
SEHEMU YA THELATHINI NA SABA
ILIPOISHIA...
Haraka alirudi ndani na kuangalia kwenye kioo chake na kumwona Rania anatembea porini mwenyewe bila uelekeo wowote huku akiangaza huku na kule huku ameshikikia kile kisu cha kumshambulia Suya.Rai alichoka.....alihisi mambo yameharibika zaidi
SASA ENDELEA..
Mama naomba unisamehe sana...nimeshafanya kosa Mara ya kwanza.. Siwezi kuacha mabaya yamkute Dom kwa ajili ya ujinga wangu... Alijisemea Rania huku akiendelea na safari.Akiwa anatembea mara aliona askari wawili wakitembea..aliwafahamu kua ni watu wa Suya maana alikua akizijua sare zao.
Kwa kujificha alianza kuwafuata nyumanyuma wale watu ili afike alipo Dom na kumwokoa.
Muda huo suya na Faritha walikua wameingia ndani ili kumwona mpelelezi.. Dom alishituka kumwona suya.. Alijua ameisha maana alizani kua suya bado anamkumbuka.
Lakini kwa upande wa Suya yeye wala hakua amemkariri Dom.. Wala hakumkumbuka..ulikua wasiwasi wa Dom tu.
Suya na Faritha walisogeza viti wakakaa karibu na Dom ili kumuuliza maswali.
Wakati huo Fasha alikua akitafuta alipo Dom au Rania bila hata ramani wala maelekezo yoyote yale.
Akiwa anazurura asijue kama yuko karibu na makazi ya suya na yeye aliwaona wale watu wawili wa Suya ambao Rania alikua amewaona wakija tena aliko yeye....alijificha ili asionekane.
Wale watu walimpitiliza bila hata kumwona Fasha.Fasha alipoona wamempitiliza alifurahi.. Mara ghafla alimwona Rania akiwanyatia...Fasha alishituka sana.
Kwa kunyata alisogea na kumshika Rania.
Rania alijua tu amekamatwa...taratibu aligeuka nyuma na kuona aliemkamata.
Alishtuka kidogo na akaondoa wasiwasi baada ya kumwona Fasha.
Rania unaenda wapi?..aliuliza Fasha.
Rania alimweleza Fasha kilichotokea kwa Dom na hali yake kwa sasa.
Fasha aliumia sana moyoni
Kwahiyo unaenda wapi?.. Aliuliza Fasha.
Naenda kumsaidia Dom.. Alijibu Rania.
Hapana Rania usiende huko.. Ni hatari.. Alisema Fasha.
Vipi kuhusu Dom?.. Hata yeye yuko hatarini.. Alisema Rania.
Nitaenda mwenyewe kumsaidia..wewe hauwawezi hata kidogo... Alisema Fasha.
Hapana Fasha.. Hata wewe hawawezi... Alisema Rania.
Fasha alimsihi sana Rania asiende lakini haikuwezekana..kama tu unavyojua Rania alivyo king'ang'anizi.
Fasha aliamua kuondoka kwenda kumsaidia Dom.. Rania nae akaanza kwenda..lakini ghafla walijikuta wameganda..hakuna alieweza kutembea..
Rania na Fasha walichanganyikiwa wasijue la kufanya.. Walihisi suya amewagandisha ili aje awaue.
Walikaa pale kama saa zima wameganda.muda wote walikua wakibishana na kulaumiana tu.
Rania kwanini utoe uhai wako kwa ajili ya hili jambo? Hujui kua kuna watu wanakutegemea?..aliuliza Fasha.
Ndio wapo wananitegemea..ni wananchi wote wa Tharia.. Alisema Rania.
Rania kwanini lakini ujiweke kwenye hatari kiasi hicho.
Fasha.. Mimi ndie nimeanzisha haya yote kwa kutaka kuokoa uzao wa kelkuni.. Kwanini sasa nisiwajibike?..niko tayari kwa lolote.. Nililolianza lazima nilimalize...alisema Rania.
Hapana Rania.. Hata bila wewe uasi ungetokea tu...alisema Fasha.
Waliendelea kubishana sana tu..
Muda huo Rai hakutaka kufanya kosa..haraka alifanya mambo yake ya kiganga kumwokoa Dom alipofungwa..pia kuwaokoa Rania na Fasha waliokua wakikazana kwenda aliko suya wakati hawamuwezi.
