AISEE KUMBE RAHA (27)

Zephiline F Ezekiel
AISEE KUMBE RAHA (27)
JINA: AISEE KUMBE RAHA Mwandishi: Pablo SEHEMU YA ISHIRINI NA SABA ILIPOISHIA... Nikaingia Chumbani kwangu kwa hasira hali iliyosababisha hata rozinta ashtuke na nilikuwa nahema juu juu huku sura yangu nimekunja kwa hasira hali iliyosababisha rozinta atumbue Macho na Hofu kubwa kumshika hadi kupelekea kujiweka vizuri kwa kujifunika na shuka kutokana na yeye kuwa hana Nguo. "Rozintaaa."...... SASA ENDELEA... Nikamuita rozinta kwa hasira jambo ambalo lilionekana kuzidi kumtia hofu. "Abee." Rozinta akaitia huku akinitazama kwa umakini wa hali ya juu jambo ambalo lilianza kunifanya presha yangu kushuka taratibu baada ya kuambiwa maneno yale kuhusu rozinta na mpangaji mwenzangu.Kwa hakika macho ya rozinta yaliokuwa makubwa kiasi yalizidi kunimaliza na hata alivyokuwa akiniangalia kwa shauku kubwa ya kutaka kujua nini nilichomuita kwa hasira.Hasira zangu taratibu zikapungua na kutulia kimya kama sio mimi niliyemuita rozinta ambaye alikuwa wakati huo kitandani. "Aaaaa kwanza …