
SEHEMU YA THELATHINI NA MOJA
"Weeeee Pablo tangulini umeanza kunywa pombeeee weweeeee paaabloo.""Toka zako fala mkubwaaa weeeee hebu nipisheeee....." Kwa akili ya kilevu nikamtukana david kisha nikamsukumiza na kupita pale mlango na kumuacha haamini kile anachokiona.........
SASA ENDELEA...
Moja kwa moja nikaeleka mpaka katika chumba changu huku nikipepesuka pepesuka kutokana na kukosa balance pombe ilikuwa inafanya kazi yake kisha nikazama mfukoni baada ya kuweka mfuko ule chini nikachukua funguo na kufungua mlango ambao ulichukua kama dakika kumi kutokana na jinsi nilivyokuwa nahangaika hangaika kutokana na ukali wa pombe nilizokunywa.Nikafungua mlango na kuingia ndani bila ya kuufunga na wala sikuchukua ule mfuko nilioudondosha nikapita moja kwa moja mpaka kitandani na kujibwaga bila ya kuvua hata viatu na mkono wangu mwingine nilikuwa nimeshika chupa ya konyagi.Nilikuja kushtuka na nilipofungua macho yangu ilikuwa ni Asubuhi kichwa kilikuwa kinaniuma kupita maelezo niliamka na kuangaza angaza ndani nikagongana uso kwa uso na david ambaye alikuwa amekunja uso kwa kukasirika."Eeeee....mmmmh vipi broo david." Niliamka na kukaa sawa huku nikikodoa kodoa macho na kumuangalia david nilipojiangalia mguuni nikaona nipo kitandani na viatu na nilipoangalia kwenye mto nilioulalia pembeni kulikuwa kuna chupa ya konyagi jambo lililonikumbusha kuwa jana yake nilikuwa nimelewa.
"Aaaaa samahani broo halikuwa kosa langu samahani sana nina matatizo makubwaa."
"Pablooo matatizo gani hayo yanakupeleka unywe pombe haya basi naauliza hizo pombe pesa umpepata wapi kwenye hela zangu au pesa zako za mshahara wako nataka kujua please." David aliongea kwa hasira huku akiniangalia kwa kunikazia macho kama mtu ambaye alikuwa tayari kunidhuru.Nikaamka pale kitandani bila ya kujibu kisha nikaangaza macho mpaka nilipouona ule mfuko ambao jana yake niliudondosha mfuko nikauchukua kisha nikazama ndani na kutoka na karatasi ndefu nikamkabidhi david ambaye aliipokea kihasira sana.Ghafla uso wake ukabadilika na kumuona mtu anahema hema juu kila alipokuwa anaisoma ile karatasi alikuwa akigeuka na kuniangalia na kuanza kama kutetemeka alionekana kuogopa kama vile ilikuwa karatasi ya majibu yake kumbe ilikuwa yangu.
"Heeeee lini hiii pablooo??."
"Jana hiyo kaka david."
"Daaa Aisee poleeee sana poleeee."
"Siwezi kupoa david pole haiwezi kubadilisha kitu zaidi ya machungu yanayosababisha nianze hata kunywa pombe sio kusudio langu lakini naona kama ndio njia sahihi yule demu rozinta kumbe sio bwana hakia Mungu najuta kwanini sikusikiliza Maneno ya watu waliponishauri na kuniambia kuhusiana na rozinta kuwa malaya daaah najuta..."
"Aiyaaaaa pablo kwani ulikuwa unaenda naye kavu kavu.??"
"Daaaah hapo ndipo ulipoharibu kila kitu mimi nilikuambiaga mwanangu hii morogoro sio ya kwenda na demu bila ya kuwa na kinga mwanangu daaa."
"Aaaaa nguvu ya mapenzi ndio ilinipeleka ikawa hivyo so yashatokea nitafanyaje.??." David alionekana kuishiwa nguvu kabisa kutokana na majibu yangu kuwa nimeathirika alikuwa akiniangalia kwa huruma sana.Sikuwa na budi tena nikanyanyuka na kuchukua maji na kuchukua vile dawa za Arv ambazo nilikuwa nimeshaelekezwa kila kitu na jinsi ya kuzitumia nikanywa na kumuacha david akiwa katika masikitiko makubwa.
