Dom tunanafanya nini?..aliuliza Rania.
Twende kwa mama...sisi kama hatuna la kufanya... Alisema Dom.
Ndio twende... Lakini muda sio mrefu wewe utatafutwa..ukikosekana itaonekana wewe mhalifu na watahisi ndo umemdhuru Mfalme na sasa umetoroka..hili unalionaje?..aliuliza Rania.
Ni kweli....sasa tutafanya nini na hii ni dharura?..aliuliza Dom.
Nitaenda peke yangu.. Alisema Rania.
Hapana Rania.. Huwezi kwenda mwenyewe.. Alisema Dom.
Naweza na ni lazima niende peke yangu... Alisema Rania huku akisimama na kuanza kuondoka.
Rania.!!!!!!....
Dom kua mwelewa...ukitafutwa usionekane utabeba kesi kubwa sana... Alisema Rania.
Dom alimruhusu Rania kwenda mwenyewe kishigo upande..
Aliondoka moja kwa moja hadi kwa mama yake Dom.
Ooh...Rania.. Umekuja mwenyewe!!.. Alisema mama yake Dom.
Ndio mama...alisema Rania.
Mama...kimenileta hapa kitu kimoja....alisema Rania
Niambie mwanangu... Alisema Rai.
Mama..mwanamfalme Fasha amepatwa tatizo... Hali yake sio nzuri kabisa..alisema Rania kisha akaweka kituo.
Rai alipata mshtuko mkubwa hadi mwenyewe akajishangaa kwanini ameshituka kiasi kile..
Amepatwa na nini?...aliuliza Rai
Hata sielewi... Alikua amesimama tu mara akadondoka chini...inasemekana anajeraha jeusi kwenye paji la uso... Alisema Rania.
Jeraha jeusi kwenye paji la uso!!!??..aliuliza Rai kwa mshangao.
Inamaana Dom alishirikiana na mwanamfalme kwenye kuivunja ile dawa?..Aliuliza Rai..
Ni kweli.. Alisema Rania na kumweleza jinsi ilivyotokea siku hiyo.
Sasa kwanini Dom hakusema mapema?...daaah hapa sina jinsi...alisema Rai.
Mama...kwahyo mwanamfalme atakufa?....Aliuliza Rania kwa wasiwasi.
Hilo tatizo haliwezi kumuua..mganga amefanya hivyo ili tu kumkamata Fasha....Wala lile sio jeraha la kweli...ni mazingaombwe tu na hata asipomtibu litaondoka lenyewe baada ya siku tatu... Alisema Rai.
kwahiyo mganga amemjeruhi Fasha makusudi!!..hana hofu?..aliuliza Rania
Kwakua Fasha alikua na Dom wakati wa tukio,bila shaka Mganga amefanya hivyo baada ya kushindwa kuwatambua ni akina nani maana alikua anaona vivuli tu kwakua kinga ya Dom ni kubwa...kwahyo amefanya hivyo ili akirudi amtafute mwenye jeraha ndo ajue ni nani mhusika...alisema Rai.
Sasa hapa nikisema nimtibu Fasha haitasaidia kitu.. Maana kwakua Mfalme na watu wake walishajua kua Fasha amepatwa tatizo, Mganga akija lazima atauliza kama kuna mtu amepata jeraha jeusi kwenye uso,na lazima watamwambia hata kama Fasha akiwa ameshapona mda huo... Alisema Rai.
Kwahiyo mama tutafanya nini?.. Aliuliza Rania
Rania...njia yako ni hii..vita yako ni ya wazi sio kujificha...wanatakiwa kukujua kua wewe ni nani na upigane nao bila kificho.....kwahyo acha mambo yawe hadharani..ndio vita ianze..alisema Rai.
Mama...na ikijulikana huoni Dom atakua matatizoni!?...aliuliza Rania kwa wasiwasi.
Rania mwanangu...hicho kitu hakipo..wewe ngoja utaona...alisema mama yake Dom.
Mama!!!!...
Rania, hivi umeshajiuliza mfalme atakua katika hali gani akijua Fasha sio mwanamfalme halali?....na malikia atachukua hatua gani baada ya kuumbuka?....aliuliza Rai.
Rania alisita kujibu.
Wala usiwaze sana....baada ya ukweli kua wazi..vita itakua kati ya malikia na wapambe wake na mfalme na wapambe wake...hapo utatumia akili..na huo ndio utakua wakati pekee wa nyie kumfanya Mfalme kuachia madaraka kwa hiari yake...nazani umeshanielewa.. alisema Rai
Ndio mama nimekuelewa..alisema Rania
Sasa kuweni wavumilivu...na hata mambo yakienda tofauti na nilivyosema bado sina wasiwasi.. Nitawalinda wanangu na hakuna kibaya kitakachowakuta...alisema Rai.
