AISEE KUMBE RAHA (31)
JINA: AISEE KUMBE RAHA Mwandishi: Pablo SEHEMU YA THELATHINI NA MOJA ILIPOISHIA... "Weeeee Pablo tangulini umeanza kunywa pombeeee weweeeee paaabloo." "Toka zako fala mkubwaaa weeeee hebu nipisheeee....." Kwa akili ya kilevu nikamtukana david kisha nikamsukumiza na kupita pale mlango na kumuacha haamini kile anachokiona......... SASA ENDELEA... Moja kwa moja nikaeleka mpaka katika chumba changu huku nikipepesuka pepesuka kutokana na kukosa balance pombe ilikuwa inafanya kazi yake kisha nikazama mfukoni baada ya kuweka mfuko ule chini nikachukua funguo na kufungua mlango ambao ulichukua kama dakika kumi kutokana na jinsi nilivyokuwa nahangaika hangaika kutokana na ukali wa pombe nilizokunywa.Nikafungua mlango na kuingia ndani bila ya kuufunga na wala sikuchukua ule mfuko nilioudondosha nikapita moja kwa moja mpaka kitandani na kujibwaga bila ya kuvua hata viatu na mkono wangu mwingine nilikuwa nimeshika chupa ya konyagi.Nilikuja kushtuka na nilipofungua macho yangu ilikuwa…