AISEE KUMBE RAHA (20)

Zephiline F Ezekiel
Mwandishi: Pablo

SEHEMU YA ISHIRINI
"Hivi david wewe na baba mko vipi maana urafiki wenu sijaonaga aisee."Nikajikuta nikimuuliza david swali ambalo baada ya kulisikia akaachia tabasamu kidogo kisha akaniangalia na kuanza kusikitika.

SASA ENDELEA...
"Baba yako amenisaidia vitu vingi maana baba yangu mimi alikuwaga anafanya kazi kama ya baba yako hiyo ya magali.Sasa katika familia yetu nipo peke yangu yani baba na mama kisha na mimi na baba na mama wote hawakuwa labda na watoto nje ya ndoa sasa Mama akafariki ghafla miaka kama kumi nyuma alipokufa mama haikupita hata miezi miwili baba akapata ajali naye akafa sasa sikuwa na kimbilio lolote ndipo baba yako sasa akachukua jukumu la kunilea akanitengenezea Mazingira mazuri hapa morogoro akaniwekea watu wakuniongoza Aisee nimepiga sana pesa kwa hiyo mimi baba yako ni baba yangu kwa sababu daaaah amenisaidia kama mwanae yani."
"Daaah aisee pole sana."
"Ila pablo leo sitaki kukuchosha ila kesho nataka uniambie umefanya nini dar maana baba yako aliniambia ulifanya kitu ndio maana."
"Nitakwambia david wewe kaka yangu."Hakika mimi na davidi tuliongea mengi mno na tulipofika katika sehemu wanapouza chips mimi nikanunua sahani mbili ambayo moja nitakula mchana huo nyingine usiku kisha nikamsindikiza david kituoni ambapo yeye akaniaga na mimi nikarudi nyumbani pale ambapo nilianza kuishi maisha mapya ya kuwa peke yangu maisha ambayo niliyatamani sana.kutokana na uchovu mkubwa niliokuwa nao haikupita hata muda mwingi baada ya kula tu nikajikuta nikipatwa na usingizi wa nguvu ambao ulisababisha nilale mpaka mida ya jioni ambapo nilishtushwa na mlio wa simu simu ambayo nilipoangalia nani anapiga alikuwa ni mama yangu ambaye niliongea naye mengi huku akiniambia kuwa alikuwa amenimiss sana.Baada ya kumaliza kuongea naye mwanaume nikajikusanya nikavua zote na kuvaa taulo tu kisha nikachukua mswaki wangu nakuuweka mdomoni kisha nikachukua na maji ambayo yalikuwepo mule ndani na nikatoka nje haraka na kuelekea chooni ambapo nilielekezwa tu.Ilikuwa ni mida ya jioni na kigiza giza kilikuwa kinaingia na taa mulemule tayari zilikuwa zishawashwa.Lakini kabla sijaingia katika chumba cha choo nikiwa nje ya mlango wa choo ambavyo vilikuwa vitatu ghafla sisimizi akanitambaa haraka kuanzia mguuni na kuelekea mapajani ambapo nikajikuta haraka nikajikuna kwa kutumia mkono lakin ghafla mswaki wangu uliokuwepo ukaniponyoka na kuanza kudondoka Mwanaume sikutaka kuruhusu hali ile haraka nikaanza kutaka kuudaka ule mswaki la haulaa bahati mbaya taulo nililolivaa likanivuka na kudondoka chini na sikuvaa kitu chochote msumali wangu ulikuwa umesimama barabara haraka haraka nikanyanyuka nikachukua taulo langu na kulivaa kisha nikauchukua mswaki wangu ambao licha ya nguvu zote lakini ukanidondoka.ile najiweka sawa tu baada ya kumaliza kuliweka taulo ghafla nikakutana uso kwa uso na rozinta ambaye nilimuona amesimama na kushababisha nigande kumuangalia.
"Heee ameniona nini??"nikajikuta nikijiuliza swali ambalo halikuwa na jibu..............


