RANIA (35)
JINA: RANIA Mtunzi: Teddy Mibaraka SEHEMU YA THELATHINI NA TANO ILIPOISHIA... Haraka alimwita mlinzi wake mkuu na baadhi ya watu wanaowaamini. Haraka alituma mjumbe apeleke taarifa kwa Mfalme wa Tharia kuhusu uasi unaoendelea ili nao waungane. SASA ENDELEA.. Mjumbe yule bila kuchelewa alikwenda hadi Tharia safari ambayo ilichukua kama siku mbili njiani. Alifika ikulu na kuonesha kitambulisho chake kisha akaruhusiwa kuingia ndani na kuonana na mfalme.mjumbe yule alimkabidhi mfalme ujumbe ule na kukaa kusubiri majibu. Mfalme aliwaita watu wake wa karibu ili kujadili nao jambo la kushirikiana na mfalme wa Lazi. Mfalme alikua ashajua tayari mipango yote ya suya na kuhusu kushirikiana ba Faritha.kwahiyo aliita watu wake ili tu kuona kama kushirikiana na Lazi inafaa au la. Alimwita omandi, Fasha na Rai na kuwaeleza kilichojiri. Fasha na omandi waliifika ila Rai alikua bado hajafika. Baada ya kumsubiri kwa muda mrefu kidogo Rai aliingia. Oooh..tumekusubiri sana...alisema mfalme baada ya Rai kufika. Ingia..…