
SEHEMU YA THELATHINI NA SITA
ILIPOISHIA...
Dom alishtuka sana kusikia Rania akisema "sijui kama nitarudi nikiwa hai au nitakufa huko""Alishituka sana mapigo ya moyo yakaenda kwa kasi sana..
SASA ENDELEA..
Sawa nitakuruhusu uonane nao mara moja tu ila ukiwa unaonana nao na mimi nitakuwepo kuhakikisha hamliongelei hili swala.. Alisema Rai.Sawa.. Naweza kwenda kuwaona sasa?..aliuliza Rania.
Haina haja... Ngoja kwanza... Alisema Rai.
Dom..toka huko ulikojificha njoo hapa....alisema Rai.
Dom alishituka..haaa kumbe mama ameshaniona!?..alijisemea Dom.
Fanya haraka.. Alisisitiza Rai.
Dom kwa aibu kidogo alitoka na kuja pale alipokua rai na Rania.
Mama,kwanini usiniweke wazi juu ya hili?.. Aliuliza Dom.
Rai alibaki kimya..Rania na Dom walibaki wanaangaliana tu maana na kusema hakikuwepo.
Mama....aliita Dom.
Nazani ulipokua umejificha ulisikia angalau kidogo.. Inatosha...alisema Rai.
Lakini mama....alisema Dom kabla mama yake hajaingilia na kusema.
Rania.. Tunachelewa sasa...muage Dom twende.
Rania alishindwa hata aseme nini?...alimwangalia tu Dom kisha akamwomba Rai waondoke.
Dom alibaki njia pana..hakujua undani wa jambo lile..alicho sikia hakikutosha kueleza undani wa jambo lile zito
Rania akiwa na Rai wanaelekea kwenye chumba cha siri Rai akasema, sasa si umeona.. Ndio maana sitaki uonane na yeyote maana hii inakurudisha nyuma..ona sasa umekua mnyonge.
Hapana mama..mimi niko sawa tu...alisema Rania.
Basi sitakuruhusu uonane na yeyote kwa saaa hata Fasha..! Alisema Rai.
Waliendelea kwenda hadi wakafika chumbani.
Rania akiwa peke yake aliandika barua ndefu sana ambayo alieleza kila kitu kuhusu suya na yeye..aliandika pia kwamba sio rahisi kutoka salama..Alisema kua maisha yake yako hatarini kwa sababu ya hili maana Suya ni hatari sana.
Mwisho aliomba wamuombee huenda atarudi salama na wataonana tena..hii barua aliandika kwa ajili ya watu wake wa karibu Dom na Fasha.
Baada ya hapo aliificha wala Rai hakuiona.
Kesho yake ndio ilikua siku maalum ya vita kuanza. Rania alitoka na baadhi ya walinzi waaminifu wa Mfalme kuelekea moja kwa moja alikokua Suya. Ila Kabla hawajaanza safari alimuomba mtumishi mmoja aipeleke ile barua kwa Fasha kwa siri sana.
Yule mtumishi alifanya hivyo na kurudi haraka bila kuonekana.
Safari ilianza rasmi ya kwenda vitani.majeshi yote kutoka Lazi na Tharia yalikua yameshakutana.
Huku Suya alikua chumbani kwake peke yake ameandaa silaha zote za kupambana na NADISH. Vita yake kubwa ilikua hiyo.
Baada ya kumaliza mambo yake alitoka ndani na kwenda kukutana na Faritha. Walipanga mpango wao na majeshi yao vyema kwa ajili ya vita.
Baada ya muda kupita tayari majeshi ya pande zote mbili yalikua yameshakutana kwenye uwanja wa vita.viongozi wa pande zote mbili walitoa amri na vita ikaanza.
Ila suya alishangaa baada ya kutomwona bakanga maana yeye ndie alikua mkuu wa majeshi Tharia. Alipata wasiwasi huenda bakanga ameshagundulika na mfalme.
Vita iliendelea kwenye uwanja ule wa damu.
Upande wa Dom na Fasha pamoja na vikosi vyao walibakia ikulu kwa ajili ya kupalinda maana ndo palitamaniwa sana na adui.
Siku hiyo dom alikua amekaa hana amani..mara alikuja Fasha akiwa amehamaki kweli kweli.
Tatizo nini?..aliuliza Dom baada ya kumwona Fasha kwenye hali ile.
Fasha hakuongea..alitoa ile iliyotoka kwa Rania barua na kumpa Dom.
Dom alishtuka sana baada ya kuisoma barua ile...alipata mshtuko mkubwa sana.alibakia anatetemeka mikono.
Haraka aliamka na kwenda alikokua anaishi mama yake. Alipofika wala hakumkuta..aliwauliza watu waliokua pale wakamwambia kua hayupo na hawajui alipo...aaaah...Dom alichoka.
Alirudi pale alipokua Fasha akiwa na Farasi wa vita tayari amempanda.
