RANIA (27)

Zephiline F Ezekiel
RANIA (27)
JINA: RANIA Mtunzi: Teddy Mibaraka SEHEMU YA ISHIRINI NA SABA ILIPOISHIA... Dasu...nini maana ya haya maneno... Aliuliza Mfalme akimtazama mganga.. Muda huo suya alikua akisikia yote... Alihisi kuishiwa nguvu ghafla. SASA ENDELEA.. Nini?...Fasha amejuaje kwani?..alijiuliza malikia. Dasu!!!!....mbona uko kimya na husemi kitu?.. Aliuliza Mfalme kwa ukali.. Mfalme... Mimi si....alisema Dasu kwa kutetemeka... Omandi... Haraka Nenda kamlete suya hapa!!!!...alisema Mfalme. Omandi ile anatoka nje tu alikutana na malikia anataka kukimbia. Mtukufu malikia.. Mfalme anakuhitaji...alisema omandi. Kwa uoga Malikia aliingia ndani. Suya...naomba useme kitu kuhusu hili...Fasha kasema yeye hahusiani na ufalme huu na amesema wewe na Mganga mnajua kwanini..naomba useme haraka!!..alisema Mfalme. We Fasha!!... Inamaana leo unataka kukataa kwamba wewe sio mtoto wetu?.. Alijiulizisha suya kwa ukali.. Mfalme alimgeukia malikia kwa hasira!!... Nini?... Umesemaje?.. Aliuliza Mfalme kwa mshtuko... Inamaana Fasha kwanini anikane …