
SEHEMU YA TISA
ILIPOISHIA...
Mfalme, wazazi wangu wako kwenye hatari.. Tafazali usinikatalie mpango wangu huu. Tafazali naomba ....alisema RaniaSema tu huo mpango wako...Alisema mfalme
Rania alimwelezea mpango mzima Mfalme.
Haaa....umefikiria kwa haraka sana.. Nitahakikisha unaipata pete hiyo kwa gharama yoyote ile na nitakupa....alisema Mfalme.
SASA ENDELEA..
Usiku huo Mfalme alihakikisha anatimiza ombi la Rania..alimwamuru mtumishi wake mmoja anaemwamini kumwandalia kinywaji kilichokua na dawa ya usingizi mzito sana.Mtumishi aliileta na kumkabidhi Mfalme. Mfalme bila kuchelewa alikunywa dawa ya kuzuia nguvu za ile dawa ya usingizi halafu akatulia.
Usiku huo Mfalme alimtumia taarifa mama yake Azza (Faritha) kua ndie atakua na mfalme usiku mzima..
Faritha alishangaa sana maana Mfalme alikua na muda mrefu Kabla hajalala nae...alihisi labda ameshabadilika kwakua mambo yamemuwia magumu.
Faritha alikuja na kumkuta Mfalme chumbani.
Weka kinywaji tunywe kwanza..alisema Mfalme.
Faritha alichukua birika lenye kinywaji akatia vikombeni wakanywa..Faritha hakuhisia chochote maana walikunywa kinywaji ambacho kilitoka kwenye birika moja..kwahyo alihisi ni salama tu.
Baada ya kunywa walilala...Faritha alipitiwa usingizi mzito sana..Mfalme bila kuchelewa alimvua Faritha pete ya ndoa na kumvisha nyingne inayofanana na ile lakini haina ile alama ya pete za familia ya kifalme.
Kulipokucha Faritha aliondoka bila kushtukia lolote..
Mfalme bila kuchelewa aliichukua pete na kumkabidhi Rania.
Asante sana mfalme... Nitahakikisha sifanyi kosa...alisema Rania.
Rania alikwenda kumtafuta Hanna ili kumsaidia kwenye mpango wake.
Hanna,najua wewe ni mmbea mzuri sana.. Kama unavyojua yaliyonikuta na wewe ndo rafiki yangu wa pekee..naomba unisaidie kitu hapa... Alisema Rania.
Nini hicho Rania, sema nikusaidie..alisema Hanna.
Naomba usambaze umbea ikulu nzima kua Faritha mke wa Mfalme,mama wa Mwanamfalme Azza jana usiku alikwenda kuzini na mtumishi mmoja wa ikulu... Alisema Rania.
Heee....Mbona hatari jaman?..na nikiulizwa nimejuaje nitasemaje? ..aliuliza Hanna.
Utasema kuna mtu hapa ikulu aliwaona..halafu uongeze kwamba Faritha alipokutana na bwana yake huyo aliivua pete ya ndoa na kuvaa ya huyo bwana maana hampendi Mfalme.
Wakikuuliza zaidi useme kua pete hiyo imeshaokotwa na mtu hapa ikulu ila usinitaje kua ni mimi..sawa eee.. Alisema Rania.
Duuh... Sawa.. Lakin kwani unapanga kitu gani Rania?.. Aliuliza hanna.
Wewe subiri tu utajua... Alisema Rania.
Kwani pete anayo kweli?.. Aliuliza hanna.
Ninayo...ila usiulize ilikotoka maana wewe mmbea sana.. Alisema Rania na wote wakacheka.
Kesho yake tayari ubuyu ulikua umeshasambaa kasri nzima...yaani hiyo ndio ilikua habari ya mjini maana hanna alikua mmbea hatari.
Ndani ya dakika chache tayari taarifa zilimfikia Faritha..
Haaa...nini?. Aliuliza Faritha kwa mshangao mkubwa sana.
Nani anazusha uongo huu?..aliuliza Faritha kwa hasira.
Sijajua ni nani..ila habari ndo hizi nimeshazipata...alisema mtumishi wa Faritha ingawa na yeye alikua kundi mpja la wasambaza ubuyu.sasa
Faritha alibaki ameshangaa asijue la kufanya.
Nani lakini huyu?.. Ananitafuta nini lakini?..alijiuiza Faritha.
Mama...tulia tu...tutatafuta ufumbuzi wa hili tatizo... Alisema Azza.
Kweli kabisa.. Tulia tu Faritha... Alisema waziri mkuu.
Siku hiyo ilipita..ubuyu ulikua umeshasambaa kwa kiasi kikubwa..Faritha aliangaliwa kama kinyesi kila alipopita.ilimbidi aingie ndani ajifungie mlango maana mambo si mambo tena
Muda wa kukutana na Rania ili awape jibu ulifika.. Azza na mama yake walikwenda alikokua Rania.
Haya..hatuna muda..tupatie jibu..umekubali kuungana na sisi?. Aliulza Azza
Sijakubali na wala sikubali....Alisema Rania.
Sawa.. Baba na bibi yako utawasahau...alisema Azza.
Hata wewe na mama yako ufalme mtausikia kwa jirani..alisema Rania.
Haa..haahaaaaa....nini?... Eti sisi??..suburi uone...nitahakikisha unakua hai na utaona ninavyokua mfalme... Alisema Azza huku akiinuka na kutaka kuondoka.
Je hujui kwamba kama mama yako akitolewa kwenye cheo chake cha mke wa Mfalme wewe hautakua na kibali cha kua mrithi?.. Hujui?..aliuliza Rania.
Faritha alishtuka.
Nini?... Niondolewe na nani? Kwanini?..aliuliza Faritha.