Unataka kuelekea wapi?..aliuliza Fasha.
Huko walikoenda...alisema Dom.
Hata mimi naenda huko...lakini twende kwanza tukaombe ruhusa....alisema Fasha.
Wala hatutopewa...alisema Dom na kisha akaanza safari huku sehem yake ya kulinda alikua amemwachia msaidizi wake ndo asimamamie.
Fasha alihisi hii ni Hatari zaidi...alimwita jao mlinzi wake na kumkabidhi majukumu ya ulinzi wa ikulu kisha akaondoka na kuelekea alikokua anaenda Dom.
Vita ilikua kali sana...kila sehemu ilikua imejiandaa vilivyo...Mfalme na omandi pia walikua huko ingawa kwa muda huu walikua bado wako kambini pamoja na mfalme wa Lazi wakipanga kuongeza nguvu kama ikihitajika.
Wakiwa wanajadili mara ilikuja taarifa kutoka uwanja wa vita kua kikosi chao kimepigwa na ngome ya kwanza imepokonywa mikononi mwao.
Mfalme wa Lazi na mfalme wa Tharia walichanganyikiwa.
Baada ya muda kilikuja kikosi kilichopigwa huku wengi wao wakiwa wamejeruhiwa vibaya na wengine wamekufa kwenye uwanja wa vita..
Mfalme wa Tharia alijua kuna kosa moja limefanyika...ni kwamba kiongozi wa vita alikua wa Tharia kwenye hicho kikosi. Kwahiyo mbinu zote za Tharia suya anazijua kwakua alikua mtu wa karibu wa bakanga.
Ni kweli..siku chache kabla ya vita bakanga alikua amemtumia suya barua na ramani zote za vita ya Tharia.. Kwahiyo kama kikosi kikiongozwa na mtu kutoka Tharia basi suya atakua anajua.
Mfalme wa Tharia alimwambia Mfalme wa Lazi kuhusu jambo hilo analolihisi ndio limefanya washindwe.
Kwa upande wa Lazi.. Mkuu wa majeshi alikua mtu wa Mfalme kwahiyo njia zote za vita za Lazi zilikua siri kwa maaadui zao.
Walikubaliana kubadili viongozi wa vita isipokua omandi ndie pekee alibaki kutoka Tharia maana yeye hajawahi kufanya kazi na bakanga kwahiyo mbinu zake hawazijui.
Waliuguza majeruhi wao na kujipanga kwa vita tena.
Huku Fasha na Dom walikua wameshafika maeneo ya vita ingawa hawakua pamoja..
Dom alikua amesimama....alipokua amesimama palikua karibu sana na ngome ya kwanza ya kina suya ambayo ndio suya na Faritha walikua humo. Dom yeye hakujua kama yuko karibu na kambi ya adui.
Dom akiwa bado anashangaa mara ghafla alishtuka kuona watu wawili mbele yake..kabla hajafanya kitu walimpulizia dawa fulani iliyomfanya akose kabisa nguvu na kupoteza fahamu muda huohuo.
Wale watu walimkamata Dom na kumpeleka huko kambini kwao wakizania ni mpelelezi wa adui yao.
Upande wa Rania na Rai walikua wako sehemu moja ya siri sana wakifanya ibaada ya kuongeza nguvu za kupambana na Suya.
Baada ya kufanya ibaada ya muda mrefu sana waliamua kupumzika.
Baaa ya mapumziko Rai alienda kuangalia usalama wa wanae.
Alipofika kwenye kioo chake cha miujiza alishtuka kuona alama ya hatari...Rai Alihisi kuchanganyikiwa... Hakujua kama ni Dom au Fasha aliepatwa na tatizo.
Haraka aliingia ndani na kuanza kufanya yake ili agundue tatizo ni nini..
Baaada ya masaa kama mawili hivi alikua meshapata...kioo chake kilimwonesha kila kitu kilichotokea na kinachoendelea kwa Dom hadi sasa.
Rai alishangaa sana...alijiuliza Dom kwanini ameacha kazi aliyopewa ya kulinda ikulu akaja huku?..au ameshajua kila kitu kitakachomtokea Rania?.. Na alijuaje?..
Alitudi kwenye kioo chake na kufanya uchunguzi zaidi..
Hatimae alishuhidia jinsi Rania alivyowapasha habari Dom na Fasha na kuwaeleza yote kwenye barua ile.
Rai alikasirika sana..siku zote alikua akimsisistiza Rania asiwaambia kwa kujua kua wangeweza kuja kumsaidia wakati uwezo huo hawana..na wangeishia tu kuuawa mikononi mwa Suya.
Muda huo Rania alikua amekaa anamsubiri Rai atoke ndani.. Cha ajabu Rai alikua hatoki..Rania alipatwa wasiwasi ila alijifariji kua hakuna baya lolote limempata Rai.
