LISEME JINA LANGU (11)

Zephiline F Ezekiel
LISEME JINA LANGU (11)
JINA: LISEME JINA LANGU Mwandishi: Pablo SEHEMU YA KUMI NA MOJA ILIPOISHIA... Hakika kama inavyosema usimuamini mtu usiyemjua hali hiyo ya kutomwamini steven ilitawala katika kichwa changu na kujikuta Nikijiandaa Muda wote na kama kikinuka basi mimi nilikuwa tayari kabisa kukiendeleza.Nilijikuta nikikataa chakula alichopika na kumshangaza sana. SASA ENDELEA... "ilikuwaje mpaka ukawa unafanya kazi na robertson" "Ugumu wa Maisha kaka halafu mimi ni Dereva mwenye vyeti vizuri Mimi kwa robertson nilionganishiwa tu na Rafiki yangu mmoja hivi" "Oooo kwa hiyo ushawai kuuua" "Aaaaaa...hapana mimi..sio jambazi kaka mimi dereva tu nawapeleka wanafanya kazi zao kisha Tunarudi" "Ni kazi gani wanazofanya Ambazo wewe unawapeleka" "Kama kuua,Kwenda kuiba kwenye Mabenki haya katika shughuli za Madawa ya kulevya yote hayo" hakika siku hiyo tuliongeaa mengi Lakini kila nilipokuwa nakumbuka harusi kesho ya robert akimuoa moureen ndio ilinifanya niwe na sh…