
SEHEMU YA ISHIRINI NA MOJA
Hakika nikajikuta nikipata faraja kubwa ndani ya nyumba ile kwa sababu sikutegemea kuwa kwa mara ya kwanza ndani ya nyumba ya kupanga kupokelewa vizuri na watu walionekana wastaarabu kabisa maana nilikuwa naogopa sana kupanga kwa kipindi hicho baada ya kuweka sana ule msemo kuwa nyumba za kupanga zinamatatizo mengi.............SASA ENDELEA...
Maisha ya morogoro yakaanza vizuri na Asubuhi na mapema kesho yake nikaamka na kwenda kuoga haraka na kujitayarisha vizuri nikiwa na udi na uvumba wa kuanza kazi ambayo haikutakiwa nipumzike na bila ya kuchelewa baada ya mimi kumaliza kujitayarisha tu david naye akabisha hodi na mimi nikamkaribisha na yeye akionyesha kufurahishwa na mimi kuwahi kwa sababu alitegemea labda ningeweza kuchelewa kutokana na uchovu mkubwa wa safari ambao labda ungeweza kunisababishia usingizi mzito."Daaah pablo sikutegemea yani umeamka mapema na nimekukuta tayari ushajitayarisha hakika nimependa tabia hii."David aliongezea na kunisifia baada ya hali ile kumfurahisha hali ambayo ilipelekea mwanaume niachie tabasamu la kipekee usoni mwangu baada ya kufurahishwa na maneno yale ya david.
"Daaa ahsante broo david ila ni kawaida maana ni wajibu wangu siunajua tena Mambo ya kazi."
"Aaaaa safi mdogo wangu nimependa nataka upige kazi uchape kazi kama baba yako anavyopiga kazi haya sasa ila umelalaje usiku wa jana na umepaonaje hapa umepapenda au magumashi tutafute sehemu nyingine."
"Aaaaaa hapa safi kaka angu safi sana watu wa humu ndani wakarimu wastaarabu hadi raha kiukweli nimepapenda kutoka moyoni na nimefurahi sana daaah nimepapenda."sikusita kutoa yangu ya moyoni na kumwambia david ambaye naye alitingisha kichwa kuelewa huku akitabasamu.
"Nyie masharobaro nawajua siunaona ulivyopendeza hakia ya Mungu morogoro watachinjwa sana maana wasichana wa huku malimbukeni lakini nakuomba ukienda nao tumia mipira kaka huku inauzwa kibao usiruke mechi kavukavu utaumia ndugu yangu utapotea maana maukimwi sasa hivi nje mimi nakusisitizia tu."David akaniambia yale maneno kwa msisitizo maneno ambayo yaliniingia kichwa mwangu nakujikuta nikikubali maneno yake yake kwa kumthibitishia kuwa sitamuangusha kwa lolote kuhusu maswala ambayo aliyokuwa akiniambia.Baada ya mazungumzo mafupi wote tukatoka nje kisha mimi nikafunga chumba changu kwa funguo kisha nikaongozana na david mpaka katika ofisi kubwa ya wakala wa tigopesa na mpesa ambayo ndio nilikuwa sasa nimeambia nifanye kazi pale tulipofika david kwa kutumia funguo zake akafungua ofisi ile ambayo ilinifurahisha baada ya kuona ndani na nikajikuta nikifurahia sana baada ya kuona mandhari ya ofisi ile ambayo ilikuwa imejengwa vizuri.wote tukazama ndani baada ya kufungua milango kisha moja kwa moja tukaenda kuketi katika viti ambavyo vilikuwa viwili.
"Mmmmh ofisi hii nzuri lakini nishaanza kuogopa sasa nikuulize swali majambazi hapa vipi."nikajikuta nikimuuliza swali ambalo cha kushangaza david akaangua kicheko cha nguvu sana baada ya kusikia kile nilichokisema.