Mara ghafla Rai alitoka ndani akiwa amekasirika sana..Rania alitoka haraka na ili kujua kinachoendelea... Ila Alipokua nasogea karibu zaidi alishtuka kuona Rai alimwangalia kwa hasira sana.
Rania alipatwa na wasiwasi alijiuliza tatizo ni nini..Pole pole alisogea kumuuliza nini tatizo.
Mama kuna tatizo gani?.. Aliuliza Rania kwa hofu.
Rania alishtuka baada ya kupewa bonge la kofi kwenye shavu lake...alibaki haelewielewi nini kinaendelea
Kwahiyo uliniona mimi mjinga sana Nilipokwambia kua usiwaambie Dom na Fasha?... Aliuliza Rai kwa hasira.
Rania alishtuka kuona siri yake imevuja..aliinama chini asijue la kusema.
Utafanya nini sasa kumwokoa Dom ambae maisha yake sasahivi yako hatarini sababu ya ujinga na kutosikis kwako?..aliuliza Rai kwa ukali.
Rania alishtuka sana kusikia Dom yuko hatarini kwa sasa...
Wapi?... Yuko wapi Dom?.. Aliuliza Rania kwa papara.
Kwahiyo unataka kufanya nini kwa mfano?.. Aliuliza Rai.
Mama niambie tafazali.. Nakuomba nielekeze alipo...alisema Rania huku machozi yakimtoka.
Rai alirudi ndani na akafunga mlango kwa hasira.
Rania alibaki pale mlangoni na akilia kumsihi Rai amwambie Dom alipo...masaa yalipita Rania akiwa bado yuko pale analia kumsihi Rai.
Mama nakuomba tafazali.. ..halikua lengo langu mambo yawe hivi...mimi nilitaka tu wajue maana kama ingetokea nikafa huku halafu wewe uliwaficha wangekulaumu na kudai usingeficha wangekuja kunisaidia wakati ni wazi kabisa hawawezi...alijitetea Rania akiwa mlangoni.
Rai akiwa ndani alimsikiliza tu Rania.. Mara ghafla alitoka ndani na kumkuta Rania yuko hapo nje.
Kwahiyo wewe ulipokua unawajulisha uliwaza kua wakipata habari watafanya nini kama sio kuja kukusaidia na kuambulia kufia mikononi mwa Suya?...hilo hukuliwaza?..aliuliza suya kwa ukali.
Nisamehe mama..nimekosea..ila niambie alipo Dom.
Kimya!!!!!...unazani ukienda huko utamsaidia?..na wewe unazani utarudi mzima?..aliuliza suya kwa ukali.
Tafazali mama....naomba.. Alisisitiza Rania.
Rai alihisi hasira zaidi akarudi ndani na kufumga mlango.
Huko Dom alikokamatwa alikaa masaa mengi amefungwa hata baada ya kuzinduka.
Muda anakamatwa suya na Faritha walikua wametoka na kwenda mlimani.. Kwahyo walisubiriwa hadi waje Ndo Dom apate adhabu yake inayomstahili.
Baada ya muda mrefu sana tangu Dom akamwa na wale watu wawili.
Hatimae Faritha na Suya walifika..walipofika tu walipewa taarifa kua kuna mpelelezi wa adui yao amekamatwa.
Safi... Ngoja tukashughulike nae...alisema Faritha.
Walipelekwa hadi Dom alikokua afungiwa..
Waliingia ndani na kumkuta Dom ameinama..
Dom alipoinua uso wake Alisema alishtuka sana baada ya kukutana uso kwa uso na Suya...
Yote hayo Rai alikua akiyaona...ila alishindwa aanzie wapi kizaazaa..alihisi kuchanganyikiwa.. Alimlaumu sana Rania.
Muda huo mvua ilianza kunyesha..Rai aliona afungur mlango ili Rania aingie ndani..
Ila lipofiungua Rania hakuwepo.. Rai alishtuka kidogo.. Alizani labda yuko maeneo yale. Aliita hadi akachoka lakini Rania hakuitika..alitoka na kuanza kumtafuta maeneo yale yote lakini Rania hakuwepo...
Rai alipagawa...alijua tu Rania atekua ameenda kumtafuta Dom anakojua yeye.
Haraka alirudi ndani na kuangalia kwenye kioo chake na kumwona Rania anatembea porini mwenyewe bila uelekeo wowote huku akiangaza huku na kule huku ameshikikia kile kisu cha kumshambulia Suya.
Rai alichoka.....alihisi mambo yameharibika zaidi NINI KINAFUATA?
USIKOSE SEHEMU YA THELATHINI NA SABA
TAZAMA VIDEO HII KISHA BONYEZA SUBSCRIBE CHINI YAKE WAKATI TUKIELEKEA KWENYE MUENDELEZO
TAZAMA VIDEO HII KISHA BONYEZA SUBSCRIBE CHINI YAKE WAKATI TUKIELEKEA KWENYE MUENDELEZO