Macho yangu yalizidi kumuangalia rozinta kwa hofu baada ya tukio lile ambalo wala sikutegemea kama lingetokea kwa wakati ule.lakini kilichozidi kunichanganya na kusababisha nigande tu na kushindwa kunyanyua mguu kutembea ni jinsi rozinta alivyokuwa akiniangalia kwa macho flani ya kimahaba na bila ya hofu wowote katika macho yake yeye aliendelea kunikazia macho huku naye akiwa amesimama mkononi akiwa ameshika ndoo yake ya maji ambayo alikuwa ametoka naye chooni na alionyesha wazi alikuwa ametoka kuoga na alikuwa amevaa kanga tu.
"Aaaah pablo mbona uendi kuoga wangu wee ingia humo hamna watu vyoo hivyo viwili."rozinta akavunja ukimya akaniambia huku akitabasamu na mimi nikajifanya nikitabasamu kinafiki na kupiga hatua huku nikimuangalia rozinta kwa macho ya kuibia ibia na nikaingia chooni na kufunga mlango ule wa chooni.

"Mmmh ila rozinta ana shepu ya ukweli halafu mweupe sasa ana macho mazuri yani ananitamanisha daah."Nikajikuta nikijisemea kimoyomoyo wakati nilipojimwagia maji kopo la kwanza kisha nakuanza kujipaka sabuni huku bado nikiwa namuwazia yule rozinta ambaye pia alikuwa amenipa wakati mgumu sana kwasababu sikujua kama kweli alikuwa ameona msumari wangu ambao ulikuwa bado umesimama kutokana na kuona picha ya umbo la rozinta katika macho yangu.
"Weee pablo mi nakuambia morogoro sio dar kumbuka huko ugenini utakuja kurogwa ohoo shauri yako kuwa muangalifu."Maneno ya mama yalinijia haraka kichwani mwangu wakati bado naoga nakujikuta nikiacha kuoga na kuanza kutafakari sana juu ya maneno ya mama ambayo alinisisitizia sana kuwa niache maswala ya wanawake jambo ambalo hata baba naye alitia nakshi nakshi na kunikanya kuwa muangalifu kuepuka na hali ile.

"Mmmh lakini mimi mwanaume bana nitawezaje kujizuia kuchinja wakati mimi mwanaume nasimamisha vizuri tu daah."Nikajikuta nikishindana na nafsi mbili ambazo zilikuwa tofauti moja ilikuwa imesimamia mawazo ya mama ambayo aliniambia kuwa niachane kabisa na mambo ya wanawake na nafsi nyingine ilikuwa imesimama kuwa nisijari maneno ya mama na niliwafanyie kweli warembo ambao walikuwa ndani humo huku nikianza kumshughulia kwanza rozinta ambaye nilikuwa nina mshuku kuwa alikuwa ameniona wakati taulo liliponidondoka kwa bahati mbaya.Baada ya kuwaza sana nikajikuta nikiyapuuzia yote kisha nakuanza kuoga haraka haraka kwa maana giza lilikuwa linaingia na nilikuwa nimepanga nioge haraka kabla hata giza alijazama.Kwa muda wa dakika tano nikautumia kwa kusafishwa mwili wangu ambao ulikuwa na uchovu na safari na nilipomaliza nikatoka mule chooni.lakini ghafla nikakutana uso kwa uso na msichana mwingine ambaye alikuwa mara ya kwanza amekaa kati ya wale waliokuwa watatu pamoja na mwenye nyumba na ndio yule aliyekuwa akinitetea kuwa nisifanye usafi na kwamba angefanya usafi yeye wote.baada ya kukumbwa na hali ambayo eti yeye alitaka kuingia katika choo kile na kujikuta nikijiuliza swali kwamba je huyu mwanamke ajasikia maji.

