RANIA (38)

Zephiline F Ezekiel
JINA: RANIA
SEHEMU YA THELATHINI NA NANE
ILIPOISHIA...
Walishinda ingawa walibakia na huzuni maana hata Mfalme wa Lazi alikua amepoteza watu wake wa karibu sana aliowaamini pamoja na asilimia kubwa ya jeshi lake.

Hatimae vita ilibakia kati ya Suya na Rania.

SASA ENDELEA..
Licha ya kua vita kubwa iliyobakia ilikua kati ya Rania na Suya lakini wanajeshi hawakujua.

Wanajeshi wa Tharia na lazi walizania vita imeisha..lakini ukweli ni kwamba suya alikua na uwezo wa kuwaangamiza kwa kutumia jeshi dogo alilonalo kwakua ni mtu wa miujiza sana.

Mfalme wa Tharia alilijua hilo ingawa bado alikua hajaliweka wazi kwa Mfalme wa Lazi.

Suya akiwa peke yake chumbani alikua akifanya ibaada ya kumwongeza nguvu. Baada ya ibaada yake kukamilika alitoka ndani kwenda kuonana na Faritha ili amwambie hali halisi na mipango na ukuu wake wote alionao.

Alimwita Faritha pamoja na mganga sehemu ya faragha na kuwaeleza yote.

Mganga alistaajabu sana..hakuamini alichokisikia.

Kwanini ulinificha Siku zote hizi?..aliuliza Mganga.

Nisamehe sana mdogo wangu.. Sikuweza kuamini kama ungeweza kuihifadhi siri hii hadi mwisho.. Nisamehe kwa kukosa uaminifu.. Alisema Suya.

Sasa huyo nadishi tukamakamate sasa hivi?.. Maana si umesema unajua alipo...alisema mganga..

Hapana..hamuwezi..hata kama nikiwapa ramani.. Mtaishia kufa tu... Alisema Suya

Hawakua na jinsi... Walikubaliana na hali ya Suya na kusubiri mapambano yatakayoibua ushindi halisi.

Upande wa pili Mfalme wa Tharia alimweleza yote kuhusu suya Mfalme wa Lazi na watu wao wa karibu sana.

Wote walishtuka na kuogopa sana.

Sasa kwanini hukusema mwanzo?..tumepoteza watu wetu kumbe hamna tunachofanya!!!....alisema Mfalme wa Lazi.

Kuna tumaini moja tu...alisema Mfalme wa Tharia.

Lipi hilo?.. Aliuliza Mfalme wa Lazi.

Mfalme wa Tharia aliwaeleza habari za Rania na NADISH.

Angalau walipata ahueni na kurejesha matumaini na kusubiri mapambano.

Wanajeshi wote wa pande zote mbili walitangaziwa vita ile ya kihistoria kati ya Rania na Suya.

Habari Za vita ile zilienea sana hata kwa wananchi..hatimae zikaifikia familia ya Rania.

Kaasha na mwanae pame walisikitika sana na kuzidi kusali kwa ajili ya Rania.

Namadi na Hanna pamoja na Lau walikua na wasiwasi pia.. Siku zote walisali kwa ajili ya usalama wa Rania.

Huko Lazi Mars alikua peke yake chumbani akijuta ujinga alioufanya..alitamani sana kurudi kwa Fasha ila alikosa pa kuanzia.. Alijiona hafai.

Muda wote alikua mwenye wasiwasi juu ya uhai wa Fasha, baba yake Mfalme wa Lazi na kaka yake mwanamfalme wa Lazi.Hakua akipata usingizi vizuri.

Baada ya mawazo ya muda mrefu sana alifanya maamuzi magumu liwalo na liwe.alifunga safari na kuelekea uwanja wa vita ili angalau kujua kinachoendelea huko juu ya watu anaowapenda.

Mfalme wa Baseki na watu wake waliomba sana suya auawe ili wakose mpingamizi ili waje waitawale Tharia na Lazi baadae.

Hatimae siku ya vita ile kali kati ya Rania na Suya ilifika.

Ndani ya muda mfupi wapambanaji walikua uwanja wa vita.

