
SEHEMU YA ISHIRINI NA SABA
ILIPOISHIA...
Dasu...nini maana ya haya maneno... Aliuliza Mfalme akimtazama mganga..Muda huo suya alikua akisikia yote... Alihisi kuishiwa nguvu ghafla.
SASA ENDELEA..
Nini?...Fasha amejuaje kwani?..alijiuliza malikia.Dasu!!!!....mbona uko kimya na husemi kitu?.. Aliuliza Mfalme kwa ukali..
Mfalme... Mimi si....alisema Dasu kwa kutetemeka...
Omandi... Haraka Nenda kamlete suya hapa!!!!...alisema Mfalme.
Omandi ile anatoka nje tu alikutana na malikia anataka kukimbia.
Mtukufu malikia.. Mfalme anakuhitaji...alisema omandi.
Kwa uoga Malikia aliingia ndani.
Suya...naomba useme kitu kuhusu hili...Fasha kasema yeye hahusiani na ufalme huu na amesema wewe na Mganga mnajua kwanini..naomba useme haraka!!..alisema Mfalme.
We Fasha!!... Inamaana leo unataka kukataa kwamba wewe sio mtoto wetu?.. Alijiulizisha suya kwa ukali..
Mfalme alimgeukia malikia kwa hasira!!...
Nini?... Umesemaje?.. Aliuliza Mfalme kwa mshtuko...
Inamaana Fasha kwanini anikane mimi na wewe kama wazazi wake.. Nani alimzaa basi?..
Suya...suyaa... Umethubutuje kunidanganya miaka yote hii?...aliuliza mfalme akiwa amekodoa Macho kwa mshangao.
Mfalme mimi sijakudanganya..ni huyu tu Fasha ndo ana...alisema malikia kabla hajakatizwa na mfalme.
Kimya!!!!...kwani umesikia Fasha ametamka hilo neno?..kwamba sisi sio wazazi wake?...Aliuliza mfalme kwa hasira.
Malikia alijua kua ameshavuruga...kitendo cha kujishtukia kukanwa na Fasha kua sio mama yake wakati Fasha hajaongelea hilo jambo kilimfanya Mfalme ajue kumbe hicho ndo Fasha alisema malikia na Mganga wanajua sababu...Mfalme alipata pichanya ukweli halisi uliokua haukubaliki kirahisi.
Mfalme tafadhali nisamehe!!!... Alisema malikia kwa woga.
Nikusamehe kwa kosa gani?..aliuliza mfalme.. Malikia alishindwa kusema hata anahitaji msamaha wa nini.
Huko mganga alikua ameshachanganyikiwa hasa..alitamanu ardhi ipasuke immeze.
Mfalme alihisi kuchanganyikiwa....
Omandi... Aliita mfalme.
Ndio mtukufu Mfalme....aliitika omandi.
Mtoe malikia ukamfungie kwenye chumba chake na uweke ulinzi mkali... Alisema mfalme.
Wakati yote hayo yanaendelea Fasha alikua akisikilizia tu akiwa kitandani...
Fasha... Nilichosikia unataka kusema ni kweli?...Mfalme.
Mfalme....Ni kweli... Mimi sio damu yako wala ya malikia... Wazazi wangu hata siwajui...alisema Fasha.
Ulijua tangu lini?.. Aliuliza Mfalme.
Nikiwa na miaka 13...alisema Fasha.
Kwanini usingekua muwazi tangu zamani?..Aliuliza Mfalme.
Usingeamini baba...alisema Fasha
Mfalme alijikuta akitokwa chozi...alimkumbatia Fasha.
Fasha... Wewe ni mwanangu tu...haijalishi sijakuzaa wala nini.. Alisema Mfalme
Walikumbatiana kwa muda mrefu kila mtu akitirish machozi.
Baada ya hayo mfalme aliwaita Mganga, malikia na mwanamfalme na omandi.
Suya malikia wa hii ardhi.. Naomba uniambie ukweli juu ya hilo jambo... Fasha ni mtoto wa nani?..aliulza Mfalme akiwa amekunja sura.
Mfalme..Fasha ni mtoto wa aliekua msaidizi wa mganga aliekufa...alisema malikia.
Ulimpataje?..aliuliza mfalme.
Malikia alieleza alivyompata Fasha.
Mfalme alizidi kuchanganyikiwa...alichoka hasa.
Kwahyo kumbe ulikua na mimba ya mtu mwingine!..haikutosha ukaiba mtoto wa mtu baada ya mwano kufa!!!...alisema Mfalme.
Malikia wangu.. Siwezi kukuvumilia kwa haya uliyoyatenda...ni aibu...alisema Mfalme.
Kwahyo na huyu mganga ukamrubuni akawa upande wako..mtu niliemwamini sana... Alisema mfalme.
Usimhukumu mganga.. Alifanya yote kwa amri yangu... Nihukumu mimi..alisema suya.
Mama...haina haja ya kuficha zaidi.. Mambo yalishaharibika tayari...mganga ni ndugu yako wa damu ndo maana mkashirikiana....alisema Fasha.
Mfalme alihisi kuzimia....alihisi yote ni ndoto lakini ndi ilikua ukweli...
Nitakuvua cheo cha umalikia,na kaka yako nitamvua cheo cha uganga.. Mmenifanyia mambo ya kutisha...alisema Mfalme.
Lakini mfalme utawaeleza nini watu?.ukinivua umalikia basu watu watasema hata Fasha umvue cheo cha Mwanamfalme maana sio mtoto wako..utafanya nini?.alisema malikia
Nitajua mimi nitakavyofanya!!!! Usinirubuni zaidi...alisema Mfalme kwa ukali.
