
SEHEMU YA THELATHINI
Nilikubali maneno ya mpangaji mwenzangu na kutulia kabisa na hapo safari ya kurudi nyumbani ikachukua hatamu machozi yalikuwa yananitiririka mashavuni na hapo ndio maneno ya mama yangu mzazi yaliponirudia kichwani mwanangu na kusababisha nikumbuke ya nyuma.........SASA ENDELEA...
Hakika nilijiona kama mtu ambaye ana mikosi katika maisha kwa sababu kila sehemu niliyokuwa naenda basi lazima majanga yanitokee.Nilikumbuka vitu vingi sana kuhusu maneno ya baba na david na mama ambao walinisihi sana huku david akiwa mstali wa mbele kunisisitizia kuwa wanawake wa hapo morogoro sio watuliaji kwa hiyo kama nitakuwa nao basi nisisahau kutumia kinga ili kujilinda na Maradhi ya magonjwa ya ngono yakiambatana na ugonjwa hatari wa ukimwi.Nilipokumbuka kuwa mimi na rozinta tulipofanya mapenzi tulifanya kavu kavu ndio majonzi yalipozidi na kujikuta nikilia kama mfiwa ndani ya kibajaji kile na kumpa tabu mpangaji mwenzangu kunibembeleza."Mwanangu pablo mwanaume alii Mwanaume anatuliza kichwa ili ajue anafanya nini sasa wewe utakapolia lia kama Mtoto wa kike mwanangu aisadiii kama kutokea yameshatokea Cha msingi ni kwamba kesho hakikisha unaenda kupima ili ujue afya yako pablo mimi nitakusindikiza tena hospitali ya mjini."Aliniambia Mpangaji mwenzangu ambaye mara kama mbili alishawai kuniambia habari za rozinta lakini sikumpa nafasi yoyote ya kumsikiliza.Tulifika nyumbani mimi na Mpangaji mwenzangu ambaye pia alikuwa mstari wa mbele kunipaka spirit akiwa na lengo la kuzuia damu kutoka na kunifunga bandeji maeneo ya paji la mso na mkononi kisha akaniaga na kuondoka zake.Siku hiyo sikupata hata lete la usingizi kichwa changu kiliwaza mno na kila nilipokuwa nakumbuka jina la rozinta chozi yalitiririka mashavuni mwangu.
"Aisee nimeamini kuwa rozinta ni malaya nasikitika sana kuwa nilimtegemea eti leo amenifanyia hivi kwanini sikusikia maneno ya Mama wakati nakuja huku na kunisisitizia huku ni morogoro na sio darKwanini sikusikiliza maneno ya baba ambaye alijitolea tena kwa moyo wake wa kipekee na kumuomba rafiki yake anaitengenezee maisha huku daaah david naye alikuwa na nia nzuri tu na mimi alinijua kabisa kuwa mimi naonekana napenda wanawake akanipa ushauri wa bure kwamba nitumie mipira ya kujikinga nimefanya nini sasa nimeenda naye kavukavu nitafanya nini nitakapokuja kujua kuwa na mimi muathiriki eeee Mungu najua mimi ni mja wako na ni binaadamu ambaye nina mapungufu ya hapa na pale naomba basi nihurumie kwa hili tenda miujiza niende kesho kupima nikutwe sijaathirika daaah ila maneno ya watu haya wanaosema amewamaliza wengi rozinta na umalaya wake mimi nitapona kweli haya bwana." Nililia sana na kulalamika peke yangu huku nikiona kama Mwenyezimungu kama amenionea kumbe niliyatafuta mwenyewe majanga ambayo kama ningesikiliza miono na ushauri wa watu basi yasingenikuta.Usiku huo pia mwili wangu ulianza kuuma na kunikosesha kabisa na usingizi wenyewe kwa sababu pale nilipokuwa napigwa na mpaka kutolewa nje nilikuwa sijikii maumivu lakini muda huo wakati nilipokuwa nimejiegesha katika kitanda ambacho Tulishaserebuka sana mimi na rozinta nilikuwa muda huo nasikia maumivu ambayo yalitokana na kipigo cha nguvu nilichopokea huku msichana niliyempenda akinifanyia timbwili hilo huku akishadadia kabisa nipigwe na wale watu wake.Kama Mungu alivyopanga asubuhi kukakucha usingizi hata kidogo haukuja nilikuwa macho na kusikia majogoo wote waliokuwa wakiwika kuwaamsha watu.Asubuhi ile ile na mapema nikajikusanya huku mwili wangu ukiwa unauma sana sehemu zote nikajikaza kisabuni na kwenda kuoga haraka kisha nikachukua kiasi cha fedha kama laki moja kutoka katika mauzo