RANIA (8)

Zephiline F Ezekiel
JINA:
RANIA
SEHEMU YA NANE
ILIPOISHIA...
Azza fanya mpango haraka utafute wazazi wa huyo Rania wanaishi wapi..akikataa ushirikiano wetu tutawafanyia kitu kibaya....alisema waziri mkuu.

Hilo wazo liko vizuri sana nitahakikisha najua...alisema Azza huku anatikisa kichwa....

SASA ENDELEA..
Lakini mimi naona tumwendee kwanza..akikataa kutoa ushirikiano ndo tutamtishia. Alipendekeza waziri mkuu.

Hapana.. Anaweza kutushtukia akawatorosha.. Inabidi twende na Vyote...alisema Azza.

Kweli...inabidi tuseme hivyo... Alisema mama Azza.

Rania alikwenda rasmi kwenye chumba kilichokua cha mganga na kuangalia maandhari ya mule ndani..kiukweli hapakua pazuri wala, kila kitu kilipangwa hovyo tu.

Mmh..jamani humu ndani..halafu pananuka duuuh...ila itanibidi nipambane tu sasa ntafanyaje...alijisemea Rania.

Alijaribishia mavazi ya mganga na kuchukua vifaa vyake na kuanza kujaribu kama anawanga vile..

Bruuuuu...bruuuu...alifanya Rania huku akirukaruka huku na kule.

Msaidizi wake ilibidi ainame chini acheke maana sio kwa Mganga huyo

Unacheka nini?...aliuliza Rania kwa aibu...

Aaah.. Nisamehe mkuu...alisema msaidizi Rania.

Mfalme, unahisi yule mtoto ataweza kuhimili mkiki ya hawa mafisadi?..aliuliza malikia Najja wa Lazi.

Yule mtoto sio wa kawaida Najj,hateteleki..alisema Mfalme.

Mfalme, mimi hapa ni malikia lakini sina nguvu wala msaada kwako Mfalme wangu...najisikia vibaya sana...alisema malikia wa Lazi.

Usiseme hivyo mke wangu... Wala usijisikie vibaya...alisema Mfalme.

Azza ushafuatilia lile swala?...aliuliza mama Azza.

Ndio mama...nimewaagiza watu na baada ya siku chache nitapata majibu..alisema Azza.

Baada ya siku mbili tayari makazi ya pame na kaasha yalikua yameshajulikana..

Baada ya kupata makazi yao waliona wamemaliza kazi.usiku wake walimfuata Rania kumweleza dili lao.

Rania akiwa amelala mara alisikia mtu akibisha hodi...Rania alikua ashawashtukia kua watakuja...alifungua mlango..

Kulikoni mbona usiku namna hii?..aliuliza Rania.

Ndio muda wenyewe unaotakiwa...alijibu Azza.

Mmh..haya..sema shida...nina usingizi wa kutosha mimi... Alisema Rania.

Wewe binti!!.....unajua unaongea na nani hapa?..aliuliza Azza.

Rania alitabasam shavu moja akasema..wewe ni Azza mwanamfalme wa hii ardhi.

Azza alikasirika ila akaona asilete shida sana maana alikua na dili huo muda.

Ni maongezi ya muda mrefu kidogo kwahyo nakuomba utoke nje kidogo tukae sehemu...alisema Azza.

Enheeee...ndio hivyo sasa unatakiwa kuongea...sio unakuja kwa kasi kama mwanga...aah....alisema Rania

Mmmh....mbona hii kazi ngumu sana?..huyu mtu mbona simwelewi?.....alijiuliza Azza.

Rania alitoka chumbani na wakakaa sehemu na Azza.

***************(katika nchi ya Tharia).************

Dom...unampango gani mwanangu? Naona siku hizi unaoiga mazoezi na kuwinda umeacha...aliuliza mama yake Dom.

Dom aliendelea tu kupiga mazoezi.

Dom mwanangu..njoo basi nina jambo la kukwambia...alisema mama Dom.

Dom ilibidi aache kazi yake akamsikilize mama yake..

Mwanangu, kwanza umekua..halafu una mawazo sana siku hizi...mimi naona uoe ili upate wa kukutuliza...alisema mama Dom.

Kuoa....mama!..sina mpango wa kuoa sasa hivi... Alisema Dom..

Hivi Dom itakuchukua muda gani kumsahau huyo sijui Rania?.. Miaka mingi imepita sasa na uliambiwa amefariki. Sasa una matumaini gani?...oa mwanangu, pengine utaweza kuzoa maumivu ya kifo chake...alisema mama Dom.

Mama...alisema Dom huku amepoa kwelikweli..

Kweli mwanangu, mama yako napenda uwe na furaha siku zote.. Alisema mama Dom.

Najua mama....najua unapenda niwe na furaha.... Lakini nashindwa kua na furaha mama...najilazimisha lakini hamna kitu... Alisema Dom.

Sass utafanya nini Dom?... Muoe hata warid hapo... Utapata furaha mwanangu.

Mama, kufanya hivyo hakutanipa furaha bali nitajikuta namuumiza tu warid...nitakua sawa tu mama....na nikiwa sawa nitaoa tu mama yangu.. Usijali.. Alisema Dom.

Sawa mwanangu mimi nakusikiliza wewe...alisema mama Dom.

***********(NCHINI LAZI)*****************

Mganga, nazani mtukufu Mfalme alishakutaarifu kua tutakuja kukuomba ujiunge nasi...si ndio hivyo?.. Aliuliza Azza.

