RANIA (40)

Zephiline F Ezekiel
RANIA (40)
JINA: RANIA Mtunzi: Teddy Mibaraka SEHEMU YA AROBAINI ILIPOISHIA... Daah..Dom aliumia sana moyoni mwake...machozi yalimtoka kwa kasi. Utapona tu Rania.. Naamini utaweza kusema tena.. Alisema Dom huku amemuweka Rania kifuani kwake machozi yakimtoka. SASA ENDELEA.. Dom umeshamwona Rania?.. Nasikia ameamka..aliuliza Fasha kwa pupa lakini Dom alionekana mnyonge sana. Nini tatizo kwani?..aliuliza Fasha baada ya kuona Dom amepoa. Rania ni kweli amezinduka..lakini.. Alisema Dom kisha akasita. Nini kwani?... Mbona umesita?..aliuliza Fasha. Hawezi kuongea.. Alisema Dom. Fasha alishangaa sana na kuhuzunika..haraka alikwenda alikokua Rania ili ajihakikishie. Rania... Aliita Fasha kwa sauti ya upole. Rania alitabasamu tu na kuitika kwa kutikisa kichwa. Fasha aliumia sana...alijua yote Haya yamempata Rania kwa ajili ya nchi.. Kwa upendo alisogea ba kumkumbatia huku akimpa maneno ya faraja. Upande wa Rai pia hali haikua nzuri sana..alikua mzima sehemu zingine lakini hakuweza kutembea. Yalikua maumivu ndani ya ile f…