LISEME JINA LANGU (11)

Zephiline F Ezekiel
0
Mwandishi: Pablo

SEHEMU YA KUMI NA MOJA
Hakika kama inavyosema usimuamini mtu usiyemjua hali hiyo ya kutomwamini steven ilitawala katika kichwa changu na kujikuta Nikijiandaa Muda wote na kama kikinuka basi mimi nilikuwa tayari kabisa kukiendeleza.Nilijikuta nikikataa chakula alichopika na kumshangaza sana.

SASA ENDELEA...
"ilikuwaje mpaka ukawa unafanya kazi na robertson"
"Ugumu wa Maisha kaka halafu mimi ni Dereva mwenye vyeti vizuri Mimi kwa robertson nilionganishiwa tu na Rafiki yangu mmoja hivi"
"Oooo kwa hiyo ushawai kuuua"
"Aaaaaa...hapana mimi..sio jambazi kaka mimi dereva tu nawapeleka wanafanya kazi zao kisha Tunarudi"
"Ni kazi gani wanazofanya Ambazo wewe unawapeleka"
"Kama kuua,Kwenda kuiba kwenye Mabenki haya katika shughuli za Madawa ya kulevya yote hayo" hakika siku hiyo tuliongeaa mengi Lakini kila nilipokuwa nakumbuka harusi kesho ya robert akimuoa moureen ndio ilinifanya niwe na shauku nilipomuumwambia steven yeye akaniambia atanisaidia na michogo yote nimuachie yeye.Kama kawaida mida ya saa nne nne usiku wote tukajikuta tukilala.Kwa mimi Nilizuga kama nimelala lakini ilikuwa ni kama kumzuga Steven ambaye kwa muda huo alishajua kuwa nilimuamini vya kutosha na kumuachia yeye kila kitu.katika mida ya saa sita sita hivi usiku ghafla steven dereva akaamka alipoamka akanisogelea mpaka nilipo mimi na kuanza kuniangalia kwa muda na kuanza kunitingisha tingisha vizuri kwa lengo la kujua je nimelala fofofo au la.mimi kama kawaida nilijilegeza kabisa na kujifanya nimelala usingizi mzito kwa lengo la kumzuga kabisa steven ambaye baada ya kugundua kuwa nimelala kabisa fofofo akanyata na kwenda kuchukua simu yake ya mkononi niliyomuana nayo ameishika mkononi kisha mdogomdogo akaanza kutoka nje kwa mwendo wa kunyata.Baada ya kutoka nje mwanaume kwa hasira nikanyanyuka na kunyata kisha nikaufungua Mlango polepole na kutoka nje.Macho yangu yalimshuhudia steven akiwa anabonyeza bonyeza simu mara aweke sikioni Mara andike andike namba alionekana kama aliyekuwa akimpigia alikuwa apatikani.bila ya kusita nikamsogelea kwa nyuma na kumshtua kwa kumgusa bega lako ambalo baada ya kugeuka tu akarusha ngumi kali iliyonipata sawa sawa kichwani na kuniyumbusha kidogo.nikiwa katika maandalizi ya kukaa sawa tena akaachia teke ambalo nilikwepa sawa sawa lakini nikalisahau na lingine lililotua kifuani na kunidondosha chini.nikajibetua na mfumo wa kuruka beki na kukaa sawa kisha nikaanza kumsogelea taratibu dereva steven ambaye kwa mara ya kwanza nilijua hajiwezi kabisa kumbe alikuwa naye ana gusa gusa mkono.nikamsogelea lakini kabla sijamfikia akabetuka mateke mawili dabo yaliotua kifuani kwangu na kuniyumbushia lakini safari hii sikudondoka kwa awali nilirudi nyuma kidogo.Kwa hasira nikamsogela tena na kumuacha steven tena akirusha makonde mawili makali yalionipata vizuri usoni na kunitoa damu ambazo niliishia kutema chini kisha nikaendelea kumsogelea tena kwa hasira nzito.kwa hali ile ya kudindisha kila anachonipiga na mimi kuzidi kumsogelea aniongezee kumlimshua sana dereva ambaye baada ya kunipiga mpaka Akachoka.

Steven baada ya kuona hali imekuwa ngumu upande wake akaanza kuniomba msamaha huku akirudi kinyume nyume na hakusita kutoa machozi yaliozidi kunipandisha hasira kali na kuzidi kumfuata huku nikiwa tayari nishakunja ngumi kwa lengo la kumshambulia pale tu nitakapomfikia.safari ya steven kurudi kinyume nyume iligota katika mlango ambao licha ya kuusindika tu akaanza kuangaika nao kufungua kama vile umefungwa vile.bila ya kuchelewa nilipofikia tu Nikamtandika teke kali lilompeleka mpaka ndani na kumfanya aanze kupiga kelele za maumivu niliingia mpaka ndani kisha nikamuinua na kwenda kumbamiza katika tv yake ya flatscreen na kumpasua kichwa chake kidogo na kuanza kutokwa na damu kichwani.sikutaka tu kuishia hapo nikaendelea kumshambulia kwa ngumi kalo zisizokuwa na idadi mpaka nilipoona awezi kuinuka kisha nikamuachia akiwa anavuja damu huku akiugulia kimya kimya kwa maumivu.