Kesho nitaitisha mkutano na kuwafukuza rasmi..kosa lako linahitaji hukumu ya kifo hata wewe unajua...sasa ili usife nitasema kosa tofauti na hili na utafukuzwa badala ya kufa...alisema Mfalme.
Kosa gani hilo utalisema...aliuliza malikia.
Suya!!!...usiniudhi zaidi..uliyonifanyia yanatosha sana...alisema mfalme na kuwaamuru waondoke.
Kama Mfalme alivyosema.. Kesho yake Mfalme aliitisha kikao cha viongozi wakubwa wa nchi ya Tharia.
Aliwaeleza kua malikia na mganga watafukuzwa ikulu kwakua wameonesha dharau kwakua Mfalme aliwaita mara tatu na kwa siku tatu mfululizo wakakataa kwenda..hivyo anawafukuza.
Wakuu wa nchi walimuunga Mfalme mkono na kukubaliana kuwafukuza kwakua walitia aibu ufalme.
Baada ya hapo Mfalme alikua akiongea na omandi.
Mfalme... Kwanini umeamua kuuficha ukweli ili kumlinda msaliti?..aliuliza omandi.
Sijafanya hivyo kumlinda suya wala Mganga.. Nimefanya hivyo kumlinda Fasha ili asije akavuliwa hadhi ya mwanamfalme.. Alisema omandi...
Ni sawa..lakini Fasha hawezi kua mfalme kulingana na sheria za hii nchi... Alisema Mfalme.
Ni kweli...lakini nitafanya nini?...itabidi awe...hakuna mwingine zaidi yake...alisema Mfalme.
Mwanamfalme.. Pole kwa misukosuko..alisema Rania Baada ya kukutana na Fasha.
Ni afadhali sasa nimekua huru.... Alisema Fasha.
Dom yuko wapi?... Aliuliza Fasha.
Kabla Rania hajajibu Dom alikua amefika pale.
Mwanamfalme... Pole kwaa matatizo..alisema Dom.
Asante Dom... Nina maongezi na wewe...alisema Fasha.
Walitoka wakakaa kuongea.
Dom..siku tunaitegua dawa tulikua wote...mbona wewe hujapata madhara?.. Aliuliza Fasha.
Mama kabla hajanipa kile kisu alinipa kinga.. Na ndo maana hata mganga hakuweza kututambua hadi akatuma kombola ili aje ajue ni nani...alisema Dom.
Mama yako atakua mtu mkubwa sana.. Atakua anajua mengi sana...alisema Fasha.
Ni kweli....Alisema Dom
Nahitaji kuonana nae...huenda kupitia yeye nitapata kujua ukweli kuhusu wazazi wangu....alisema Fasha.
Hilo halina shaka...nitakupeleka...alisema Dom.
Sawa nashukuru.. Alisema Fasha kisha wakaagana.
*******
Huku Malikia akiwa na Mganga walikua wakikusanya virago waondoke ikulu huku wakiwa chini ya ulinzi mkubwa.
Baada ya hapo waliondoka na kwenda nje ya ikulu..
Mida ya usiku mkuu wa majeshi alikua katika msitu mnene wenye giza akielekea waliko malikia suya na Mganga.
Baada ya muda alikua ameshakutana nao sehemu waliyokubaliana kabla ya kuondoka kwao.
Walikaa chini na kuanza kuongea.
Malikia suya..niko hapa nakusikiliza...alisema mkuu wa majeshi.
Kama unavyoona..tumefukuzwa ikulu... Na Fasha hayuko upande wetu...sasa jambo la kufanya ni moja tu..alisema malikia.
Niambie jambo hilo..alisema mkuu wa majeshi.
Naomba ufanye juu chini Fasha asiwe mrithi wa hicho kiti cha ufalme... Kwakua Mfalme hana mtoto mwingine basi wewe mdogo wake utakua Mfalme... Alisema malikia.
Mkuu wa majeshi kusikia hivyo aliwaka tamaa.. Akakubali haraka sana.
Sasa malikia, tutamtoa Fasha kivipi?..au tutoboe siri?..alisema mkuu wa majeshi.
Hapana... Ukitoboa siri utaonekana muongo mkubwa maana hauna uthibitisho...na unaweza kuuawa kwa kosa hilo.. Tafuta njia nyingine....alisema malikia
Basi tufatanya hivi... Kwakua Fasha alimsaidia NADISH adui wa nchi basi nitatumia huo udhaifu....alisema mkuu wa majeshi.
Hapana... Hata hilo halitawezekana maana hakuna wa kulithibitisha halafu jambo la NADISH ni siri..huwezi kuliweka wazi...alisema Mganga.
Sasa tunafanya nini?...aliuliza mkuu wa majeshi.
Njia ni moja tu....kumuua mwanamfalme... Alisema suya.
Malikia!!!!..aliita mkuu wa majeshi kwa hofu.
Ndio hivyo...hakuna njia nyingine... Alisema malikia.
Sawa nitafanya hivyo...Alisema mkuu wa majeshi maana tamaa ilikua imeshawaka.
Kumbuka kitu kimoja....nitakusaidia kwenye kua mfalme lakini kwa shariti moja...alisema suya.
Lipi hilo?...
Utanifanya malikia wako...alisema suya..
Hilo halina shida... Alisema mkuu wa majeshi.
Waliagana na mkuu wa majeshi akaondoka.
Njia nzima mkuu wa majeshi alikua akiwaza juu ya kumuua Fasha...
USIKOSE SEHEMU YA ISHIRINI NA NANE
TAZAMA VIDEO HII KISHA BONYEZA SUBSCRIBE CHINI YAKE WAKATI TUKIELEKEA KWENYE MUENDELEZO
TAZAMA VIDEO HII KISHA BONYEZA SUBSCRIBE CHINI YAKE WAKATI TUKIELEKEA KWENYE MUENDELEZO