"Hee samahani bwana nilikuwa najua eti humu hamna mtu aaa kichwa hiki kinamawazo."yule mwanamke akaniambia vile huku akinionea aibu kwa kuangalia angalia chini huku akiburuza mguu wake chini kama vile nilikuwa namtongoza pale mlangoni.
"Usijali dada yangu mawazo kwa kila mtu yapo daima hatutoweza kuyazuia mawazo."Na mimi nikajitutumua kumwambia yule mwanamke ambaye baada ya kuniambia vile akaniangalia kwa jicho flani hivi ambalo lilinifanya nishtuke lakini sikuonyesha mshtuko huo ila moyo ukaanza kunidunda kwa kasi baada ya kunionyesha silaha yake ya urembo kuniangalia kule kulinifanya sasa nione urembo wake na hata nilipomtathimini nikaja kugundua naye alikuwa amejaaliwa sema hakumzidi rozinta kwa shepu na yeye pale alikuwa amevaa kanga na alikuwa na ndoo ya maji aliyokuwa ameshika mkononi mwake.

"Sawa jamani kaka yangu ila mimi usiniite dada me naitwa sabra bwana."
"Anha sawa sabra basi acha niende kupumzika maana nimechoka kwa uchovu wa safari."Nikamaliza mazungumzo kati ya mimi na yule mwanamke aliyeniambia jina lake kuwa alikuwa anaitwa sabra na nikamuacha yeye akiingia chooni na mimi haraka nikakimbia haraka haraka nakuingia katika chumbani kwangu ambapo nilijibwaga kitandani na kuanza kuwaza na kuwazua na kuendelea bado kujiuliza maswali ambayo hayakuwa na majibu sahihi.baada ya kuwaza sana nikanyanyuka na kuwasha television ili kupoteza mawazo ya yale mambo yaliosababisha mpaka nifike pale lakini hata television sikuangalia sana kwa sababu niliona ilikuwa hata hainisimui na kujikuta nikitulia kitandani tu nakuenda kuwaza.Nikiwa katika mawazo mengi simu yangu ya mkononi ikaita taratibu nikaichukua nakuangalia mpigaji alikuwa ni Mama yangu hali ambayo ilisababisha nitabasamu baada ya kuona simu yake.

"Nambie mama yangu yani nimekukumbuka sana."
"Aaaa mwanangu hata mimi lakini ndio hivyo jifunze kuishi popote mwanangu sema nimependa kwanza unaanza kazi huko nimefurahi ishi na watu vizuri wakupende usiwe mkorofi pablo mwanangu kuwa mtu wa watu jichanganye katika misiba nenda kazike kwenye shughuli tengeneza jina lako kama pablo na pia naendelea kukusisitizia achana na wanawake huko au hata ukimpata basi awe mmoja uache uzinzi mwanangu tengeneza maisha yako mwanangu me ya kwangu hayo nakusisitizia na usiku mwema."
"Haya mama nawe pia."Mama aliendela kunisisitiza kwa maneno yake ambayo yalinifanya nitafakari sana maneno yale ambayo kwa namna moja ama nyingine yaliniingia barabara na kukaa katika kichwa changu na kujikuta nikitulia.lakini nikiwa bado natafakari ghafla mlango wangu ukagongwa na kusababisha mwanaume nivae nguo na kwenda kuangalia mgongaji alikuwa nani maana ilikuwa ni usiku wa kama saa mbili na nusu hivi.nikaufungua mlango lakini mshtuko ukanivamia na kujikuta nikitoa macho kwa mshangao alikuwa ni mwanamke mwingine wa watu ambaye yule nilimuona tu kwa sura lakini sikuwa na mfahamu wala kusikia sauti yake.
"Mambo unaniruhusu kuingia chumbanii??."...

Yalikuwa maneno ya yule mwanamke ambaye alikuwa amesimama na kuniangalia kwa makini na maneno yake yalisababisha nipigwe na kama butwaa na kujikuta nikimuangalia pasipo kusema chochote.Lakini nilipokuwa namuangalia yeye alikuwa ndani ya tabasamu pana usoni mwake na hakika swali lake sikujua nimjibuje na kujikuta nikimuonyesha kama sijamsikia maneno yale aliyoniambia.