"Pablo nipe pesa za mafao yote kwanza ya mpesa na tigopesa changanya na vile za luku na dstv startimes na zuku." David akaniambia huku akiniangalia kwa huruma na mimi haraka nikaenda mpaka katika droo nakutoa kiasi cha pesa chote kilichokuwepo na kumkabidhi david ambaye alizichukua zile pesa na kuzihesabu na baada ya kumaliza kuzihesabu akakunja uso kwa hasira tena na kuniangalia kwa hasira na kusababisha niiname chini kutokana na kujua nilichofanya.
"Pablo tunaelekea wapi sasa kwa hali yani umenipa hasara ya laki tano? Laki tano kwelii hivi kweli sasa hizo pesa umezipeleka wapi yanii umekaa hapa miezi tisa unaanza kuleta mambo yako haya ya kijinga lakini sawa mimi nimekusamehe kwa sababu najua ulikuwa haujui ulitendalo Sasa basi naomba sasa hivi ukafungue ofisi na uendelee na kazi."
"Haya kaka." Kama ujuavyo ukiingiwa na tabia mpya ni ngumu kabisa kuacha licha ya david kunipa ushauri sana kuhusiana na kunywa pombe nisinywe pombe lakini mimi sikuacha tabia ya kunywa pombe kwangu ilikuwa kama kuvaa nguo vile.Mtaani waliniita mlevi sasa kampani yangu ilikuwa ni kunywa sana pombe kupunguza mawazo.
"Haaa yani kubabeki hapa wala sikubali nife peke yangu nitakufa na watu kibao hapa."Yalikuwa ni maneno yangu nilijiwekea sikutaka kufa mwenyewe na ugonjwa wa ukimwi licha ya kuwa hivyo sikuacha kutumia dawa za Arv lakini nikaanza tabia mpya ya umalaya kila mwanamke nilikuwa naye nilitumia pesa vibaya sana bila ya kuogopa chochote kile kilichokuwa kinapatikana katika ile ofisi ya david nilikuwa nikimaaliza kwa kunywa pombe na kubadilisha wanawake.Mawasiliano yangu na wazazi yalikatika kabisa hakuna simu ya Mama wala ya baba na wala ya david niliiyoipekea tamaa ya pesa ikabadilika na kunishika na kujikuta nikiuza kila kitu kilichokuwepo ndani ya chumba kile nilichopangiwa na david ofisi ya david nikaiuza bila mwenyewe kujua na kugushi ile sehemu kisha nikamuuzia mtu fremu bila ya kuwasiliana na mwenye sehemu na david kisha pesa yote ile nikakimbia nayo na kwenda mjini nakuanza kuitanua ile pesa na kusahau kabisa ule usemi wa Pesa ni za kupita.Kama ujuavyo Mungu akitaka kukueleleza pesa zile nilizokuwa nazo baada ya kwenda morogoro mjini na kupanga chumba cha hoteli huku nikitanua na mrembo niliyemuokota bar aitwaye aisha naye akanidhurumu pesa kwa kukimbia nazo na kuniacho hoteli nikiwa nimelala baada ya kulewa chakali.Hali ikabadilika ghafla nakujikuta nikichanganyikiwa sana katika hoteli ile nikafukuzwa baada ya kiasi nilicholipa kuisha nikaingia mtaani nikiwa nimechanganyikiwa katika jiji kubwa la morogoro sikuwa hata na pesa yoyote mfukoni jambo ambalo lilinifanya nianze kazi mpya ya kupiga debe katika Magari ya mkoa yakuelekea dar-es-salaam sikuwa na makazi ya kuishi nikawa nalala stendi na wenzangu ambao tulikuwa tunapiga nao debe.Kutokana na ugumu wa pesa niliyokuwa napata na kama nilipokuwa na pata ilikuwa pesa ya kula tu ikasababisha niharibu na dozi juu ya Arvs dawa za kurefusha maisha na ikapita kama mwezi pasipo kunywa dawa hiyo hali hiyo ikasababisha nianze kuumwa kidogo kidogo mapele yakaanza kuota katika mwili wangu nakujikuta nikiwashwa sana na vipele hivyo vikubwa ambavyo nilipokuwa navitumbua ni damu tu ndio ilikuwa inatoka.Nilianza kuumwa kidogo kidogo lakini hali ikabadilika sana na kuanza kuumwa sana sikuwa na msaada wowote hakuna mtu aliyenionea huruma nikabaki naumwa sana peke yangu Ugumu wa maisha ndio ukasababisha mpaka wenzangu waliokuwa wanapiga debe na mimi kuniacha na kujitafutiwa wao peke yao rizki.