"Morogoro hii Majambazi wote hawawezi kuja kuiba hapa kwa sababu ukiwa tu ndani ya duka hili na wewe ndio unafanya biashara hii unawapa watu pesa wanapotoa na kuchukua pesa za watu waoweka kwanza chumaulete yoyote yule aibu kwa namna yoyote duka hili limeoga pablo usiwe na shaka wala hofu na duka langu hili."Maneno ya david yalinitisha sana lakini sikuyatilia maanani kwa sababu nilijua tu watu wa morogoro wengi ni wanapenda kufanya mambo ya kishirikina.kwa utaratibu david akanielekeza utaratibu mzima wa kufanya vizuri kazi ile ambayo ndio aliyonipa kisha baada ya kumaliza akaniaga na kunitakia kazi njema huku akinisisitizia kuwa atakuja jioni kuja kufunga na mimi ofisi.Mwanaume nikajiweka sawa sawa na kufuta futa vumbi vumbi ndani ya ofisi yangu mpya kisha nikachukua simu yangu nakumtaarifu baba kuwa nimeanza kazi na baba alipokea taarifa ile vizuri huku na yeye akinisisitizia kuwa nifanye kazi kwa bidii jambo ambalo nilimuhakikishia kuwa nitakuwa mchapakazi bora.Lakini ghafla ile namaliza tu kuongea na simu na baba macho yangu yakutua katika uso wa mwanamke mweupe akitembea kwa maringo na alionekana kama mwenye mawazo flani kutoka na jinsi alivyokuwa akionekana taratibu akapiga hatua mpaka katika ofisi yangu lakini akashtuka baada ya kuona sura ngeni.
"Unaonekana una mawazo sana lakini karibu."Nikajikuta nikianza mazungumzo na yule dada ambaye baada ya kuyasikia maneno yangu akatabasamu na kusababisha nione vishimo katika mashavu yake na kuonyesha kuwa alikuwa na vishimo vya dimpoz katika mashavu yake.
"Jamani wee kaka umenitisha usione nimetabasamu umejuaje kama mimi na mawazo."yule mwanamke mweupe akanijibu na kusababisha nimuangalie kwa makini na kuregeza macho yangu ambayo yalisababisha yule mwanamke acheke kisha akaangalia chini alionekana kama alishakuwa dhaifu baada ya kuniangalia.
"Hamna kawaida unaonekana tu unawaza na kama sikosei itakuwa umetendwa na mtu labda kimapenzi au."
"Wala kawaida enhe mimi nataka kuweka pesa sijui salio unalo na vipi devi yupo wapi"
"Wee weka tu na david hayupo sasa mi ndio nitakuwa nakaa hapa now nafanya kazi hapa ofisi yangu hii."Nilimwambia yule dada ambaye alizama mfukoni na kutoa kiasi kadhaa cha pesa kama elfu sabini na kunikabidhi nimuwekee katika salio lake na mimi sikuwa na hiyana nikazipokea na kuanza kubonyeza namba kwa lengo la kumuwekea.
"Jina Elizabeth julius si ndio."nikamuuliza yule mwanamke mweupe ambaye alitikisa kukubali swali ambalo nilimuuliza.
"Ndio jina lako hilo.??"
"Yes mimi naitwa elizabeth vipi jina langu baya eee."
"Hamna jina zuri sana elizabeth ni majina ya watu warembo kama wewe siunaona ulivyo una dimpozz hadi raha."nilimsifia yule mwanamke aliyejulikana kwa jina la elizabeth ambaye baada ya kumwambia yale maneno akatabasamu kidogo kisha akaniangalia na kunitazama kwa makini.
"Nimependa ukarimu wako sana sijui unaitwa nani wee kaka."elizabeth akaniuliza swali na mimi nikamuangalia na kumuona elizabeth akiwa amesimama akiniangalia mimi kwa makini.
"Aaaaaa naitwa pablo elizabeth".
"Anha sawa jamani je unaweza ukanipa namba yako ya simu labda tuwe tunawasiliana na kushaurina na kufajiriana siunajua bwana sisi binadamu........"