"Jamani wee kaka si nakwambia unaniruhusu niingie chumbani."
"Naaam"
"Ujasikia au nirudie."
"Aaaa ingia hapo kwako bwana karibu karibu."Nikajikuta nikimkaribisha ndani huku nikiwa na wasiwasi mkubwa na kujiuliza uliza maswali imekuaje hata jina sijamjua na hata sijazoena naye kabisa na ndio siku yangu ya kwanza kuja pale tayari alikuwa anataka kuingia ndani.Mwanaume nikaingia ndani nakumkaribisha ndani lakini yeye alibaki palepale jambo ambalo lilinifanya nipatwe na mshangao baada ya kumuona yeye ameganda pale mlango akiangalia tu.
"Vipi wewe karibu mrembo mbona umesimama mlangoni."
"Hahahaha mgeni ndio anakaribishwa hivyo cha muhimu njoo unishike mkono tuingie wote ndani sio wewe unaanza kuingia unaniacha mimi hapa mlangoni sasa mimi nitaingiaje jamani
"Pumzi nzito nikazishusha baada ya kusikia maneno ya yule dada na kusababisha niishie nguvu na kuficha hali ile kwa kujifanya nitabasamu huku nikimuangalia na bila ya kuongeza chochote nikamsogelea na kumpa mkono wangu nikimaanisha aupokee nimuingize ndani.yule mwanamke hakuwa na hiyana akanipa mkono wake ambao sio siri ulikuwa mlaini kupita maelezo na kunipa kamzuka flani na msisimko baada ya kumshika lakini cha ajabu nilipojaribu kumvuta aingie ndani yule mwanamke akagoma badala ya mimi nimvute akanivuta yeye mpaka nje ya mlango wa chumba changu hali ambayo ilisababisha nitabasamu kwa mshangao.

"Hee unapenda masihara wewe."
"Hahahha hamna bwana unaitwa uani huko na mama mwenye nyumba anataka kuongea na wewe mawili matatu."
"Anhaa nakuja basi ngojea nikavae shati."Nikamwambia yule mwanamke ambaye baada ya kumwambia vile cha kushangaza akanibania jicho kuonyesha amenikonyeza hali ambayo ilinishtua kidogo na kujikuta nikitoa macho huku mdomo wangu ukiwa wazi hali ambayo ilisababisha yule mwanamke aangue kicheko cha deko kisha akanigeuzia mgongoni na kuelekea kule alipotoka na kutembea kwa makusudi.macho yangu yakatua katika kiuno chake alichokuwa akikuzungusha kwa madaha na kwa maringo ya haja na kusababisha nishushe macho yangu mpaka katika makalio yake ambayo ndio yaliyozidi kumpa kichwa na alikuwa akiyatingisha na kunisisimua sana na kusababisha udenda unitoke kabisa.yani kwa mara ya kwanza ndio nikaja kugundua kuwa sasa nilikuwa nakaa nyumba ambayo ilikuwa na warembo wakali lakini ndani mule wotr wanawake wale walikuwa wazuri lakini rozinta alikuwa amewazidi wenzake kwa kila kitu kuanzia shape uzuri wa sura hadi ongea yake na miondoko yake.baada ya yule mwanamke kutoweka katika macho yangu mwanaume nikazama ndani na kwenda kuchukua shati langu kisha nikalivaa na nilipomaliza nikajiweka sawa sawa kwa kujiangalia kwenye kioo kisha nikatoka nje na kuelekea mpaka uani ambapo nilikuta watu wengi kidogo wapata kama kumi au kumi na moja.

"Karibu baba hebu rozinta mpe hiyo stuli akae mgeni."mama mwenye nyumba akamwambia rozinta ambaye hakuwana hiyana akajisogeza na kwenda kuchukua stuli kisha akanisogelea na kunikabidhi mkononi na mimi nikaipokea huku nikikwepesha macho yangu nisimuangalie rozinta ambaye alikuwa akiniangalie kweli kweli kama mtu ambaye alikuwa anataka kuniambia kitu.Nikaweka sawasawa kile kistuli na kukifuta angalia kuwa hakukuwa na hata fumbi kisha nikakiweka chini na mimi nikaketi na kuwatizama wale watu ambao walionekana kabisa walikuwa ni wapangaji wenzangu.

