RANIA (30)

Zephiline F Ezekiel
RANIA (30)
JINA: RANIA Mtunzi: Teddy Mibaraka SEHEMU YA THELATHINI ILIPOISHIA... Lakini mwanangu mbona alikufa?..au habiri atakua alizaa na mwanamke mwingine?.. Au ni mtoto wa ndugu yake habiri?.. Alijiuliza Rai bila kupata majibu sahihi.. SASA ENDELEA.. Mama..tatizo ni nini?...aliuliza Dom baada kuona mama akishangaa sana. Aaah....hamna kitu.. Alisema Rai. Wote walibaki wakishangaana. Wakikaa kimya kwa muda mfupi baadae Rai aliuliza; Mlikua mnaelekea wapi?. Tulikua tunakuja hapa...alisema Dom. Kuja hapa?....alisema Rai kwa mshangao. Ndio mama...alijibu. Ikawaje mkaumia?..aliuliza Rai. Walimweleza yote yaliyotokea hadi wakaumia hivyo. Mmh....poleni sana wanangu.. Haya hapa mlikua na shida gani?... Aliuliza Rai. Mwenye shida ni mimi hapa...kuna jambo natamani kufahamu...Alisema Fasha. Jambo gani?...aliuliza Rai. Bila shaka wewe unajua mambo mengi kuhusu ikulu na utawala....nahisi pengine unaweza kunisaidia kuwajua wazazi wangu halisi...alisema Fasha. Kwani una mwanga wowote kuhusu wazazi wako?.. Aliuliza Rai. Sina mw…