ya biashara ya david pasipo kumuomba na kutoka jumatatu hiyo ambayo sikufungua ofisi na kuamua kwenda kupima ugonjwa hatari wa Ukimwi.Sikutaka kusindikizwa na mtu maana mpangaji mwenzangu alinihaidi kunipeleka kama nikihitaji haraka nikaenda mpaka katika kituo na kupanda gari za kwenda morogoro mjini ili nikatafute kituo kizuri cha upimaji wa ugonjwa wa ukimwi huko baada ya kuogopa kwenda katika kituo cha mwanzo niliyoenda kupima ugonjwa huo na rozinta kwa kuogopa nitaweza kuanzisha vurugu mpya baada ya kuamini sasa muda huo kuwa rozinta mara ya kwanza alimlipa mama yule wa kile kituo.safari ikaanza mara moja huku nikiwa miongoni mwa abiria niliosimama kutokana na kutopata siti ya kukaa mawazo yangu yalikuwa kituoni moyo ulikuwa unaenda mbio kama mtu aliyekuwa anakimbizwa kwa wakati ule.Kutokana na kutokuwa na umbali mrefu kutoka morogoro mjini na pale tulipokuwa naishi nikafika mapema morogoro mjini nakuanza kuulizia kituo cha upimaji wa ugonjwa wa ukimwi.Kama ujuavyo desturi ya watanzania walivyokuwa sio wachoyo kwa kuelekeza mtu anayehitaji kuelekezwa mahali nikaelekezwa katika kituo cha upimaji wa ukimwi na bila ya kupoteza muda nikatembea kwa mguu mpaka nikafika katika kituo hicho na kukaribishwa na Maneno yaliyoandikwa Angaza bila ya kusita nikaingia ndani na kukuta watu wengi walikuwa tayari washafika nikapewa namba na kuambiwa nikae nisubirie.Nilikaa kama nusu saa zamu yangu ikafika nikaingia ndani mpaka kwa daktari ambaye alinichoma sindano katika kidole changu na kukusanya damu kupitia katika kioo chake maalumu na kuniachia spirit ya kuzuia damu isitoke katika kidole ambacho alinichoma.Baada ya kumaliza nikaambiwa nijumuike na wenzangu kusubiri majibu na mimi nikaenda kujumuika huku nikiwa na mawazo mengi.Sehemu tuliyokuwa tunasubiri kulika na semina kubwa pale kulikuwa kuna television kubwa na mwalimu ambaye alikuwa akituelekeza Madhari ya ugonjwa wa ukimwi Na kusisitizia kuwa kama utakuwa umepata ugonjwa huo basi inatakiwa kutumia dawa ipasavyo ili kupunguza makali ya ugonjwa huo na dawa hizo zinasaidia kurefusha maisha ya wale walioathirika na ugonjwa wa ukimwi.Hakika semina ile kwangu haikuniingia nilibaki nikiangalia tu yule mdada aliyekuwa anatuelekeza na kutuonyesha na vitu katika ile television iliyokuwa flatscreen kila baada ya dakika tano ilikuwa kila mtu anaitwa kwenda kuchukua majibu yake Nilijikuta nikiogopa baada ya mdada mmoja kutoka katika sehemu ya kuchukua majibu yake akiwa analia.
"Jamaani nitakuwa mgeni wa nani mimi nimeaathirika nani atanitaka mimi naniiii jamaniii aaaaaaaaaa." Yalikuwa ni maneno ya huyo mdada ambaye kwa hakika aliniogopesha sana mimi na kubaki nikimuangalia huku nikiona kabisa kuwa tutakuwa tunafanana majibu.Zamu yangu ikafika namba yangu ikatajwa taratibu kwa hofu nikanyanyuka huku nikimuomba Mungu aweze kunifanyia miujiza nikaingia na kumkuta mama mwenye makamo ya kuitwa mzee kabisa kutokana na mvi zilizokuwa kichwani mwake.
"Karibu uketi."akaniambia yule bibi na mimi nikafanya kama alivyosema huku mikono yangu ikitetemeka vilivyo kwa hofu kubwa.
"Weee ndio pablo."
"Naaam ndio mimi bibi."
"Mi nisingependa kukupa presha sana juu ya majibu yako lakini ningependa kukwambia kuwa kuwa na ukimwi sio kusema eti ndio mwisho wa maisha mmh hapana zipo dawa zinaitwa Arv zitakusaidia kurefusha maisha yako.unatakiwa kufanya sana mazoezi kula vyakul bora kula sana matunda ili kujiweka sawa.Ukimwi hatakuua kama utatimiza masharti yote na kuzingatia vitu ambavyo nimekutajia lakini utakuua kama hautofatisha nilivyokuambia napenda kukuambia Pablo umeathirika namaanisha wewe ni muathirika wa ugonjwa wa ukimwi"..............
