
SEHEMU YA KUMI
Macho yangu kakuta na mzee gardner aliyekuwa akikimbia kwa kasi na kunifanya mimi nizidi kuwa na hofu kubwa iliyosababisha nipigwa na butwaa la nguvu.SASA ENDELEA...
"Pablo kimbiaaaaaaa" maamrisho ya kukimbia hakuniingia kabisa nikajikuta miguu yangu ikifa ganzi na kujikuta nikiendeleaa kusimama pale pale na kuangalia nini kilichomfanya mzee gardner kukimbia.nikiwa katika mshangao ghafla gari kubwa likatokeza na kufungwa breki umbali kidogo na nyumba yetu pale kisha watu wapatao ishirini wenye kuvaa miwani meusi na suti nyeusi wakashuka huku wakiwa na silaha ambapo baada ya kushuka tu wakaanza kunimiminia mimi risasi ambazo zote hazikunipata kisha na mimi pia nikaanza kukimbia kwa kasi.nilianza kukimbia na kuanza kuita jina la gardner bila mafanikio huku kila nilipokuwa naangalia nyumba nilikuwa nafuatwa na watu wale ambao nilishawajua walikuwa ni wafuasi wa robertson.sikutaka kumpambana nao peke yangu kwa kuhofia kwamba wapo wengi.mbio zangu ziliishia katika kichaka chenye majani mengi ambayo yalinisaidia kujificha na kuanza kuangalia nini kinachofuata hakika nilipotezana na mzee gardner alitangulia kukimbia nikiwa katika hali ya kujificha bahati nzuri nilikuwa sijasahau upinde wangu na mshale ambayo nilianza kuiweka sawa baada ya kumuona jamaa mmoja ambaye alikuwa kashikilia risasi vizuri huku sura yake akiwa ameikunja kuasiria kwamba yupo kazini.ghafla mzee gardner akatokea pasipo julikana na kwenda kumkaba jamaa huyo ambaye baada ya kukabwa akatoa roba ya mzee huyo na kuanza kumtembezea kichapo kikali kilichoniogopesha sana na kujikuta nikishindwa hata kuingilia kutokana na nguvu nyingi alizokuwa nazo jamaa huyo.baada ya kuhakikisha kuwa kamdhibiti jamaa huyo akaokota bunduki aliyoidondosha wakati akipigana na mzee gardner kisha bila hata ya kuremba akafyatua risasi iliyompata sasa mzee gardner ya kichwa na kufa hapo hapo.hakika macho yangu yakanitoka ghafla nikajikuta nikipiga kelele na kutoka kichakani na kwenda kumvamia jamaa huyo kisha.............
Kilichonigharimu kuwa kwa wakati huo nikiwa na hasira ambazo zilizokuwa zimefika pomoni nikajikuta kwa hasira nikimvamia jamaa huyo ambaye baada ya kusikia kelele zangu huku nikiwa namfuata kwa mfumo wa kukimbia jamaa huyo akazunguka kwa kipiga msamba ambapo akanikwepa kisha mimi nikajikuta nikivamia mguu wake alioutegesha baada ya kupiga msamba na kusababisha mimi nijikwae katika mguu wake na kudondoka vibaya huku speed yangu ya kukimbia ikasababisha nirushwe vibaya baada ya kukwaa mguu huo.hali ya kubimbirika ndio ikafuata huku na kusababisha nipate maumivu makali sana ya mgongo.nikaanza kunyanyuka kwa shida sana huku nikiugulia lakini kabla hata sijanyanyuka ngumi kali sana ya uso iliyonitoa damu puani ikatua katika uso wangu na kunirudisha tena chini huku maumivu ya mgongo sasa yakaanza kuchanganyika na uso kutokana ngumi niliyopigwa ilikiwa ni kali sana tena ikazidi kuniua nguvu.hasira zote nilizotoka