
SEHEMU YA THELATHINI NA TISA
ILIPOISHIA...
Suya hakuamini macho yake.. Alizani yanamdanganya.Muda huo Rai alikua njiani anakuja kwa kasi licha ya hali mbaya aliyokua nayo.
SASA ENDELEA..
Suya..Muda ukifika umefika..huwezi kupeleka mambo yote kama wewe utakavyo kwakua dunia sio yako..alisema Mtu yule.Kumbe uko hai.. Kwahiyo nilidanganywa!...alisema Suya.
Hauna muda wa kufikiria hilo..haitabadili kitu.. Alisema mtu yule.
Hata kwako haina faida yoyote ya wewe kurudi...alisema Suya.
Ipo faida.. Mke wangu na watoto wangu wawili watakua wanahitaji kuonana na mimi bila shaka... Alisema mtu yule.
Watoto wawili?... Wawili?... Aliuliza Suya kwa dharau.
Hakuna siri zaidi kua Mwanamfalme Fasha sio mtoto wako wa kuzaa...alisema Mtu yule.
Funga mdomo wako!!!...alisema suya kwa ukali.
Sawa nafunga..ila huo ndio ukweli... Alisema mtu yule.
Suya alikasirika sana...alihema kwa hasira.
Hata kama huo ndo ukweli.. Mfalme hatakubali kirahisi na wala hajui...alisema Suya.
Hadi nakuja hapa..najua kila kitu..kwahiyo wala usijisumbue kunidanganya...alisema mtu yule.
Wakiwa wanabishana mara ghafla alifika Rai.
Habiri aligeuka kuona ni nani aliekuja hapo.
Rai alishituka sana kwa alichokiona mbele yake.. Hakutaka kuamini hata kidogo.
Habiri alitulia tu ili kumpa Rai muda wa kushangaa.
Suya alitaka kutumia muda huo na nafasi hiyo kummaliza Rania lakini kabla hajafanya kitu habiri alimdhibiti tena
Mchukue Rania uondoke nae mengine utaelewa baadae...alisema habiri akimwambia Rai lakini Rai alikua bado anashangaa.
Rai!!!... Aliita Habiri.
Rai alishituka na kumchukua Rania na kuondoka nae.ila kabla hajaondoka aligeuka na kumwangalia Suya kwa hasira.
Hakika sitakuacha salama..alisema Rai.
Kwanini labda.. Alisema Suya.
Nimeishi maisha mabaya sana kwa ajili ya uovu wako..nimeshi nikimlilia mwanangu kumbe yuko hai..yote ni wewe...na mme wangu Vilevile.. Alisema Rai.
Sasa huoni kua nilikusaidia kulea?..aliuliza Suya.
Kwani nilikwambia nahitaji msaada?.. Aliuliza Rai.
Nitamfanya Fasha asikupende hata kama akikujua...alisema Suya.
Umeshachelewa...alisema Rai na kuondoka.
Suya roho ilimuuma sana.. Alihisi huenda Fasha ameshafahamiana na mama yake..na ndio ilikua hivyo.
Rai na Rania walipofika mbali kidogo habiri aliondoka na yeye akawafuata huku akiacha amempora Suya mkuki wake.. Suya alibakia amelala chini.
Mganga na Faritha waliposikia hatima ya vita ile walihisi kuchanganyikiwa.
Haraka Mganga alienda alipo suya na kukuta amelala chini.
Dada...aliita Mganga huku machozi yakimtoka.
Suya alimwangalia mdogo wake kwa jicho la huruma na yeye machozi yakimtoka.
Nisamehe mdogo wangu.. Nimeshindwa kupambana na hatimaye tumepoteza uelekeo... Alisema Suya.
Hapana Dada.. Hatujapotea...bado kuna tumaini.. Alisema Mganga Dasu.
Dasu alimchukua dada yake na kuondoka nae kuelekea kambini.
Ilikua huzuni kubwa sana kwa wanajeshi wa Suya na Faritha waliobakia..walivunjika moyo kabisa.
Suya aliomba abakie peke yake kwa muda usiku mzima maana akili ilikua haijakaa sawa.
Huku Rai alimfikisha Rania sehemu ile waliyokua wakiishi.. Hali ya Rania ilikua mbaya sana..hapakua na tumaini la hakika juu ya kupona kwake.
Rai alikua mwenye mawazo mengi kupita kiasi.
Baada ya muda mfupi habiri aliingia..
Rai,nisamehe mke wangu kwa kuchelewa sana...alisema habiri akiwa pembeni anaongea na Rai.
Muda wote Rai hakutoa macho yake kwa habiri..alihisi kama ndoto kumwona tena.
Ilikuaje?.. Aliuliza Rai.
Yule alietumwa kuniua alinihurumia na akaniambia niondoke zangu niende mbali nisije nikaonekana na Suya kamwe...alisema habiri.
Rai alimkumbatia mmewe huku machozi ya furaha yalimtoka.. Alikosa hata cha kuongea kwa muda huo.
Muda huo si Dom wala Fasha aliekua ametulia..wote walikua na wasiwasi sana juu ya Rania.
Wakiwa ikulu mara taarifa ya ushindi ule iliwafikia..walifurahi mno wakijua kua sasa Rania yuko salama..walitarajia baada ya muda mfupi Rania atakuja na watamwona tena.