Suya alipotaka kuuuliza swali la kwanza mara ulikuja upepo mkali na ndani ya dakika chache tu Dom hakuwepo.
Suya alishangaa sana na kushituka...nani huyu alieingilia himaya yangu???.. Alijiuliza suya ingawa hakutaka kujionesha mbele ya Faritha.
Nini hiki?. Aliuliza Faritha.
Hata sijui...alisema suya kama kweli hajui lolote.
Walishangaa sana.baada ya hapo suya alitoka kwenda kuona nani kamuingilia.
Rai alitokea na kumchukua Dom haraka na kutoweka..nguvu aliyoitumia kwenye jambo lile ilikua kubwa sana kiasi kwamba ilipunguza hata nguvu ya kupambana na Suya.
Mara baada ya muda mrefu kupita alikuja Rai huku akiwa na Dom pale walipokua wameganda Rania na Fasha.
Nyie wajinga mlikua mnazani mnataka kwenda wapi?.. Aliuliza Rai.
Wote walishangaa sana kumwona pale Rai.. Walizani watakua walifungwa na Suya.
Rania usirudie tena..umenigharimu nguvu nyingi sana kiasi kwamba hata zile za kupambana na Suya umezipunguza... Umekosea sana mwanangu.. Alisema Rai.
Rania aliumia sana moyoni.. Alijiona mkosaji mkubwa.. Aliinama chini.
Rai aliwafungulia pale na kuambatana nao Hadi alikokua anaishi yeye na Rania.
Baada ya kufika huko walikaa pamoja.
Mama..nisamehe nimekosea sana...alisema Rania kwa msisitizo.
Huu sio muda wa kuongelea yaliyopita..muda ni mchache sana.. Inabidi tupange njia zaidi za kupambana na Suya... Alisema Rai.
Na Nyie wawili.. Haraka mrudi ikulu.. Hii kazi hamuiwezi hata kidogo.. Yaan mtaishia kufa...alisema suya akiwaambia Dom na Fasha.
Dom na Fasha kwa shingo upande walitii na kuondoka huku wakiwa na mawazo tele juu ya usalama wa Rania.. Hapo bado walikua hata hawajajua kua hata Rai yuko hatarini.. Wakijua sijui itakuaje.
Rai alirudi chumbani kwake na kuweka ulinzi mara dufu ili Suya asije akampata alipo.
Suya alihangaika usiku kucha kumtafuta huyo mbaya wake mpya tofauti na wale wa Baseki lakini haikua Rahisi.
Aliingia kwenye ibaada ya siku kadhaa kujiongezea nguvu na ulinzi na pia amjue mbaya wake.
Rai na Rania nao walifanya ibaada sana kuongeza nguvu na ulinzi ili suya asiwapate haraka kabla wao hawajamuwahi.
Kaasha alikua mnyonge sana tangu siku Rania aondoke na kuwaacha matatani.
Siku zote hizo aliekua akifuatilia maendeleo ya Rania alikua namadi..hivyo hadi sasa walikua wanajua kua Rania yuko vitani ingwa hawakuujua ukweli kiundani zaidi.
Kaasha na pame waliomba kila siku kwa mungu wao Rania apone na arudi salama maana hawakua na ujanja mwingine.
Baada ya hapo vita aliendelea kama kawaida... Hatimae upande wa mfalme wa Lazi na Tharia walipata nguvu na kushinda mapambano mengi zaidi ya kambi ya Faritha na Suya.. Hata hivyo Mfalme wa Tharia hakua na amani maana alijua kazi kubwa na ngumu kuliko zote ya kumuua suya haijafanyika bado.
Wakiwa wanaendelea na vita mara siku moja walitembelewa na wageni..wageni hao ni watu kutoka nchi ya Baseki ambayo iliwahi kuwavamia zama zile.
Wageni walipokelewa vizuri na kukaribishwa kwa mazungumzo zaidi.
Wageni wale hawakua na maneno yoyote yale.. Walikua na barua kutoka kwa Mfalme wao wa Baseki.
Barua ile ilikua inahusu kuomba kushirikiana kwenye vita ile.
Mfalme wa Baseki alikua amewaandikia wafalme wale wawili akiwaambia kua atawasaidia kupambana na Suya maaba suya sio mtu wa kumshinda kirahisi kama wanavyozania.