Chozi likanidondoka baada ya kusikia yale majibu yaliosomwa na yule bibi aliyeonekana kuwa makini na kile anachokisema Alikuwa ananiangalia kwa kunikazia macho na kusubiri nini nitakifanya baada ya kunitajia majibu yangu ya upimaji wa ukimwi.Sikuamini kabisa majibu yale taratibu nikapeleka mkono wangu wa kulia mpaka katika karatasi ile aliyokuwa ameishika yule bibi na kuichukua macho yangu yakaangalia vizuri ile karatasi niliona kama vile yule bibi atakuwa amekosea kuyatamka majibu yangu.
"Positive." Nikalitamka lile neno huku nikimuangalia yule bibi na baada ya kufikiria sana akili yangu ikanipa kuwa majibu yako yatapoandikwa positive katika ukimwi basi utakuwa umeathirika.Nikajikuta nikiangua kilio cha nguvu kilichosababisha hata waliokuwa nje ya kile chumba cha majibu kusikia.
"Rozintaaaaaaaaaaa umeniuaaa mimiii aaaaaaaa rozinta kwanini hukuniambia mapemaaaaa whyyyy why me kwanini kila siku mimi jamani kwaniiii ona sasa nimeaaathirika atanitaka nanii mimi mimi nimekwisha hakia Mungu nimekwishaaaa." Nililalamika mwenyewe kwa hakika majuto ni mjukuu yale yote niliyoambiwa yakinijia kama filamu katika kichwa changu nilichoka kwa kweli.Washauri baada ya kusikia kilio changu wakaingia ndani ya chumba kile cha majibu kuanza kunishauri kuhusiana na mambo ya ukimwi na jinsi ya kuishi na virusi hivyo vya ukimwi katika mazingira salama ambayo hayatakuja kuniathiri.Kituo kile kikanishauri niwe natembelea katika kituo kile mara kwa mara kisha wakanipa na dawa mpya kabisa za Arvs na kunipa masharti yake yakuzitumia ili kuepuka ugonjwa huo usiendelee kunisambulia kwa sababu mpaka muda huo virusi hivyo vilikuwa bado havijasambaa sana.
"Hiii dawa ndio mkombozi wa maisha yako Hakikisha unazitumia ipasavyo na hakikisha kila siku unakunywa na wala hautakiwi kuharibu dozi utakapoharibu tu kumbuka utajisababishia matatizo.Tunakupa ushauri Mwingine kama utakuwa umepata na mwanamke hakikisha mnatumia mpira nikimaanisha kondom nakutakia maisha mpya pablo nakupa nakala hii nzuri kabisa na hakikisha unasoma makala hii ili kuweza kujua miilo yote salama na matundaa ambayo unatakiwa kula makala hii tunatoga special kwa ajili ya waathirika kama wewe kuwa na ukimwi sio mwisho wa kufa."Yalikuwa ni maneno ya jamaa mtanashati ambaye alikuwa naye kama mshauri kwa watu walioathirika na ugonjwa wa ukimwi alinipa sana moyo na wala hakutaka kuniruhusu niondoke kwanza alinihadithia visa vingi sana na kuniambia pia na yeye alikuwa anapenda sana wanawake na kwangu ameshatembea na wanawake wengi kwa kupenda raha hali iliyosababisha mpaka na yeye kuathirika.
"Pablo maisha yangu yamebadilika kwa kweli sasa naishi kwa kujiamini kuliko wengine maisha yangu yananyooka sasa kila ninachogusa dhahabu nimekuwa mshauri na cha kushangaza sasa nina familia yenye watoto wawili ambao sio hata waathirika usisononeke sana Angalia maisha yako mbele." Kila nilipokuwa nakumbuka kuwa nilikuwa na mimi muathirika ndipo machozi yalipochukua nafasi yake baada ya maneno yote ya wale washauri nikaondoka huku mkononi mwangu nikiwa na makala huku nikiwa nimeshika na dawa zangu mpya za Arvs dawa ambazo wenyewe wanaziita vinarefusha maisha kwa kila aliyekuwa na maambukizi ya ugonjwa wa ukimwi.Kabla hata ya kupanda gari ili nirudi nyumbani kwanza nikaenda dukani na kununua mfuko na kuzidumbukiza zile dawa na kile kitabu ili watu wasinione kama nilikuwa nimekanyaga miyawa lakini nilipopiga hatua mbili tu nikakuta uso kwa uso na Elizabeth msichana ambaye aliniambia ananipenda baada tu ya kufika morogoro akiwa na mwanaume ambaye alikuwa ameshika elizabeth kiuno.
