AISEE KUMBE RAHA (25)
JINA: AISEE KUMBE RAHA Mwandishi: Pablo SEHEMU YA ISHIRINI NA TANO ILIPOISHIA... Lisaa limoja na nusu likapita yule mama afya ambaye baada ya kutochoma sindano hakutoka sasa akatoka akiwa katika hali ya umakini katika uso wake. "Haya wanangu nawaombeni wote muingie ili myapokee majibu yenu."....... SASA ENDELEA... Baada ya kusikia yale maneno ya yule mama wa kile kituo cha afya tukasimama mimi na rozinta ambaye alikuwa wa kwanza kusimama haraka haraka akiwa anajiamini kuliko mimi ambaye nilikuwa mnyonge kupitiliza.Hofu kubwa ilikuwa katika kusikia majibu yangu na hali hiyo ilipelekea nikose na nguvu majasho yakawa yananitiririka kama mtu ambaye alikuwa ndani ya chumba chenye joto kumbe wala.Baada ya kujiungia tukakuta yule mama ameshatayarisha viti viwili ambavyo ile tunaingia yule mama akaonyesha ishara ambayo ilituambia tukae na sisi wote wawili mimi na rozinta tukakaa kitiifu kupita maelezo. "Haya wanangu wapendwa nimependa mlivyokuja kupima mkiwa wote wawili kwa hakika mmef…