"Nilisikia pale kwamba una kadi ya mualiko hiyo kadi ipo wapi??"
"A..aa...aa.......ka.d.dii...ipii"
"Usinifanye mtoto nitakuua nilisikia pale ulipokuwa unaongea na yule mwenzako"
"M...ssssijui"
"ok" Sikutaka kuendelea kumuongelesha kwa haraka nikajikokota mpaka katika mfuko wangu na kutoa upinde wangu wa mshale kisha nikachomeka mshale na kwa haraka nikaweka na kumfyatulia Mshale katika Mguu wa steven hali iliyomfanya apige ukelele wa juu kabisa ambao kabla hata hajaendelea tena nikawahi na kumziba mdomo.
"Hey hebu nambie kwa mara ya mwisho kabla sijakumaliza safari hii je kadi ya mualiko wa harusi ipo wapi.??"
"I...po..kwen...ye be.gi Pale..." kwa haraka nikanyanyuka na kwenda katika begi lake kisha nikalifungua na kuanza kupekenyua pekenyua na kisha kwa macho yangu nikaiona kadi na kuitoa.nilikaribishwa na picha ya moureen aliyokumbatiwa na robertson katika pozi nene lilinifanya nitoe msonyo wa hali ya juu.hakika kadi ile ilikuwa imepambwa pambwa vizuri nakaanza kuangalia kadi hiyo na kuanza kuisoma kwa umakini kidogo

"Nathan church posta..??" nililitaka jina hilo la kanisa lilinifanya nirudi nyuma kifikra kidogo baada ya kulikumbuka kanisa hilo ambalo nilishuhudia kwa Macho yangu jackline mpenzi wangu wa kwanza kuolewa na mtu mwingine.Hakika kufanyika harusi ile katika kanisa hilo lilinipa kamshangaao fulani ambao ulinionyesha ni kama kamchezo lakini kwa upande wa pili niliona ni njia rahisi kutokana na kulijua vizuri kanisa hilo.Nikaendelea pia kuangalia je ni mchungaji atakaye fungwa hiyo ndoa na kuona pia jina lake.sikutaka tena kuichukua kadi hiyo ya nikarudisha mule mule kwenye begi kisha nikakusanya mzigo wangu niliowekea upinde na mishale yangu.nilipomaliza nikaenda mpaka katika suruali ya steven na kuchukua wallet yake iliyojaa pesa iliyosababisha mpaka itune kisha nikachukua pesa kiasi bila hata ya kuzihesabu wakati huo steven alikua bado ananiangalia huku akiugulia maumivu ya mshale ule niliompiga ambao ulikuwa bado upo ndani ya paja.Nikamsogelea na kuuchomoa mshale huo na kuziba mdogo wake kwa nguvu ili asipige ukelele.

"Wahi hospitali kabla haujafa Maisha mema" nilimuaga kwa staili hiyo kisha nikatoka nje na kushika hatamu ya kwenda kutafuta gesti usiku huo huo ikiwa mida ya saa nane nane.Hakika Mipango yangu yote ilivurugika kutokana na kumuamini steven ilinibidi nibadilishe mipango na kuandaa mipango mingine ambayo ilinilazimu nifanye chini juu niweze kufika kanisani Asubuhi na Mapema kutokana na ndoa hiyo kufungwa saa Mbili Asubuhi.Nilifanikiwa kupata gesti ya mapema kabisa katika mitaa ya kariakoo mida ya saa tisa na kulala usingizi wa kushtuka shtuka kwa lengo ili nisichelewe.Nililala kidogo tu lakini niliposhtuka saa ukutani katika gesti hiyo ikaonyesha saa kumi na Moja asubuhi nikajivutavuta na kuamka kisha kwa haraka haraka nikatoka huku nikiwa na mzigo wa mishale yangu na upinde nilioweka katika mfuko mkubwa mfano wa gunia mweusi uliokuwa hauonyeshi kisha nikaubeba begani na kutoka katika chumba hicho nilichokuwa nishakilipia.kwa haraka ya mwendo wangu nikajikuta nikivuta pumzi ndefu Baada ya kufika mbele kabisa ya jengo la kanisa ambalo kwa muda huo kulikuwa na watu wachache ambao wengine walionekana wanatoka wengine wanaingia.Nikajisogeza taratibu na kuingia katika kanisa hilo kisha nikajichanganya na watu katika mkusanyiko mmoja ambao kulikuwa na muhubiri mmoja aliyekuwa anatoa neno la mungu ndani kabisa ukiingia getini.Nikiwa katika mkusanyiko huo wa watu ghafla Magari ghafla yakaanza kumiminika na kutoka watu wa heshima kutokana na suti zao walizokuwa wamevaa huki kila aliyekua anatoka Alikuwa ameambatana na mkewe.Maubiri yale ya kwetu yakasitishwa na muhubiri na kutuamuru tutoke nje ya kanisa ili tuendele sikusikiliza Amri hiyo kwa haraka haraka nikaanza kuelekea ndani ya kanisa huku nikipishana pishana na watu ambao walikuwa wanaamrishwa watoke.Nikafanikiwa kuingia ndani ya kanisa hilo na kukimbilia chooni ambapo wakati nikijiandaa kujificha nikashtulia na jamaa aliyekuwa amevaa miwani na suti.