"Eeee Mwenyezimungu uliyeziumba mbingu na Ardhi naomba uniokoe katika mateso haya ambayo sijui yataisha lini naomba unisamehe kwa yote hayo niliyofanya naomba unisamehe kwa kila nilichofanya na kuwakosea Watu wengi.Najua sina kimbilio lolote zaidi yako sina sehemu yoyote ya kwenda kuweza kuponyeka na hali hii eeee Mungu naomba unisaidie niweze hata kumuona Mama yangu kabla sijafa eeee Mwenyezimungu naomba unikutanishe tena na kila niliyemkosea na kumuomba msamaha kabla sijaingia kaburini nakuomba Mungu wangu nakuomba." Yalikuwa ni maneno niliyoyasema Huku nikiwa nimelala stendi kama chizi kila mtu alipokuwa ananiangalia alikuwa akinionea huruma kwa jinsi nilivyokuwa nimekonda Ni mpiga debe mmoja tu ambaye alinionea huruma sana kila alivyokuwa ananiangalia na kudiriki mpaka kwenda kuninunulia dawa za maumivu na chakula na kunilisha na ndipo nilipoamini pia kuna binadamu katika dunia wanamioyo ya dhahabu sana katika maisha.hakuishia hapo tu akaamua kutafuta mbinu mbadala ya mimi kwenda hospitali akaamua kuchonga bango kubwa na kuandika.
"EWE MWENYE MOYO WA DHAHABU SAIDIA NDUGU YANGU MWENYE TATIZO LA MOYO AWEZE KUTIBIWA CHOCHOTE ULICHONACHA BASI TUNAKUOMBA UCHANGIE KUTOA NI MOYO NA SI UTAJIRI." Maneno yale yule mpiga debe mwenzangu aliyejulikana kwa jina la mkudesimba ndio aliyeshika lile bango huku mimi nikiwa nimelala chini nikizidi kukondeana siku hadi siku huku mapele yakiniandama na kumsisimua kila aliyekuwa ananiona.Wasalimia wema na kila aliyeguswa na hali wakaanza kunichangia kwa wingi na wote wale walionichangia kwa siku ile wakafanikisha mpaka mimi nikafanakiwa kila tulichokuwa tunakihitaji.mkudesimba akanipeleka hospitali ambapo tulipokolewa vizuri sana kutokana na hali yangu kuwa mbaya sana.Matibabu yakaanza kwa kina na zile hela tulizoomba msaada zikasaidia sana mimi kutibiwa na wala mkude simba hakuchukua chochote.Mkudesimba akawaelezea madaktari hali yangu halisi na waliponiomba mimi niwahadithie sikuficha niliwahadithia kila kitu na kumsisimua kila daktari aliyekuwa akisiliza kile nilichoongea.
"Kutokana na Ugonjwa wako huo tutahakikisha utapata matibabu mpaka hali itakapokuwa nzuri bila ya kutoa chochote Mpaka hali itapokuwa nzuri na kisha tutakuruhusu uende kutafuta uwezekano wa kurudi nyumbani kwa wazazi wako." Hakika ule msemo wa atakayefunzwa na mamae hufuzwa na ulimwengu ndipo nilipokubali kuwa msemo ule ulikuwa sahihi kabisa miezi mitatu ikapita nikiwa hospitali natibiwa hali yangu ikarudi kidogo nikawa naweza hadi kukimbia lakini mwili wangu ulikuwa umedhoofu sana nilikuwa nimekonda vilivyo.Kitu kilifanya nishangae na kumshukuru Mungu ni kunipa mkude simba hakika mpiga debe yule alikuwa na mimi bega kwa bega hakuna hata siku moja aliyekosa kuja kuniangalia wakati wote naumwa na hata niliporuhusiwa akanipa habari mpya.