Huku Rai alikua katika ibaada nzito ya kumdhibiti Suya na nguvu zake.

Rania akiwa uwanja wa vita alikumbuka maneno ya mwisho ya Rai Kabla hajaja kupambana na Suya.

Ukifanikisha kumnyakua hiyo pete basi nguvu zake ndio zimeisha ingawa hautaweza kumuua...hiyo pete ndio imeibeba nguvu zake zote.. Alisema Rai.

mara moja pambano lilianza.Suya alitumia nguvu zake zote kupambana na Rania..Rania nae vile vile.

Pambano la kwanza lilichukua mda mrefu sana..kila mmoja alikua na nguvu za kutosha kwa wakati huo.

Baada ya saa zima la mapambano wote wawili walikua chini wamelala hoi.

Suya alikua wa kwanza kuamka..alimtupia kombola moja hatari sana Rania..Rania alizidi kuishiwa nguvu.

Rai alichanganyikiwa kupita kiasi.. Alihisi Rania atashindwa...aliamua kutumia mbinu mpya.

Huko aliko aliamua kutuma kombola kuzuia nguvu za Suya kitendo ambacho huenda kingegharimu maisha yake.

Rai hakujali..aliachia nguvu Zake zote kumshambulia Suya.

Muda huo Rania alikua bado yupo amelala chini hoi.suya alinua mkono kumshambulia tena ili amuue kabisa.. Kabla hajafanya lolote lile alipigwa na kitu kama radi na kushindwa kufanya shambulizi.nafasi hiyo Rania aliitumia vizuri na kumshambulia Suya.

Suya alipoteza nguvu na kuanguka chini.
Haraka Rania alichukua kisu chake na kumwendea Suya aliekua amelala chini ili kuiondoa ile pete.Suya alipoona hivyo alijitahidi akajikakamua kufanya mashambulizi ili amzuie Rania kumshambulia.

Rania alitumia kisu kile cha miujiza na kuikata pete ya suya. Alifanikisha!!..lakini Hata hivyo suya alimtupia kombola zito sana Rania. Rania alianguka chini akawa hali mbaya ya kufa.

Nguvu za suya zilikua zimeisha kabisa... Hakua na jeuri tena.. Alikua chini ameanguka ingawa yeye hakua hali mbaya kama Rania.

Rai alikua ameanguka hali mbaya ila sio sana baada ya shambulizi lile alilolifanya..ila baada ya muda alipata nguvu zake na kuamka kwenda alipokua Rania ili amwokoe maana hapakua mbali sana.

Suya alikaa pale alipo kama nusu sas hivi bila kuamka.muda huo Rai alikua anakuja.

Suya hakua wa kukubali kushindwa kirahisi.. Alichukua mkuki aliokua nao ingawa haukua wa kichawi na kuamka kwenda mummaliza Rania.

Alianza kujiburuza kusogea alipokua Rania amelala.

Alipomfikia aliuinua mkuki ule kwa shida ammalize Rania.. Kabla hajafanya hivyo ulitupwa mkuki mwingine na kuupiga ule wa Suya yote miwili ikaanguka pembeni.

Suya aligeuka kuona nani alietupa ule mkuki...hakuamini macho yake alichokiona mbele yake.. Mtu aliezania kua alishakufa siku nyingi kumbe yupo hai..

Nini?...Amekujaje hapa huyu?..si nilisikia amekufa na wakanihakikishia?..imekuaje?.. Alijiuliza Suya.

Mtu yule alisogea pale alipokua suya na kuchuchumaa karibu yake.

Suya...inatosha sasa..huwezi kuendelea zaidi.... Alisema mtu yule kwa sauti nzito sana.

Suya hakuamini macho yake.. Alizani yanamdanganya.

Muda huo Rai alikua njiani anakuja kwa kasi licha ya hali mbaya aliyokua nayo...NINI KINAFUATA? NI NANI HUYO?

USIKOSE SEHEMU YA THELATHINI NA TISA

TAZAMA VIDEO HII KISHA BONYEZA SUBSCRIBE CHINI YAKE WAKATI TUKIELEKEA KWENYE MUENDELEZO

Chapisha Maoni