AISEE KUMBE RAHA (30)

Zephiline F Ezekiel
AISEE KUMBE RAHA (30)
JINA: AISEE KUMBE RAHA Mwandishi: Pablo SEHEMU YA THELATHINI ILIPOISHIA... Nilikubali maneno ya mpangaji mwenzangu na kutulia kabisa na hapo safari ya kurudi nyumbani ikachukua hatamu machozi yalikuwa yananitiririka mashavuni na hapo ndio maneno ya mama yangu mzazi yaliponirudia kichwani mwanangu na kusababisha nikumbuke ya nyuma......... SASA ENDELEA... Hakika nilijiona kama mtu ambaye ana mikosi katika maisha kwa sababu kila sehemu niliyokuwa naenda basi lazima majanga yanitokee.Nilikumbuka vitu vingi sana kuhusu maneno ya baba na david na mama ambao walinisihi sana huku david akiwa mstali wa mbele kunisisitizia kuwa wanawake wa hapo morogoro sio watuliaji kwa hiyo kama nitakuwa nao basi nisisahau kutumia kinga ili kujilinda na Maradhi ya magonjwa ya ngono yakiambatana na ugonjwa hatari wa ukimwi.Nilipokumbuka kuwa mimi na rozinta tulipofanya mapenzi tulifanya kavu kavu ndio majonzi yalipozidi na kujikuta nikilia kama mfiwa ndani ya kibajaji kile na kumpa tabu mpangaji mwenzangu kunibembe…