nazo zikaisha na kujikuta tena nimepoa.juhudi zangu tena zikagonga mwamba baada ya jamaa huyo huyo tena kunikalia kwa juu na kuanza kushambulia tena uso wangu kwa ngumi nyingi nyingi na kuzidi kunipasua uso wangu ambao nilijaribu sana kujiziba kwa mikono lakini jamaa huyo akafanikia tena kunikamata mikono yangu vizuri katika miguu yake na kunizidi nguvu kabisa iliyosababisha nishindwe kumtoa juu aliponikalia na kumpa nafasi ya kunisambulia kwa ngumi zilioambata na vichwa vikali vilivyozidi kuleta maafa katika sura yangu.baada ya kushindwa kabisa kutoa katika mwili wangu nikajifanya nimezimia baada ya ngumi zisizo na idadi kuzidi kumiminika nikajifanya nimepoteza fahamu na kusababisha jamaa huyo aache kunisambulia na kisha akanyanyuka.kupitia jicho langu moja niliangalia kidogo huku nikimzuga jamaa huyo ambaye alidhania nimezimia nikamuoana akichukua bunduki aliyoiyutumia kumuulia mzee gadner na kuanza kurekebisha vizuri kwa kuiweka risasi na kujiandaa kunielekezea mimi.ile kwangu ndio ilikuwa nafasi kubwa sana niliyoipata baada ya kumuona jamaa huyo akiwa anajiandaa kunipa risasi huku miguu yake akiwa kajichanua.kwa nguvu zote huku nikiwa nimelala nikampigapp jamaa huyo teke kali sana lililompata sehemu nyeti katika silaha yake anayoitumia katika uwanja wa mapenzi na kumfanya atoe ukelele mkali sana wa maumivu na kujikikuta akiachia bunduki yake aliyoishika na kuidondosha chini huku naye akadondoka chini huku akipiga magoti na mikono yake ikiwa imeshika sehemu ile niliyompiga.nikabimbirika kidogo kisha nikajibetua kwa ufundi na kusimama na kwa mwendo wa taratibu nikaenda kuichukua bunduki ile aliyoidondosha na kumuelezea huku nikimuangalia kwa jicho la hasira kali.
"Fuck you fuck you Msenge wewe unasubiri nini niue sasa mrembo wew" yule jamaa akaanza kunishambulia kwa matusi huku akijaribu kunitemea mate mdomo wangu ulikuwa mzito sana kumjibu huku nikiwa na hamu kubwa sana ya kumjibu.kumbukumbu ya kukumbuka kuwa alikuwa hayupo peke yake ndio ilinishtua na kujikua nikimfyatulia risasi iliyompata sawa sawa katika kichwa na kufumua kabisa ubongo wake ulimwagika baada ya kumpiga risasi ile.nilimsogelea mzee gardner ambaye roho yake ilikuwa ishaacha mwili lakini kabla hata sijainama kumuangalia mzee gardner wafuasi wengine wapatao watano wakiwa wanakimbia nikawaona kabla hata wao hawajaiona bila ya kuchelewa kupitia bunduki ile niliyokuwa nayo kwa shabaha ya hali ya juu nikawafyatua wote watano waliopoteza maisha hapo hapo.sikutaka kwanza kushughulika na mzee gardner baada ya kukumbuka kuwa licha ya kuwauwa wafuasi sita nikakumbuka kuwa walikuwa wengi na nilikuwa sina budi kukabiliana nao sikutaka tena kuvaana nao kwa kutumia risasi nikachukua mshale niliokuwa nao kisha nikaanza kuwafuata kwa mwendo wa kujificha ficha.nikiwa katika mawindo nikawaona wafuasi wengine wakiwa wamekaa baada ya kuonekana kama walikuwa wamechoka.kwa hali ya kujificha nikaanza kuwalenga wote wanne ambao