"Pablo nimepata zari Mwanangu kuna mishe niliipiga ya kupaki mzigo kama mwezi hela niliyoipata imeniwezesha nipange chumba." Ilikuwa habari nzuri sana kwake na kwangu tabu ya kuumwa na mbu na kulala stedi niliona imeisha kabisa.kule hospitalini nikapewa dawa za Arvs za kutosha huku wakinisisitizia nifanye kazi kwa bidii niweze kupata mlo mzuri kidogo pia niliambia nifanye sana mazoezi kwa bidii zote.Tukarudi kazini kupiga debe upya na dawa zile zikanisaidia kurudisha hali yangu lakini licha nilikuwa nimekonda vile vile iliyoniwezesha mimi na mkude simba kutafuta riziki.Nakumbuka siku moja tukiwa tunapiga debu kuita abiria ghafla nikaona umati mwingi wa watu wakikusanyika sehemu mmoja na kuangalia kitu ambacho sikujua kwa wakati ule kilikuwa nini.Nikajikuta nikipatwa na shauku kubwa ya kutaka kujua kinachoendelea nikajisogeza mpaka watu wale walipo na kukuta kila mtu akiongea lake.
"Aaaaiyaaaa huyu demu namjua alikuwaga malaya sana."
"Daaaa kafa kifo cha kinyama sana ona." Yalikuwa maneno yaliyonivutia sana baada ya kupenya katika masikio yangu nikajipenyeza penyeza kwa watu sana maana watu walikuwa wengi nakuona gari ya mapolisi aina ya defender ilikuwa imezingirwa na watu ambao mapolisi hao walikuwa wanawaambia watu wawapishe.Nyuma ya ile defender kilikuwa na mwili ambao ulikuwa umefunikwa na kutokana na udogo wa lile shuka lilipelekea ule mwili ufunikwe kuanZia kifuani mpaka katika miguu huku sura yake ikiwa wazi.Nikajitutumua na kuangalia ile sura ilikuwa ni ya nani nikajikuta nikitoa macho nikiwa siamini kabisa kile nilichokiona.
"Aaaaaaaa rozintaaa.!!" Alikuwa si mwingine bali ni rozinta ndio ulikuwa mwili wake ndani ya pick up ya ile defender kwa hakika ilikuwa ni jambo la kusikitisha.sikujua aliuliwa na nini lakini wingi wa wale watu waliozingira ile defender ambayo sikujua kwanini ilipita pale wavuta bangi wasiokuwa na akili mmoja akajikuta akashika lile shuka na kulitoa lile shuka alilofunikwa rozinta na rozinta kubaki mtupu huku mwili wake ukiwa una damu nyingi sana.Mtafuruku ndipo ulipoanzia wale polisi waliokuwepo ndani ya defender wakawaita polisi wenzao ambao gari aina ya defender kama nane zilimiminika kwa wingi pale kituoni na kuanza kukamata kamata watu.Mimi na mwenzangu mkudesimba tulikimbilia nyumbani kwetu na kuwakimbia wale mapolisi walikamata wengi pale sikuile na hakukua na kazi yoyote hakuna hata mpigadebe aliyepiga kutokana na hali ile.Roho iliniuma nilipokumbuka nilichokiona kwa rozinta msichana ambaye alinifanyia mambo mengi sana.
"Pumzika kwa amani rozinta mimi nishakusamehe kwa yote yale uliyoyafanya." Hali ya salama ikarudi tena stendi tunayopiga debe mimi na mkude simba ambao kwa kipindi tulikuwa ndugu na kushirikiana ninachokipata mimi tulikuwa tunachangia na hata alichopata mkudesimba tulikuwa tunachangia wote.Maisha mimi na mkude yakazidi kutonyookea baada ya sisi wawili kupata tenda ya kuita abiria katika gari mpya ambayo wapiga debe tulikuwa wawili tu katika magari hayo hali ile ikasababishwa tulipwe pesa nzuri.Kuna kipindi nilipata pesa nzuri tu nakukata shauri ya kwenda kwa david lakini nilipokumbuka nilichomfanyia niliogopa sana na hata nilipotaka kwenda kwa wazazi wangu ambao ilipita mwaka wa pili kuelekea watatu nilikuwa sijawaona wala kuwasiliana nao niliona aibu kwenda na kuogopa na nilijua wazi kuwa nilichofanya kilikuwa si sahihi na wala sikupaswa kusamehewa.Siku moja nikiwa katika purukushani zangu za kutafuta riziki kama kawaida ghafla nikashangaa nikiitwa.
