AISEE KUMBE RAHA (28)

Zephiline F Ezekiel
AISEE KUMBE RAHA (28)
JINA: AISEE KUMBE RAHA Mwandishi: Pablo SEHEMU YA ISHIRINI NA NANE ILIPOISHIA... "Jamani baby mke wangu rozinta unalia nini tena." "Yani baby hapa Nimechanganyikiwa kwa sababu nimepigiwa simu kijijini kwetu hali ya mama ni mbaya sana na kesho natakiwa niende mume wangu"............ SASA ENDELEA... Yalikuwa maneno ya rozinta yalinifanya nitumbue macho kidogo huku nikiwa na masikitikio makubwa sana baada ya kuambiwa habari hiyo ambayo rozinta baada ya kuniambia aliendelea kuangua kilio na mimi ikabidi niutumie muda huo kumbembeleza. "Jamani rozinta pole Jamani pole sana lakini ataponaa tu kwani anaumwaa nini."Nilimuuliza rozinta ambaye kama nilimchokoza maana aliongeza kilio ambacho kilisababisha hata mimi mwenyewe nitokwe na machozi kutokana na kumuonea huruma sana rozinta. "Rozinta usilie hivyo unaniumiza moyo wangu Nambie mama anaumwa nini basi hata kidogo." "Mama...anaumwaga Pumu baby soo imemshika sana na hali mbaya sana baby nalia naumia kwa saba…