Mfalme wa Baseki alimfahamu vyema sana Suya na hatari aliyokua nayo.. Na kama suya angeshinda vita hii basi angepata nguvu ya kuwaangamiza au kuwafanya wote wawe chini yake...kwahiyo mfalme wa Baseki alijua hili..kwahiyo alitaka kuungana na hawa ili amwangamize suya..
Hata hivyo Mfalme wa Baseki alikua anapanga baada ya kumwondoa Suya atampora Mfalme wa Tharia na mfalme wa Lazi falme zao na kuzifanya zake.
Baada ya kuusoma ujumbe ule,Mfalme wa Tharia alimwambia mjumbe yule kua asubiri majibu nje.
Wafalme wale na watu wao wa karibu walikaa kujadili swala lile.
Huyu atakua na mambo yake ya siri.. Iweje aombe kutusaidia badala ya sisi kumwomba?..aliuliza Mfalme wa Lazi.
Ni kweli.. Taarifa zake ninazo.
Huyu Mfalme anamwogopa sana Suya. Suya ni hatari sana kwake..kwahyo anataka kuungana na sisi amuue suya lisha hata sisi atupore utawala wetu kwenye nchi Zetu..alisema Mfalme wa Tharia.
Walijadili hapo kwa muda mrefu wakakubaliana kutoshirikiana nao. Waliandika ujumbe wa kukataa msaada ule na kuwapa wajumbe waipeleke kwa Mfalme wa Baseki.
Miaka iliyopita Mfalme wa Baseki aliivamia Tharia.. Ilikua rahisi sana kuiteka lakini kwa nguvu ya Suya Tharia ilipona..kwahyo suya alikua kizuizi kikubwa kwa Mfalme wa Baseki..hivyo mfalme huyo aliapa kumuua suya ili awe huru.
Baada ya kusubiri saba hatimae majibu ya maombi yake yalifika.
Mfalme wa baseki akasema shangaa ba kukasirika sana...aliapa kumuua Suya peke yake na kuwaua wafalme wale wawili waliomdhihaki.
Miaka miwili kamili ilipita..vita ulikua imeendelea sana.. Katika mapambano hayo,majeshi ya pande zote mbili yalikua na nguvu karibu sawa..walikua waeshinda mapambano takribani saba kila upande.
Lilibaki pambano moja tu la mwisho litakaloamua mshindi..katika pambano hili wanajeshi na mashujaa wote wa pande zote mbili walitakiwa kuhudhuria ili na asibaki Mtu nyuma.. Baada ya hili pambano basi vita itaisha.
Siku moja baada ya pambano hilo la mwisho kupita..ndipo kuna pambano kati ya Suya na Rania..
Ilitokea Suya akashinda.. Basi hao wafalme wawili wameisha maana suya atawasambaratisha..ila kama Rania alishinda basi ndio ponapona yao.
Siku ya vita ya mwisho ilifika.
Majeshi yote yaliingia uwanjani..vita ilikua ni kali sana..
Watu wengi walikufa sana..damu ilimwagika sana...mashujaa wote walikuwepo hata Fasha pia. Na Dom nae alikua vitani pia.
Katika vita hii kubwa.. Kuna kijana mmoja alitaja kumuua Mfalme wa Tharia.. Omandi mlinzi wake mkuu alijitolea uhai wake ili Mfalme apone..aliukinga mkuki uliokua umemlemga Mfalme na akafa yeye.
Maskini Mfalme wa Lazi hakuamini macho yake.. Alilia si kidogo.. Hapo alipata hasira na kupigaba kama kichaa.
Ndani ya siku nne vita hiyo iliisha..mfalme wa Lazi na mfalme wa Tharia walishinda ingawa walipoteza watu wengi sana.
Walishinda ingawa walibakia na huzuni maana hata Mfalme wa Lazi alikua amepoteza watu wake wa karibu sana aliowaamini pamoja na asilimia kubwa ya jeshi lake.
Hatimae vita ilibakia kati ya Suya na Rania. NINI KINAFUATA?
USIKOSE SEHEMU YA THELATHINI NA NANE
TAZAMA VIDEO HII KISHA BONYEZA SUBSCRIBE CHINI YAKE WAKATI TUKIELEKEA KWENYE MUENDELEZO
TAZAMA VIDEO HII KISHA BONYEZA SUBSCRIBE CHINI YAKE WAKATI TUKIELEKEA KWENYE MUENDELEZO