Huku kwenye kambi za jeshi la muungano wa Tharia na lazi walifurahi pia kutokana na ushindi ule mkubwa walioupata...vita ilikua imeisha ingawa kulikua na hofu kua watu wa Suya na Faritha huenda wakaleta vurugu baada ya jeshi la muungano wa Tharia na lazi kuondoka.. Kwahiyo waliendelea kuwepo kwa muda kidogo.
Baada ya siku mbili Rania alipelekwa ikulu.. Hali yake ilikua ya kutatanisha..Rai alikua ameshatibu hadi basi lakini Rania hakuonesha unafuu wowote.
Ilikua ni simanzi kubwa hasa kwa Dom, Fasha na familia ya Rania.
Wataalamu mbalimbali wa tiba walijitahidi kumtibu lakini wapi..hali yake iliendelea kua mbaya tu.
Rai alichunguza sana tatizo la Rania na kugundua kitu kimoja.Suya alimpandikizia sumu ya kumwangamiza ndani ya siku kumi.. Kwahiyo ili aishi basi inatakiwa ibaada nzito kwa ajili yake itakayohusisha pete ile ya Mganga wa kwanza wa Tharia.ibaada hii ambae huifanya hua sio rahisi kupona..mara nyingi ni kufa kwa ajili ya kumpa mtu maisha.
Mfanya ibaada ile lazima awe Mtu wa karibu na mhanga wa tatizo. Rai alihofia kuitoa siri hii akihofia nani atakubali kujitoa.
Alihisi labda huenda Dom au Fasha wakajiweka kwenye hatari hii baada ya kupata habari hizi.
Bila kumshirikisha Mtu yeyote yule aliingia na kuamua kuifanya ibaada ile yeye mwenyewe.. Hakumwambia hata mmewe maana alihofia mmewe asingekubali..kabla hajaingia kufanya ibaada ile alimwita Dom na Fasha na kuwatambulisha kwa baba yao maana hakua na uhakika wa kuishi tena.
Wote walifurahi na walitaka kujua zaidi kilichotokea hadi baba yao akafika alipo sasa.
Baada ya hapo Rai alitoka na kwenda kufanya ibaada ile.
Usiku wa siku ile mara ghafla Rania alipata nafuu..wauguzi wake waliokua wamekata tamaa walishangaa sana.. Haraka walienda kutoa taarifa kwa watu.
Taarifa zile zilipomfikia habiri alishangaa na kushituka..alihisi Rai kafanya kitu hatari. Haraka alianza kumtafuta ila hakumpata kirahisi.
Baada ya kuzunguka sana aliingia kwenye chumba kimoja na kukuta Rai amelala chini ndani ya chumba kile.
Habiri alianza kumwamsha Rai. Kwa taabu sana Rai alimgeukia habiri na kumwangalia huku machozi yakimtoka
Nisamehe mme wangu sikua na njia nyingine ya kutatua jambo hili.. Alisema Rai kwa taabu sana.
Habiri hakutaka kuchelewa.. Alitoa dawa fulani na kumpakaa Rai kichwani...Rai alipata nguvu hapo hapo.
Habiri ,Rania.... Alisema Rai kabla habiri hajamkatiza.
Hapa mmegawana uhai..nyote mmepata nafuu ila mtapona baada ya miaka kama mitano hivi baadae. Hakuna namma ya nyote kupona..hapo mmoja atakufa.ila kwa njia hii nyote mtaishi ila itawachukua muda kupona kabisa...Alisema habiri.
Ulipata wapi huu ujuzi?..aliuliza Rai.
Habiri alitabasam tu na kumkumbatia Rai.
Hata huko Rania hali yake haikubadilika..aliendelea na nafuu yake ingawa si kupona jumla.
Wauguzi walimtoa ndani..Alikaa nje akipungwa upepo bila kusema chochote.
Dom akiwa nje mwenye mawazo baada ya kukosa usingizi mara aliona mtu akiletwa nje..alishangaa kuona ni Rania.
Haraka alifika alipokua Rania ili athibitishe..ni kweli alikua ni Rania. Dom alifurahi sana.. Bila kusema chochote alisogea na kuja kumkumbatia Rania..
Rania nisamehe kwa kuchelewa kufika hapa... Alisema Dom huku machozi ya furaha yakimtoka.
Rania imekuaje umepona ghafla?.. Aliuliza Dom kwa pupa.
Rania alimjibu kwa ishara kua hajui.
Dom hakua amegundua bado... Aliendelea kumuuliza Rania maswali lakini cha ajabu Rania alikua akijibu kwa ishara tu.
Hapo ndipo Dom alishtuka..alimwangalia Rania kwa mshangao.
Rania huwezi kusema?. Aliuliza Dom.
Kwa ishara Rania alikubali kua hawezi kuongea.
Daah..Dom aliumia sana moyoni mwake...machozi yalimtoka kwa kasi.
Utapona tu Rania.. Naamini utaweza kusema tena.. Alisema Dom huku amemuweka Rania kifuani kwake machozi yakimtoka.
USIKOSE SEHEMU YA AROBAINI
TAZAMA VIDEO HII KISHA BONYEZA SUBSCRIBE CHINI YAKE WAKATI TUKIELEKEA KWENYE MUENDELEZO
TAZAMA VIDEO HII KISHA BONYEZA SUBSCRIBE CHINI YAKE WAKATI TUKIELEKEA KWENYE MUENDELEZO