Hakika nikajikuta nikishangaa sana Maana tangia nilipotua katika mkoa wa morogoro hali ilikuwa imebadilika nikajikuta nikijishangaa kwa sababu nyota yangu ilionekana kung'aa sana pindi tu Mwanamke yoyote atakapo niona.Tendo la yule mwanamke elizabeth kuniaomba namba yangu ya simu kulinishangaza sana kwa sababu sikutegemea kwa uzuri wake kwamba angejirahisishia kabisa na kuniomba namba yangu ya simu.Nikajikuta nikaa kimya kidogo nakuanza kuwaza kitu ambacho sikukujua nawaza nini.Nilikuja kushtulia na elizabeth ambaye aliniuliza swali lakini nilichelewa kidogo kumjibu jibu lake.
"Eeee jamani mbona umekuwa kimya ghafla pabilo."
"Aaaaa hamna bwana kawaida hivi ulikuwa unasemaje eliza."
"Aaaaa mimi nataka namba yako ya simu nataka tuwe tunawasiliana."Sikuwa na hiyana kidume nikamtajia namba zangu za simu namba zangu zote mbili ambazo yeye alizihakikisha kwa kuzipiga pale na aliposikia zinaita akafurahia kisha akaniaga kuwa yeye anaondoka na anaomba tuwe na tunachati kwa njia ya uwanja wa messeji jambo ambalo sikumkatalia nikamkubalia kabisa bila ya matatizo.Hakika elizabeth ndio akawa mteja wangu wa kwanza kabisa na ndiye aliyenifungulia mlango wa wateja ambao wengi wao walimininika ofisini kwangu huku wakiwa wanahitaji huduma zile zile ambazo wengine walikuwa wakilipa umeme na hata waliokuwa na ving'amuzi vyao pia walijisogeza na kuja kulipia pale.biashara ikanikolea kabisa na kujikuta siku ya kwanza tu nikaipenda na kwa ile siku moja watu walinizoea na wengine hadi walikuja mara mbili mbili kuweka fedha na kutoa takribani wateja wengi ambao walikuwa wote wanakuja walikuwa wakiniuliza jina langu na mimi sikusita kuwatajia jina langu ambalo lilikuwa ni tatizo kubwa kwa watamkaji ambao wengi wao kiruguru kilikuwa kimewameza sana katika lafudhi zao hadi kifika wengine kuniita pabilii,pabro na kadhalika.Siku ikakatika na jioni bosi wangu ambaye alikuwa rafiki yake kipenzi baba yangu mzazi akawasilia katika ofisi ile ambayo hakika akajikuta akishangaa sana na kiasi cha pesa nilichoingiza katika ofisi ile ndani ya siku moja.
"Weee pablo unatumia nini ndani ya siku moja umeingiza kiasi chote hiki daaah kweli wewe una nyota ya biashara."kama kawaida david akaniachia pongezi zangu ambazo zilinifanya kichwa kiwe kikubwaa sana nakujikuta nikijisifia mwenyewe na baada ya yeye david kuridhika akaniachia na funguo za ile ofisi na kunisisitizia kutochelewa ofisi pale kisha akaondoka zangu nakunipa ahadi kuwa ataonekana kesho yeye.Mwanaume baada ya kufunga ofisi katika mida ya kama saa kumi na mbili kuelekea saa moja nikapitia kwa marafiki ambao nilitambulisha nao kupitia david ambao niliwasalimia kisha nao nikaelekea katika kibanda cha kuuza chips nikachukua chipsi.
"Pablo....pablooo...wee pablo simama."Ghafla nikasikia sauti ya kike ikiniita na mimi taratibu nikageuka kimachale lakini nikauona sura nzuri ambayo ilisababisha nitabasamu alikuwa si mwingine bali ni rozinta mpangaji mwenzangu ambaye alikuwa mzuri kupindukia hasa shepu yake ndio ilizidi kumfanya aonekana ni mrembo wa bei ghali.
