AISEE KUMBE RAHA (25)

Zephiline F Ezekiel
0
Mwandishi: Pablo

SEHEMU YA ISHIRINI NA TANO
Lisaa limoja na nusu likapita yule mama afya ambaye baada ya kutochoma sindano hakutoka sasa akatoka akiwa katika hali ya umakini katika uso wake.
"Haya wanangu nawaombeni wote muingie ili myapokee majibu yenu.".......

SASA ENDELEA...
Baada ya kusikia yale maneno ya yule mama wa kile kituo cha afya tukasimama mimi na rozinta ambaye alikuwa wa kwanza kusimama haraka haraka akiwa anajiamini kuliko mimi ambaye nilikuwa mnyonge kupitiliza.Hofu kubwa ilikuwa katika kusikia majibu yangu na hali hiyo ilipelekea nikose na nguvu majasho yakawa yananitiririka kama mtu ambaye alikuwa ndani ya chumba chenye joto kumbe wala.Baada ya kujiungia tukakuta yule mama ameshatayarisha viti viwili ambavyo ile tunaingia yule mama akaonyesha ishara ambayo ilituambia tukae na sisi wote wawili mimi na rozinta tukakaa kitiifu kupita maelezo.

"Haya wanangu wapendwa nimependa mlivyokuja kupima mkiwa wote wawili kwa hakika mmefanya uamuzi sahihi katika mauhusiano yenu nani hatua muhimu yakuthibitisha kuwa uhusiano wenu ni thabiti sana."Alianza yule mama na kuendelea na kusababisha wote tumsikilize kwa makini ingawaje mimi nilikuwa na hofu kupita maelezo.
"Sasa basi kama mmeamua kufanya hivyo ni vyema sana je ningependa kuanza na swali dogo tu kwa bibie hapa rozinta hivi utakaposikia kwamba huyo mpenzi wako pablo utajisikiaje."maswali yakaanza na la kwanza akaambiwa rozinta ambaye baada ya kuulizwa swali lile ukaingia ukimya mzito ambao uliniogopesha sana lakini sikuwa na la kuongea ni kakaa kimya nakumsikilizia rozinta ambaye dakika tatu zikapita bila ya rozinta kujibu.

"Mmmmh vijana nyie wa siku hizi haya nisingependa kuwauliza maswali mengi sana ninaweza kuwachanganya akili ngojea niende straight to the point kwa kuwatangazia majibu yenu naanza na rozinta."
"Rozinta."
"Abee Mama."
"Kwa vipimo vyetu tulivyopima inaonyesha kabisa kwamba wewe ni salama kabisa huna maambukizi yoyote yale ya ukimwi."Ilikuwa ni taarifa ambayo niliitegemea kwa sababu rozinta alishanionyesha cheti chake kikionyesha ni salama kabisa baada ya kupima siku mbili nyuma yake.
"Haya sasa na wewe pablo."yule Mama akaniita na kusababisha hofu izidi kuchukua mkondo wake uoga ulinifanya nisimame na kusababisha wote yule mama na rozinta kushangaa lakini nikajifanya nafunga mkanda vizuri vile kisha nikaketi kimya majasho yakizidi kunitoka kama nimefumaniwa vile.

"Mmmmh pablo unajua kuwa na ukimwi sio mwisho wa kuishi na pia kuna njia siku hizi salama tu unaweza hata ukatumia na mpenzi wako endapo utakuwa umeathirika kuwa na ugonjwa huu haumaanishi kama eti ndio wa kufa muda wowote vipo vidonge vya kuweza kurefusha maisha na ukaishi vizuri kama wengine."Maneno ya yule mama yalitosha kabisa kunivunja nguvu na kutamani hata kulia niliiona kabisa nilikuwa nimeshakwisha kutokana na risala yake aliyokuwa akinipa kwa kuniambia Kwa mbali nikawa namuangalia rozinta kwa jicho la kuibia na yeye alionekana akihema juu juu kama anakimbizwa pia naye alionekana kuwa na hofu kupitiliza na kuonyesha alikuwa ana hamu kubwa ya kusikia kile atakacho kihitimisha yule Mama ambaye baada ya kuongea maneno yale akaniangalia kisha akarudia kuitazama karatasi yake.