Nasikia umezini na umeitupa pete ya ndoa...alisema Rania.
Hahaaaaaa..kwahyo ndo umeacha bibi na baba yako wafe ukizani nitatishika na habari hizi za uongo?.. Pole sana..hakuna wa kunitoa na hakuna alie na ushahid kua nimezini hata mfalme anajua sijazini...alisema Faritha kwa majigambo..
Faritha, hebu angalia vizuri pete yako uliyoivaa..hapo nazani tutaelewana..alisema Rania.
Faritha hakuamini macho yake baada ya kukuta pete aliyonayo si halisi.. Ni chakubumba..
Kwahyo wewe ndo umefanya haya sio?...aliuliza Azza.
Una dakika chache sana za kufanya maamuzi... Pete yako iko mikononi mwangu.. Ama sivyo unajua yatakayokukuta?.alisema Rania.
Nitakuumbua kua umezusha wewe.. Alisema Faritha.
Unazani wa taamini?...pole sana ..alisema Rania
Faritha alikasirika sana..kwa hasira aliondoka na kwenda..
Mama tunafanya nini?..aliulza Azza akiwa yeye na mama yake na waziri.
Huyu Rania mjinga kweli...ameamua kushirikiana na mfalme.. Alisema Faritha.
Mfalme?.. Kiaje? Aliuliza Azza.
Wewe unazani Rania ameipata wapi hiyo pete?..Mfalme ndo alinibadilishia na kunivisha pete chakubumba nikiwa usingizini..alisema Faritha.
Hatuna jinsi... Kwa leo ametushinda..alisema waziri.
Nani kasema??...sijashindwa mimi..nikiitwa kwenye baraza nitasema ukweli kua mfalme na Rania wamenifanyia hira.
Utakua umejivunia kosa la kumsingizia Mfalme na kumzaririsha..hata hilo litakufanya uukose umalikia. Alisema waziri.
Faritha alikasirika zaidi... Zaidi yani.
Sawa.. Leo nimekubali...ila Rania atanijua.. Labda sio mimi...aliapa Faritha.
Na mfalme atalipa juu ya hili...ameamua kunifanyia hivi. Subiri. Alisema Faritha.
Baada ya siku chache kila kitu kiliisha chini kwa chini.. Rania alirudishiwa wazazi wake na Faritha alirudishiwa pete yake na mambo yakawa kimyaaaaa.
Rania mwanangu, hutakiwi kuendelea kukaa hapa..nitakufa kwa mawazo baba yako...alisema pame.
Sawa baba..nitaondoka muda sio mrefu...alisema Rania..wazazi wa Rania walipelekwa nchi ya mbali kwa msaada wa Mfalme kwa ajili ya usalama wao.
Azza, tunafanya nini juu ya hiko kikwazo?.. aliuliza waziri.
Hatuna njia nyingine tofaut na hii..kumuuua tu.. Alisema Azza.
Kweli....Kiufupi hashawishiki yule.. Hata tufanye nini... Alisema Faritha.
Wazo zuri sana...tutafanya kazi hii kwa umakini.. Ngoja upepo utulie..alisema Azza.
Rania, we ni mwerevu..nashukuru sana kwa msaada wako. Alisema Mfalme.
Nashukuru pia kwa msaada na ushirikiano wako Mfalme.. Alisema Rania.
Lakini najua watakua wanapanga kuniua...alisema Rania
Najua hilo...nimefikiria sana nikaona hili ni jema zaidi kama ukifanya
Rania, sipendi uzidi kuhatarisha maisha yako kwa ajili yangu na ufalme huu tena...naomba uondoke kwa amani kabla hawajakutafuta. Alisema Mfalme.
Cha kufanya acha umetoa ujumbe wa kumchagua mrithi wa kiti cha ufalme, mwanangu Asa niliezaa na malikia Wangu.
Hapo kila kitu utakua umemaliza maana hawa watu wakorofi sana..alisema Mfalme.
Halafu ndo nitasema naenda wapi?..aliuliza Rania.
Sema mizimu imekuamuru uende milimani ukae huko siku 56 ukiomba kwa ajili ya nchi hii isipatwe na janga..Halafu utasema imekwambia usimtaarifu Mtu wakati unaondoka na maelezo ya ulipoenda uyaandike tu. Alisema Mfalme.
Sawa Mfalme.. Alisema Rania baada ya kuona holo wazo ni zuri.
Kama walivyopanga...Rania alipanga safari na kuuandaa ujumbe ule alioagizwa na mfalme... Aliandika pia ujumbe ww kumuaga rafiki yake Hanna.
Usiku ulipoingia alianza safari na akafanikiwa kutoka ndani ya kasri salama na kuanza safari rasmi akiwa na walinzi wawili shupavu kutoka kwa Mfalme.
Rania alikua njiani akiangalia jinsi palivyo na giza nene..alitabasam na pia alihuzunika kuiacha nchi ile nzuri aliyoizoea...
Alisafiri umbali mrefu ingawa sio sana maaba hakua na kasi kubwa sana..
nini wewe?..Rania hayupo kwenye kasri ameondoka?. Aliuliza Faritha kwa hasira baada ya kupata habari hizo kutoka kwa shushushu wake.
Ndip mkuu..alisema mtumishi..
Faritha na wenzie bila kuchelewa waliagiza wapambanaji mashuhuri wawili kumfuatilia Rania..Nini kianfuata?..
USIKOSE SEHEMU YA KUMI
TAZAMA VIDEO HII KISHA BONYEZA SUBSCRIBE CHINI YAKE WAKATI TUKIELEKEA KWENYE MUENDELEZO
TAZAMA VIDEO HII KISHA BONYEZA SUBSCRIBE CHINI YAKE WAKATI TUKIELEKEA KWENYE MUENDELEZO