RANIA (8)

Zephiline F Ezekiel
RANIA (8)
JINA: RANIA Mtunzi: Teddy Mibaraka SEHEMU YA NANE ILIPOISHIA... Azza fanya mpango haraka utafute wazazi wa huyo Rania wanaishi wapi..akikataa ushirikiano wetu tutawafanyia kitu kibaya....alisema waziri mkuu. Hilo wazo liko vizuri sana nitahakikisha najua...alisema Azza huku anatikisa kichwa.... SASA ENDELEA.. Lakini mimi naona tumwendee kwanza..akikataa kutoa ushirikiano ndo tutamtishia. Alipendekeza waziri mkuu. Hapana.. Anaweza kutushtukia akawatorosha.. Inabidi twende na Vyote...alisema Azza. Kweli...inabidi tuseme hivyo... Alisema mama Azza. Rania alikwenda rasmi kwenye chumba kilichokua cha mganga na kuangalia maandhari ya mule ndani..kiukweli hapakua pazuri wala, kila kitu kilipangwa hovyo tu. Mmh..jamani humu ndani..halafu pananuka duuuh...ila itanibidi nipambane tu sasa ntafanyaje...alijisemea Rania. Alijaribishia mavazi ya mganga na kuchukua vifaa vyake na kuanza kujaribu kama anawanga vile.. Bruuuuu...bruuuu...alifanya Rania huku akirukaruka huku na kule. Msaidizi wake ilibidi ainame chin…