Nenda moja kwa moja kwenye jambo lililokuleta tafazali..ni usiku sasa.... Alisema Rania

Azza alishangazwa na tabia ya Rania ila ilibidi akaushe tu.

Nimekuja kukutaarifu kua unatakiwa ufuate maagizo kutoka kwangu,waziri mkuu,na mama yangu wala sio mtu mwingine yeyote.. Alisema Azza kisha akatulia kusikia Rania atasema nini.

Hhihii....tse..unafurahisha sana Azza... Alisema Rania.

Huruhusiwi kuniita jina langu..niite kwa cheo..alisema Azza.

Hairuhusiwi kuja chumbani kwa Mganga tena wa kike usiku kwa siri.. Alisema Rania.

Anhaa.. Wewe nakuona unajifanya jasiri sana.. Sio...alisema Azza

Hilo sijajua vizuri... Ila kuhusu ombi sijui amri yako siko tayari..alisema Rania.

Hivi unajua kwamba sisi tuna nguvu kuliko Mfalme?.. Aliuliza Azza.

Hilo sijui wala sio kazo yangu kujua.. Samahani mwanamfalme mimi nakwenda kulala sasa..alisema Rania.

Lakini kumbuka una wazazi...hauhofii usalama wao?. Aliuliza Azza.

Rania kusikia habari za wazazi wake alishtuka sana .macho yalimtoka sio kidogo.

Azza kuona hivyo akafurahi..

Nipe jibu sasa....alisema Azza.

Rania alikaa kimya asijue nini cha kujibu..

Hivi tunavyoongea hapa bila shaka wameshakamatwa na mama yangu.. Uhai wao uko mikononi mwake...na sasa wanasubiri masaada wako watoke...alisema Azza.

Rania alizidi kuchanganyikiwa.. Ghafla aliyajutia maamuzi yake ya kuingia katika vita asio ijua..

Kesho kutwa muda kama huu naomba uje..hakika nitakua nimepata jibu..kwa sasa sijakaa sawa.. Alisema Rania.

Kumbuka ahadi yako Mganga...alisema Azza na kuamka ili aondoke...

Azza Kabla huajondoka nina jambo la kukwambia...alisema Rania huku akitetemeka..

Niambie...Alisema Azza kwa kujigamba..

Naomba kesho uje na mama yako tafazali.. Kama ni kweli anao wazazi wangu naomba aje..kuna jambo kuhusu bibi yangu anatakiwa alijue kwa usalama wa kiafya wa bibu yangu hata wake yeye mwenyewe... Alisema Rania

Niambie hilo jambo mimi nitamwambia..alisema Azza.

Hapana.. Ni aibu kwa mtu wa kiume kulisikia.. Naomba sana.. Alisema Rania.

Sawa usijali hilo umepata...kesho kutwa naijia jibu...alisema Azza.

Rania alitoka pale akiwa na wasiwasi mkubwa sana maana aliwapenda sana bibi na baba yake...

Asante Mungu Azza amenipa muda wa kujipanga..nitafikiria la kufanya.... Alijisemea Rania
****

Vipi..amekubali Mganga?. Aliuliza mama Azza.

Ameanza kwa kukataa lakini nilipomweleza habari ya wazazi wake alishtuka, akasema twende kesho atatupatuia jibu.. Amesema pia niende na wewe kuna kitu anataka kukueleza wewe kuhusu bibi yake kwa usalama wa afya yako.. Alisema Azza

Hilo tu..nitaenda. Alisema mama Azza.

Sass fanya mpango wa kuwakamata maana unajua kabisa hatujawakamata ni mkwara tu.. Alisema mama Azza.

Inaonekana huo ndo udhaifu wake mkubwa...na tutautumia huo kumwendesha ...alisema Azza.

Safi sana...alisema mama Azza.
***

Kesho yake asubuhi Rania aliomba kuonana na mfalme kwa siri.. ..alifanikiwa kukutana nae...

Unasemaje Rania ..?..aliuliza Mfalme..

Mfalme, wazazi wangu wako katika hatari ya kufa kwa sababu nimekataa ombi lao....alisema Rania

Haaa...wameshawakamata tayari? Aliuliza mfalme kwa mshtuko.

Ndio wameshawakamata na wamefichwa kwatika chumba cha siri...alisema Rania.

Mfalme alichoka...alijilaumu kua kwanini hakulifikiria hilo mapema..

Mfalme ... naomba unisaidie kitu kimoja...alisema Rania.

Sema ni kipi hicho?..aliuliza Mfalme kwa pupa.

Naomba niipate pete ya ndoa ya mama Azza.. Uliyomvisha wakati unamuoa...alisema Rania...

Heeee...ya nini??..aliuliza Mfalme kwa mshtuko..

Mfalme, wazazi wangu wako kwenye hatari.. Tafazali usinikatalie mpango wangu huu. Tafazali naomba ....alisema Rania

Sema tu huo mpango wako...Alisema mfalme

Rania alimwelezea mpango mzima Mfalme.

Haaa....umefikiria kwa haraka sana.. Nitahakikisha unaipata pete hiyo kwa gharama yoyote ile na nitakupa....alisema Mfalme..UNAZANI NINI HICHO ANAPANGA RANIA?..

USIKOSE SEHEMU YA TISA

TAZAMA VIDEO HII KISHA BONYEZA SUBSCRIBE CHINI YAKE WAKATI TUKIELEKEA KWENYE MUENDELEZO

Chapisha Maoni