AISEE KUMBE RAHA (21)
JINA: AISEE KUMBE RAHA Mwandishi: Pablo SEHEMU YA ISHIRINI NA MOJA ILIPOISHIA... Hakika nikajikuta nikipata faraja kubwa ndani ya nyumba ile kwa sababu sikutegemea kuwa kwa mara ya kwanza ndani ya nyumba ya kupanga kupokelewa vizuri na watu walionekana wastaarabu kabisa maana nilikuwa naogopa sana kupanga kwa kipindi hicho baada ya kuweka sana ule msemo kuwa nyumba za kupanga zinamatatizo mengi............. SASA ENDELEA... Maisha ya morogoro yakaanza vizuri na Asubuhi na mapema kesho yake nikaamka na kwenda kuoga haraka na kujitayarisha vizuri nikiwa na udi na uvumba wa kuanza kazi ambayo haikutakiwa nipumzike na bila ya kuchelewa baada ya mimi kumaliza kujitayarisha tu david naye akabisha hodi na mimi nikamkaribisha na yeye akionyesha kufurahishwa na mimi kuwahi kwa sababu alitegemea labda ningeweza kuchelewa kutokana na uchovu mkubwa wa safari ambao labda ungeweza kunisababishia usingizi mzito. "Daaah pablo sikutegemea yani umeamka mapema na nimekukuta tayari ushajitayarisha hakika ni…