"Haya mwanangu kama unavyotuona tupo hapa tumekuita kwanza samahani kwa usumbufu maana unaonekana umechoka kutokana na safari mwanangu."
"Aaaaa usijali mama angu mimi nipo pouwa endeleaa tu."
"Mmmh yani wee kijana nimekupenda yani ni mstaarabu yani tukiishi hivi hivi yanii nitafurahia sana enhe kwanza nimekuita hapa ujitambulishe kwa wapangaji wenzako maana hapa mimi naishi na wanangu hawa wawili yani huyu sabra na huyu samira umeowaona."mama mwenye nyumba akanionyeshea watoto wake ambao alikuwa ni sabra yule mwanamke ambaye alikua akitaka kuingia katika choo ambacho nilikuwepo na kujikuta tukigongana uso kwa uso na yule mwingine aitwaye samira ndio yule mwanamke alikuja kunigongea mlango na kuniambia naitwa.

"Anhaa safi mama nashukuru kuwafahamu."
"Enhe sasa hapo ukiniita mimi mama samira au sabra itakuwa vizuri mwanangu."
"Haya mama samrasabra."Nilimjibu mama mwenye nyumba ambaye baada ya kusikia vile akaachia kicheko kilichofuatiwa na wale wengine ambao nao wote wakacheka kutokana na kauli yangu.
"Sawa sasa na huyu binti anaitwa rozinta huyu ni mpangaji mwenzako lakini sio mpangaji kwa sababu mama yake ni shoga yangu kabisa mwanangu so anakaa hapa naye na hawa wengine wanaume hawa wamepanga hawa sasa nimekuita hapa mufahamiane mjuane lakini ningependa wewe ujitambulishe kidogo."
"Sawa mama sabra mimi naitwa pablo daniel ukiniita pablo inatosha."
"Anhaa safi naamini hawa wanaume mtazoeana kwani wewe sio mpenzi wa mpira maana hawa wapangaji wenzako kwa mpira."
"Hahahaa hata mimi napenda mpira na kuifupi ahsante sana mama kwa kunikaribisha vizuri maana hadi nimesikia furaha sana kwasababu ya ukaribisho umefanya nijisikie kama nipo nyumbani yani ahsante sana."Bila ya kuwa mchoyo nikatoa shukrani zangu za dhati kwa mama mwenyenyumba ambaye alikuwa akiitwa mama sabra na kushukuru kwangu ukaribisho uliwapendeza sana wapangaji wenzangu ambao wanaume kama mimi ambao walikuja kunipa tano.

"Unajua nini pablo sisi ni ndugu na alichofanya mama nikizuri kwa sababu sote sisi ni ndugu na lazima katika nyumba tuishi vizuri karibu pablo karibu morogoro."yalikuwa ni maneno ya mshikaji mpangaji mwenzangu ambaye naye alitoa ya moyoni yaliosapotiwa na kila mmoja aliyeyasikia vyema yale maneno na baada ya mazungumzo marefu mimi na wapangaji wenzangu pamoja na mwenyenyumba yalipofikia kikomo kila mtu akachukua muda wake na kuingia katika chumba chake hakika nikajikuta nikipata faraja kubwa ndani ya nyumba ile kwa sababu sikutegemea kuwa kwa mara ya kwanza ndani ya nyumba ya kupanga kupokelewa vizuri na watu walionekana wastaarabu kabisa maana nilikuwa naogopa sana kupanga kwa kipindi hicho baada ya kuweka sana ule msemo kuwa nyumba za kupanga zinamatatizo mengi.............

TAZAMA KICHEKESHO HIKI KISHA BONYEZA SUBSCRIBE ILIYOPO CHINI YAKE WAKATI TUKIELEKEA KWENYE MUENDELEZO



USIKOSE SEHEMU YA ISHIRINI NA MOJA

Maoni, Ushauri na Chochote Share Namimi Katika Mawasiliano Haya:
+255 718 274 413 Ipo WhatsApp
+255 764 339 438
ZephilineEzekiel@Gmail.Com

Chapisha Maoni