LISEME JINA LANGU (10)

Zephiline F Ezekiel
LISEME JINA LANGU (10)
JINA: LISEME JINA LANGU Mwandishi: Pablo SEHEMU YA KUMI ILIPOISHIA... Macho yangu kakuta na mzee gardner aliyekuwa akikimbia kwa kasi na kunifanya mimi nizidi kuwa na hofu kubwa iliyosababisha nipigwa na butwaa la nguvu. SASA ENDELEA... "Pablo kimbiaaaaaaa" maamrisho ya kukimbia hakuniingia kabisa nikajikuta miguu yangu ikifa ganzi na kujikuta nikiendeleaa kusimama pale pale na kuangalia nini kilichomfanya mzee gardner kukimbia.nikiwa katika mshangao ghafla gari kubwa likatokeza na kufungwa breki umbali kidogo na nyumba yetu pale kisha watu wapatao ishirini wenye kuvaa miwani meusi na suti nyeusi wakashuka huku wakiwa na silaha ambapo baada ya kushuka tu wakaanza kunimiminia mimi risasi ambazo zote hazikunipata kisha na mimi pia nikaanza kukimbia kwa kasi.nilianza kukimbia na kuanza kuita jina la gardner bila mafanikio huku kila nilipokuwa naangalia nyumba nilikuwa nafuatwa na watu wale ambao nilishawajua walikuwa ni wafuasi wa robertson.sikutaka kumpambana nao peke yangu kwa kuho…