"Heeeee pablooo Ushakuwa mwenyeji mpaka huku." Elizabeth akanianza huku akiwa ni mwenye furaha sana mimi nikamtizama kiunyonge na kumjibu.
"Aaaa hamna sema tunazunguka zunguka tujue miji siunajua tena uawezi kukaa tu nyumbani."
"Mmmh ila leo siku ya kazi yote hiii haya bwana frank huyu ni rafiki yangu anaitwa pablo anafanya kazi mtanii kwetu pale anaofisi yake kubwa uaga ninaweka pesa na kutoa pesa ofisini kwake."
"Anhaa pablo nashukuru kukufahamu sana." Alijibu yule jamaa ambaye alikuwa anaitwa frank baada ya kutambulishwa na Elizabeth msichana ambaye kwa muda ule ndio niliuona uzuri wake na jinsi alivyo.
"Haya bwana pablo huyu ndio mume wangu mtarajiwa na hapa tumetoka kupima tupo safi kabisa."
"Haaa jamani hongereni."
"Jamani haya pablo nitakupigia simu baadae baby tuondoke." Roho ilizidi kuniuma baada ya kuwasindikiza kwa macho elizabeth na yule mtu wake ambao niliwaona kama wamekuja kunikejeli na maneno yao eti wametoka kupima na wako safi roho ilizidi kuniuma zaidi baada ya kugundua nilifanya makosa pia kumkataa elizabeth na kukubali kuwa na rozinta.Safari ya kurudi nyumbani ikachukua hatamu nikapanda gari nakueleka nyumbani huku nikiwa na mawazo mengi juu ya kila ambacho kimenitoka.Nikafika maeneo ya nyumbani mida ya kama saa tisa kuendea saa kumi tangia nilipotoka asubuhi nilitaka kwenda nyumbani ninapoishi lakini nafsi yangu ikawa ngumu kwenda nikaamua kutafuta bar nianze kunywa pombe kupoteza mawazo yaliyokuwa yananiandama.Nikafika bar nakuagiza pombe kali aina ya konyagi na kutokana nilikuwa na kama laki moja mfukoni nikaanza kuagiza tu.mpaka saa tatu usiku nilikuwa bado nipo baa nimelewa.Kilichonisaidia ni kwamba pale bar kulikuwa karibu na maeneo ya nyumbani baada ya kumaliza pesa yote kama laki moja nikaanza kujikongoja kurudi nyumbani huku nilipepesuka mkononi wa kulia nikiwa nimeshika ule mfuko uliokuwa una makala ya kitabu na dawa za Arv huku mkono mwingine nikiwa nimeshika chupa ya konyagi.Kila nilipopiga hatua tano mbele ilikuwa lazima nidondoke kutokana na pombe iliyokuwa imeshapanda kichwani sikuwa kimya nilikuwa naimba nyimbo kwa sauti kubwa na kuwakera watu ambao kutokana na usiku ule walijua labda ni mlevi tu mwingine wasiemjua.
"Nyieeee mafalaaa wote humu ndani nifungulieeeenii mlangooooo sasa hiviiiiiii pumbavu nyie wote."Nilifika nyumbani ninapoishi na kukuta geti limefungwa ghadhabu na hasira zikanishika na kujikuta nikianza kutukana huku nikiwa nagonga geti lile kwa fujo.Ghafla mlango ule ukafunguliwa nikakutana uso kwa uso na david ambaye alikuwa ananisubiri nahisi kutokana na mimi kutofungua ofisi ambayo kwa kipindi hicho kutokana na kuniamini katika biashara alikuwa akija mara moja moja kuja kuangalia biashara inaendeleaje.
"Weeeee Pablo tangulini umeanza kunywa pombeeee weweeeee paaabloo."
"Toka zako fala mkubwaaa weeeee hebu nipisheeee....." Kwa akili ya kilevu nikamtukana david kisha nikamsukumiza na kupita pale mlango na kumuacha haamini kile anachokiona.........
TAZAMA KICHEKESHO HIKI KISHA BONYEZA SUBSCRIBE ILIYOPO CHINI YAKE WAKATI TUKIELEKEA KWENYE MUENDELEZO

USIKOSE SEHEMU YA THELATHINI NA MOJA
Maoni, Ushauri na Chochote Share Namimi Katika Mawasiliano Haya:
+255 718 274 413 Ipo WhatsApp
+255 764 339 438
ZephilineEzekiel@Gmail.Com
Maoni, Ushauri na Chochote Share Namimi Katika Mawasiliano Haya:
+255 718 274 413 Ipo WhatsApp
+255 764 339 438
ZephilineEzekiel@Gmail.Com