baada ya kufyatua mmoja wao mshale wa jicho ambao ulisababisha wengine wachanganyikiwe na kuanza kutaka kukimbia lakini sikuruhusu hata mmoja kunitoka machoni mwangu wote niliwashambulia kwa mishale niliyokuwa nayo na kuwauwa.hakika kila nilipokuwa nakutana nao niliendelea kuwauwa kwa mishale yangu na kusababisha vifo vya wafuasi wale wapatao ishirini ambao nilihisi kuwa walikuwa wametumwa na robertson.Baada ya kumaliza shughuli ya kuwauwa wale wafuasi wa robert nikaenda katika mwili wa mzee gardner ambapo kwa kutumia mawe nikaanza kumzika kwa kumfunikia na mawe hayo mzee huyo ambaye sitamsahau kamwe mpaka nakufa kutokana na kukaa naye katika muda mchache na kujua vitu vingi katika maisha yangu katika kipindi hicho kigumu nilichopitia.baada ya kumaliza kumzika nikamswalia na kumuombea kisha nikaanza kuondoka huku nikikumbuka kuwa kulikuwa na gari walilokuja nalo ambalo nilitaka kulitumia kwenda jijini dar ambapo nilikuwa na kazi moja tu ambayo ni ya kwenda kumuua robertson mugalula na baba yake moureen kwa kulipiza kisasi cha familia yangu,mzee gardner na moureen ambaye licha ya kuambiwa na robertson mugalula kuwa alishamuua lakini nilitaka kwenda kuhakikisha.nikajiandaa vizuri kwa kuchukua mshale ikifuataiwa na baadhi ya bunduki za wale wafuasi niliowauwa kwa kutumia mishale.baada ya kumaliza nikaelekea katika gari lile aina ya basi kubwa la wale wafuasi waliokuja lakini baada ya kulifikia karibu nilimuona mtu aliyekaa katika sehemu ya dereva huku akiwa amelala. nikanyata mpaka katika mlango wa dereva ambao baada ya kujaribu kuufungua nikagundua haujalokiwa nikiwa nimejiandaa kwa silaha nikaufungua mlango alikaa dereva yule na kumrusha kutoka kiti alichokaa mpaka chini ambapo kutokana alikuwa ana usingizi mzito akajikuta akishtuka sana na kubaki akitumbua macho.akiwa katika hali ya kushangaa nikamtandika na kitako cha bunduki kilichomzimisha kisha nikamfunga kamba na kumpandisha kwenye gari na mimi kukaa katika siti ya dereva na yeye kumueka katika sehemu ya pembeni ya siti ya dereva.sikutaka kumuua kwa sababu nilitaka msaada wake kwanza kabla ya kumuaa.Nikiwa katika harakati za kumsubiria ahamke ghafla dereva yule akaamka kwa muda wa kama lisaa na kuanza kutetemeka baada ya kuniangalia mimi nilikuwa uso wangu umetapaakaa damu kutokana na zile ngumi kali za yule jamaa zilizonipasua sana huku nikiwa nimeikunja kwa hasira.
"Pleaase naomba usiniuwe usiniuwe mimi sina hatia bado Familia yangu inaniitaji mimi dereva tu nionee hurumaa."
"Umetumwa na nani uwaendeshe hawa jamaa waje kuniua."
"tamaa tu ya pesa nimetumwa na muhesimiwa robertson mugalula naombaa usiniuwe iihiiiiiii iiiiiiiiiiiiiiiiii"
"sitaki kusikia na kuona machozi yako kwa sababu una nipigia kelele nitakuua sasa hivi pumbavu wewe robertson yupo wapi"
"yupo kwake sasa hivi na familia yake wakijiandaaa mipango yao ya harusi"
"Harusi???? anamuoa nani??"
"sijui mourina"
"Whaaaaattttt???"
"ee...a..na..itw mouria..."