Sawa mama..alisema Rania.
******
Huku ikulu Fasha alikua amelazwa bado na hakuna tiba iliyofanya kazi juu yake.
Masaa mengi yalipita na hakuna walichomsaidia.
Kama tu Rania alivyosema, Dom aliitwa ili aje aleleze tukio vizuri kwa matabibu waone jinsi ya kumsaidia Fasha.
Doma aliitikia wito akaenda.
Wakati huo Mganga alikua tayari alishafika ikulu ingawa alikua na majeraha ya moshi ule.
Kila alipojaribu kuangalia mwenye jeraha alipo,dawa yake ilionesha huyo mtu yupo ikulu... Hiki kitu kilimchanganya sana Mganga.
Dasu....umefika!!!!....mambo yameendaje?...Aliuliza malikia kwa pupa.
Malikia.. Kuna mtu hapa ikulu amepatwa na ugonjwa ghafla?.. Aliuliza mganga.
Mbona umeuliza?..aliuliza malikia.
Niambie tu..nina maana yangu... Alisema Mganga.
Ndio.. Ni Fasha.. Amepatwa ugonjwa ghafla na anakovu jeusi usoni...alisema malikia.
Nini!!!!????..Fasha???...Aliuliza mganga kwa mshangao....
Ndio.. Kwani nini?..aliuliza malikia.
Nipeleke aliko...sasa hivi..nakuomba malikia.. Alisema Mganga.
Malikia hakutaka kubisha...aliondoka na Mganga na kwenda nae aliko Fasha.
Walipofika malikia suya alibakia nje Mganga akaingia maana Mfalme alikua ndani na hajui kua suya anaushirikiano na Mganga.. Kwahyo suya hakutaka kuharibu mambo.
Mganga hakuamini kuona kweli ni Fasha.
Aah...dasu bora umefika...ona hali ya Fasha.. Alisema Mfalme.
Mganga bila kuchelewa alimshika Fasha usoni na kovu likapotea na Fahamu Zake zikarudi..
Matabibu wote waliamuliwa kuondoka na akabaki Mganga, mfalme na omandi.
Kipindi Dom anakuja alikutana na matabibu wanatoka..wakamwambia arudu tu hahitajiki kwa sasa
Fasha... Umefanya nini hiki?..aliuliza Mganga baada ya fasha kuzinduka.
Kwani kawaje?..aliuliza Mfalme.
Mfalme samahani sana kwa kukwambia haya..alisema mganga.
Nini?..aliuliza Mfalme.
Mganga alieleza yote yaliyotokea hadi Fasha umemkuta huo ugonjwa..
Nini????...Fasha?... Aliuliza Mfalme kwa mshtuko.
Fasha!!!!!....... Aliita mfalme kwa hasira akimtazama Fasha.
Kwanini umefanya hivi?...aliuliza mfalme huku amemkaba Fasha..
Ni kwa sababu nilimpenda yule binti... Sikutaka akamatwe..alisema Fasha.
Mfalme alipata hasira akampiga Fasha bonge la kofi.
Kwahyo huyo binti ni muhimu kuzidi milki ya ufalme?.. Aliuliza Mfalme kwa hasira.
Milki ya ufalme haihusiani na mimi...nitailindaje sasa na kuacha ninaempenda afe?..alisema Fasha.
Mganga alishtuka kusikia fasha anasema hivyo..alipata wasiwasi mkubwa kua labda Fasha anajua siri.
Nini?....haihusiani na wewe?...inahusiana na nani?..aliuliza mfalme macho yamemtoka kwa hasira...
Bila shaka Mganga na malikia wanaelewa vyema nikisema mimi sihusiani na utawala..hebu waulize...alisema Fasha.
Mfalme aligeuka na kumwangalia mganga ambae alikua akitetemeka vibaya sana.
Dasu...nini maana ya haya maneno... Aliuliza Mfalme akimtazama mganga..
Muda huo suya alikua akisikia yote... Alihisi kuishiwa nguvu ghafla....NINI KINAFUATA?..
USIKOSE SEHEMU YA ISHIRINI NA SABA
TAZAMA VIDEO HII KISHA BONYEZA SUBSCRIBE CHINI YAKE WAKATI TUKIELEKEA KWENYE MUENDELEZO
TAZAMA VIDEO HII KISHA BONYEZA SUBSCRIBE CHINI YAKE WAKATI TUKIELEKEA KWENYE MUENDELEZO