RANIA (9)
JINA: RANIA Mtunzi: Teddy Mibaraka SEHEMU YA TISA ILIPOISHIA... Mfalme, wazazi wangu wako kwenye hatari.. Tafazali usinikatalie mpango wangu huu. Tafazali naomba ....alisema Rania Sema tu huo mpango wako...Alisema mfalme Rania alimwelezea mpango mzima Mfalme. Haaa....umefikiria kwa haraka sana.. Nitahakikisha unaipata pete hiyo kwa gharama yoyote ile na nitakupa....alisema Mfalme. SASA ENDELEA.. Usiku huo Mfalme alihakikisha anatimiza ombi la Rania..alimwamuru mtumishi wake mmoja anaemwamini kumwandalia kinywaji kilichokua na dawa ya usingizi mzito sana. Mtumishi aliileta na kumkabidhi Mfalme. Mfalme bila kuchelewa alikunywa dawa ya kuzuia nguvu za ile dawa ya usingizi halafu akatulia. Usiku huo Mfalme alimtumia taarifa mama yake Azza (Faritha) kua ndie atakua na mfalme usiku mzima.. Faritha alishangaa sana maana Mfalme alikua na muda mrefu Kabla hajalala nae...alihisi labda ameshabadilika kwakua mambo yamemuwia magumu. Faritha alikuja na kumkuta Mfalme chumbani. Weka kinywaji tunywe kwanza..alisem…