"Lini anamuoa"
"Kesho mkuu ila naomba usiniuee" hakika habari zile zilikaanza kunipa nguvu ya ajabu kidogo kidogo kutokana nikaanza kutoa hofu juu ya moureen ambaye nilidhania kua walishamuua na kisha nikamfungua jamaa huyo dereva aliyeitwa steven kisha nakuanza kumuelezea matukio yote ambapo kwa huruma akahidi kunisadia kwa wakati huo.nilimpisha katika siti ya udereva ili aendeshe yeye mwenyewe.Akili yangu ikaanza kuwaza kesho nakuanza kufikiria nitasimamishaje kesho yake harusi ya robertson na moureen ambayo amri mashauri yangu ya kichwa yakaanza kufikiria ulinzi utakuwepo katika harusi hiyo kutokana na kumjua vizuri robertmugalula.....
Safari yetu ikaanza kwa spidi kubwa kutokana na dereva huyo kuwa Makini sana na uwezo mkubwa wa kuendesha gari. kwa muda huo ilikuwa kama saa kumi na mbili jioni inaelekea saa moja usiku.wakati wote tukiwa barabarani dereva alikuwa anawaangalia angalia wenzake ambao kutokana na pesa kubwa aliyokuwa nayo Robert mugalula aliwaweka katika Barabara zote.Tukiwa tunakaribia kuvuka mataa ya mwenge ghafla gari yetu ikasimamishwa na waliotusimamisha walikuwa si wengine Bali ni majamaa wawili waliovaa suti safi kabisa nyeusi na miwani yao na muda wote walionekana wapo kikazi zaidi kutokana na kuonyesha katika sura zao.
"steven vp hali ya huko mmefanikiwa??" jamaa mmoja kati ya wale wawili akamuuliza swali dereva wakati huo mimi nilikuwa tayari nishajificha na nilikuwa nasikia yote yaliokuwa yanaongelewa.
"n...di..oo.mkuuu wameshamaliza kazi mbona"
"wapo wapi sasa mbona gari jeupe Maana boss robert Alikuwa anasubiri Majibu kutoka kwenu kupitia Alexandre ambaye mpaka sasa simu yake inaaita Bila ya kupokelewa"
"Aaaa siunajua wale wanapesa bana ndio wamebaki wanakunywa Mapombe yao huko huko Ila Na tumaini Waturudi....Mhesimiwa"
"Mmmh Alexandre Bana naye basi sawa wewe kapumzike mpaka kesho wewe si umepewa kadi ya Harusi??"
"Nimepewa Nitakuja" steven alimwambia Jamaa huyo ambaye baada ya kuambiwa hivyo akaturusu tuondoke hapo mimi ndio niliboibuka Baada ya kujificha.Safari yetu ndefu kutoka Bagamoyo porini ikagota katika Mitaa ya Magomeni katika Nyumba aliyopanga steven na kushuka Hapo Ambapo Bila ya hiyana steven akanikaribisha kwake.Licha ya kuniambia Alikuwa anafamilia nisimuue familia yenyewe sikuoni Hali iliyonifanya niwe na Machale machale naye.hakika kama inavyosema usimuamini mtu usiyemjua hali hiyo ya kutomwamini steven ilitawala katika kichwa changu na kujikuta Nikijiandaa Muda wote na kama kikinuka basi mimi nilikuwa tayari kabisa kukiendeleza.Nilijikuta nikikataa chakula alichopika na kumshangaza sana.
TAZAMA KICHEKESHO HIKI KISHA BONYEZA SUBSCRIBE ILIYOPO CHINI YAKE WAKATI TUKIELEKEA KWENYE MUENDELEZO

USIKOSE SEHEMU YA KUMI NA MOJA
Maoni, Ushauri na Chochote Share Namimi Katika Mawasiliano Haya:
+255 718 274 413 Ipo WhatsApp
+255 764 339 438
ZephilineEzekiel@Gmail.Com
Maoni, Ushauri na Chochote Share Namimi Katika Mawasiliano Haya:
+255 718 274 413 Ipo WhatsApp
+255 764 339 438
ZephilineEzekiel@Gmail.Com