"Weeee Pabloo!,pablooooo!!,pablooooo!!!," Niligeuka kwa shauku macho yakanitoka na moyo ukaanza kunienda mbio baada ya macho yangu kugongana na Mama akiwepo na baba wakiambata na david ambaye alikuwa akiniita.Nikajikuta nikitaka kukimbia lakini miguu yangu ilikuwa mizito mno david akanikimbilia na aliponifika akanishika mkono baba na Mama wakajiongeza na wao wakanisogelea.Vilio ndio vilisikika hapo nilijikuta nikiangusha kilio na kusababisha watu stedi kutuangalia huku wengine wakidhania labda nimeiba kutokana na kunijua na wao wakajisogeza kuja kuangalia nilivyokuwa nimepiga magoti huku nikilia.
"DAVID NAOMBA UNISAMEHE HALIKUWA KUSUDIO LANGU NAJUA ULINIFANYIA WEMA MIMI NIKAKULIPA KWA UBAYA NAJUA SISTAHILI KUISHI KWA YALE NILIYOKUTENDEA NAOMBA UNISAMEHE NAKUOMBA UNISAMEHE DUNIA IMESHANIFUNZA..." Nilimwambia david huku nikimsika miguu yake nikiwa nimepiga magoti huku nikilia na kumuomba msamaha kisha nikahamia kwa wazazi wangu waliokuwa nao wote wananiangalia huku wakilia.
"MAMA BABA NISAMEHENI MMENIFANYIA KILA KITU NILICHOKUWA NAKIHITAJI MMENIFANYIA KILA KITU ILI NIFURAHIA LAKINI MWISHOE NIMEWAABISHA SANA NIMEWALETA UGONJWA MBAYA WA UKIMWI KUTOKANA NA KUTOSIKILIZA NAOMBENI MNISAMEHE NAOMBENI MNISAMEHE." Katika dunia hakuna msahama ambao hausameheki hata siku moja david kwa moyo wake wa ukarimu akanishika mkono na kuninyanyua kisha akanikombatia na kuniambia hakuwa na kinyongo na mimi na alishanisamehe muda mrefu na hata baba na mama waliniambia wamenisamehe na wamekuja morogoro kuja kunichukua.Nililia sana kumuacha mkudesimba ambaye naye alilia sana kuniacha lakini hakukuwa na jinsi tukaondoka Morogoro mimi na baba na mama tukimuacha david ambaye baada ya kumuhadithia wema alionifanyia mkudesimba akaahaidi kumsaidia na kweli alimtafutia kazi nzuri iliyomuwezesha mkude simba anunue na simu ambayo aliwasiliana mimi kuwa david amemsaidia sana.Nilirudi dar kama kawaida na kuanza maisha mapya dar-es-salaam baba akanitafutia kazi mpya ambayo niliifanya kwa bidii sana na kufanikiwa sana kimaisha.Maisha yalisonga yale yote niliyofundisha na ulimwengu yalinifunza sawasawa licha ya kuwa na ukimwi lakini nikapata Msichana mzuri aitwaye Angel msichana ambaye alinipenda na kukubali naye kuwa na ukimwi kwa sababu yangu.Mungu akatujaliia kupata mtoto wa kike na tukaona kabisa Arvs zilikuwa Muangaza wa maisha yetu tulitumia dozi ipasavyo uzuri ni kwamba hata mtoto wetu wala hakuathirika kama sisi tulipewa njia salama ya kuweza kumlinda mtoto wetu.Maisha yalisonga sana na nilijifunza sana kutokana na makosa niliyoyafanya nilijisikia raha aiseee kumbe raha tu pia kuishi ukiwa na umeathirika na kama ukifuatisha masharti utaishi kwa raha mustarehe..............
TAZAMA KICHEKESHO HIKI KISHA BONYEZA SUBSCRIBE ILIYOPO CHINI YAKE WAKATI TUKIELEKEA KWENYE MUENDELEZO

MWISHO
Maoni, Ushauri na Chochote Share Namimi Katika Mawasiliano Haya:
+255 718 274 413 Ipo WhatsApp
+255 764 339 438
ZephilineEzekiel@Gmail.Com
Maoni, Ushauri na Chochote Share Namimi Katika Mawasiliano Haya:
+255 718 274 413 Ipo WhatsApp
+255 764 339 438
ZephilineEzekiel@Gmail.Com