"Nambie pablo jamani nakuita weee."
"Aaaaa kichwa kina mambo mengi mrembo nambie umetoka wapi."
"Mmmh eti mrembo sasa mimi ninaurembo gani."sauti tamu ya rozinta hakika ilinikosha kweli kweli hata alipoongea alikuwa akiongea kistaili kama masista duu wa dar-es-salaam hali ile niliipenda sana kutoka kwa rozinta.
"Halafu pablo bwana naomba ule niwe mgeni wako kwako najua umechoka lakini nataka nije kuangalia movie wewe si una dvd au huna."Maneno ya rozinta yalinishtua kidogo na kujikuta nikisusua kumjibu lakini wala sikumuonyesha hali ile nikajikuta nikitabasamu tu huku nikiwaza kumjibu.
"Aa...aa....aaa...n..jooo tuu itakuwa pouwa."Nikajitutumua kumjibu rozinta ambaye alifurahishwa na jibu langu ambalo nililitoa kwa tabu mno.rozinta bila ya kuogopa akaniomba na simu yangu ambayo nilimkabidhi kwa sababu aliniambia anaiomba mara moja na mimi nikampatia.Rozinta akajibipu katika simu yangu kisha akanikabidhi simu yangu nakuniambia kabisa kuwa namba yake ndio hiyo na atanitumia messeji mida ya saa tatu kwa sababu alikuwa hataka wapangaji wengine wamuone wakati atakapokuja kuingia chumbani kwangu.sikuwa na haja hata kidogo kumkatalia kwa roho nyeupe nikamkubali kisha wote tukaelekea nyumbani ambapo tulipofika kila mtu akaingia katika chumba chake.Mwanaume kutokana na kuujua ugeni nikaweka sawa chumbani mwangu na kusafisha safisha sawasawa kisha nikaenda bafuni na kujimwagia kisha nikarudi ndani na kurudi ndani mwangu na kula chips zangu ambazo nilizinunua.Lakini ghafla nikiwa naangalia tv yangu mlio wa messeji ukasikika katika simu yangu na nilijua kabisa aliyetuma messeji ile lakini nikaichukua nakuhakikisha kabisa mtuma messeji alikuwa nani.
"Enhe pablo nije.??"alikuwa si mwingine bali ni mrembo rozinta na mi sikuwa na tabu nikamjibu aje na kumwambia kabisa mlango nimeugesha tu na atakapofika asipige hodi aingie tu.hakupita hata dakika tano hamadi Mlango ukafungulia na mrembo rozinta akaingia ndani huku akiwa amevaa kanga moja tu ambayo ilikuwa imelowa maji na kuonyesha alikuwa ametoka kuoga muda huo mfupi aliniangalia na kutabasamu baada ya kuingia kisha akanipa mgongo ambapo yeye alikuwa akifunga mlango macho yangu yakatua katika mzigo wake alioubeba chini ya kiuno chake kipana taratibu kiungo changu kikuu cha siri kikanyanyuka haraka uchu ukanitoka sasa na maneno yote ya mama na baba waliyoniambia yakanitoka baada ya kuona vile.
"Mmmmh huyu rozinta hakia ya Mungu simuachi...
TAZAMA KICHEKESHO HIKI KISHA BONYEZA SUBSCRIBE ILIYOPO CHINI YAKE WAKATI TUKIELEKEA KWENYE MUENDELEZO

USIKOSE SEHEMU YA ISHIRINI NA MBILI
Maoni, Ushauri na Chochote Share Namimi Katika Mawasiliano Haya:
+255 718 274 413 Ipo WhatsApp
+255 764 339 438
ZephilineEzekiel@Gmail.Com
Maoni, Ushauri na Chochote Share Namimi Katika Mawasiliano Haya:
+255 718 274 413 Ipo WhatsApp
+255 764 339 438
ZephilineEzekiel@Gmail.Com