"Ukweli ni kwamba pablo weee nii...niii....msafi kabisa na wala haujaathirika."Hali ya furaha ikalipuka ndani mule nikajikuta nikishindwa kuizua furaha yangu nikanyanyuka na kuanza kuruka ruka kwa sababu nilikuwa siamini kama kweli nitakuwa mzima kutokana na uzinzi mkubwa nilioufanya katika jiji la dar-es-salaam.Rozinta naye hakuwa nyuma baada ya kusikia majibu yangu na kuniona nimesimama na ruka ruka naye akajiunga na mimi kwa kunituliza kwa kunikombatia na palepale tukaanza kunyonyana ndimi mimi na rozinta kimahaba zaidi palepale na kukatishwa na Mama afya yule ambaye naye alikuwa katika uso wa tabasamu baada ya kutuona wote tukiwa katika hali ile.
"Jamani vijana wangu najua mmefurahi sana na mnapaswa kufurahi lakini majibu haya ya leo yanaweza kubadilika kama utashirikiana na Mtu vitu vyenye ncha kali na muathirika wa ukimwi,kupiga mswaki wa mtu muathirika,kufanya mapenzi na mtu ambaye ameathirika hata kunyonyana kama mlivyofanya hapo hakika jamani kuna vitu vingi vya kuviepauka sana wanangu na mnatakiwa muwe makini kupita maelezo."Yalikuwa maneno ya yule mama yaliyotufanya tutulie kidogo baada ya kuyasikia maana yalikuwa na ukweli mtupu kwa sababu yale aliyoyasema kama ukiyakosea basi utaweza kusababisha hatari.yule mama alipomaliza kuongea mimi na rozinta tukamuaga yule mama ambaye bila ya aibu akatupa boxi kubwa la condom na kuambatanisha na majarida ambayo tuliyachukua na kuondoka nayo.furaha ilikuwa furaha kweli kweli kati yangu na rozinta baada ya kutoka katika kile kituo cha afya huku kila mtu akiwa na majibu salama ambayo hayakumkwaza mwenzake tukaenda kukodisha bajaj kurudi nyumbani.

"Sasa pablo leo mapema jamani mpenzi tufanye kamchezo kale."alisema rozinta maneno yale ya uchokozi uchokozi huku akipapasa katika mapaja yangu na kusababisha pablo wangu kupata msisimko wa hali ya juu.
"Mmmh unazingua wewe juzi umenibania mwenyewe na leo unaweza ukaniambia nije halafu ukajifanya ooo mara ooo.."Nilimjibu rozinta kama mtu ambaye niliyekuwa sitaki ombi lake na maneno yangu yalisababisha rozinta apoe kidogo na kuniangalia kwa huruma akinionyesha kuwa alikuwa anataka kulia.

"Pablo naomba unisamehe haikuwa kusudio langu kufanya vile."rozinta akapoa lakini mimi nikamtoa hofu kwa kumuambia nimemsamehe na kukubali ombi lake kwa sababu hata mimi nilikuwa sijiwezi uchu wa mapenzi ulinichukua kabisa kwa sababu ilipita muda kidogo kutofanya mapenzi.Kama kawaida yetu safari hii mimi nikaanza kutangulia nyumbani na kumuacha rozinta ambaye aliniaga anakwenda kwa rafiki yake ambaye alikuwa akiishi mitaa ile ile ili kuwapoteza watu wasijue kama mimi na rozinta wapenzi.Nikafika nyumbani na kuweka mambo sawa kabisa na nikaenda pia na kuoga kujiandaa kabisa na mechi na haikupita hata muda mrefu rozinta alinitumia messeji kuwa yeye anaoga na niache mlango wazi.Ilikuwa ni mida ya saa kumi jioni kuelekea kama saa kumi na moja mimi nilikuwa tayari nimevaa nguo yangu ya ndani tu boxer na kumsubitia kwa hamu rozinta.Ghafla mlango ukafunguliwa na kufungwa haraka kisha aliyefunga mlango akifunga vizuri kwa kuzungusha funguo katika kitasa ugeni wake niliutarajia na alikuwa siwingine bali ni rozinta ambaye kama anavyopenda alikuwa ndani ya kanga moja baada ya kumaliza kufunga akanisogelea karibu na aliponifikia akasimama na kuniangalia kisha taratibu akaichia kanga yake yote.

"Wooooooooow."Neno likanitoka kabisa uchu ukazidi kupanda baada ya kumuona rozinta akiwa kama alivyozaliwa na alikuja pale akiwa hana hata nguo ya ndani alikuwa amevaa kanga tu bila ya kuvaa na nguo ya ndani.Mwanaume nikakurupuka na kunyanyuka pale nilipokaa lakini nikarudishwa palepale na rozinta ambaye alinisukuma.
"Jamani ndege wako mwenyewe kwanini umshikie manati.??"............

TAZAMA KICHEKESHO HIKI KISHA BONYEZA SUBSCRIBE ILIYOPO CHINI YAKE WAKATI TUKIELEKEA KWENYE MUENDELEZO



USIKOSE SEHEMU YA ISHIRINI NA SITA

Maoni, Ushauri na Chochote Share Namimi Katika Mawasiliano Haya:
+255 718 274 413 Ipo WhatsApp
+255 764 339 438
ZephilineEzekiel@Gmail.Com

Chapisha Maoni

0Maoni
Chapisha Maoni (0)