"Mmmh wewe unafanya nini huku hebu toka haujui kwani nini kinataka kiendelee"
"Nimebanwa kidogo nataka niende nikajisaidie "
"Nakuambia hakuna kwenda hausikii" Hakika yule jamaa alinizuia kuingia chooni huku akiwa ananilazimisha niondoke pale.nilimuangalia kwa muda na kuangalia usalama kwamba je kuna mtu anaona lakini Sikuona mtu katika maeneo yale.Nikazuga kama nataka kuondoka lakini nikazunguka teke kali lililompata barabara na kumdosha chini na kumfanya agune kwa maumivu.akiwa katika hali ya kujizoa zoa ili aamke nikamtandika ngumi kali ya shingo na kumzimisha kisha nikamchukua nakumuingiza chooni na kumficha katika chumba kilichopo ndani ya choo hicho kilichokuwa hakitumiki.nilitoka nikiwa nimevaa suti za yule jamaa huku nikishindilia na miwani meusi iliyonikaa vizuri katika macho yangu usoni nilionyesha tabasamu hafifu baada ya kuona nina Asilimia kubwa kabisa kuzuia Harusi isifungwe.Nikaendelea kuzunguka zunguka upande huo ambao mara kwa mara watu waliokuwa wamefavaa nao suti kama yangu na miwani waliokuwa wananipigia saluti kila wanapopita ikiashiria kama ishara yao pindi wakutanapo.Nikiwa nazuga zuga kama Mfuasi wa robertson nikiwa Nalinda Maeneo hayo.Mtu alivaa suti kama mimi akaja mpaka pale nilipokuwa nazunguka zunguka na kunipigia saluti kisha akanishika bega langu la kulia.

"sikia taarifa zilizotufikia punde kwamba dereva steven amekufa yule aliyekuwa akiwaendesha ma agent wengine kwenda kuwamaliza Yule pablo na mzee yule aliyemuokoa Nahisi taarifa ulishapata awali pia na wale walioendaa nao Mpaka sasa wale ishirini wamekutwa nao wamekufa.Sasa hapa pameshazurugika na tunahisi kwamba hawa Majamaa wanaweza kuvuruga harusi ambayo imebaki nusu saa tu ifungwe sasa kwani wewe daraja ngapi dah..aa kumbe c nimeona kwenye mfuko wako sasa basi Macho yako yawe makini sana kwa nguvu mmoja tuhakikishe boss wetu anafunga ndoa.." hakika wayasemayo wahenga usilo lijua ni sawasawa na usiku wa giza ndio hali iliyotokea baada ya jamaa yule kudhania kuwa mimi mfuasi mwenzake na kuniambia vitu ambavyo nilivisababisha mimi mwenyewe Huku mimi nikiwa ndio adui wao mkubwa.ilinibidi nimuitikie kwa katikisa kichwa na kumuacha jamaa huyu akiondoka huku akigeuka geuka nyuma na kuangalia mfuko wangu mkuukuu ambao ulikuwa mchafu lakini akajikuta akipotezea na kuniacha mimi palepale.hakika nilijikuta kwa muda mchache nikiingia katika dimbwi kubwa la mawazo yaliosababishwa na mauwaji niliyoyafanya kwa muda mfupi.hakika moyo wangu uliniuma sana kufanya vile lakini nilikuwa sina jinsi ya kufanya vile ilinibidi niuwe ili nimalize vizingiti vyote vilivyokuwepo.Nikiwa katika mawazo nikajikuta nikishtusha na matarumbeta flani yaliambatana na Nyimbo ya dini ambayo ulinioamasishwa nitoke pale chooni na kujiongeza mpaka katika kanisa lenyewe.Moyo wangu ukadunda ghafla mapigo ya moyo ambayo yalisababishwa baada ya kumuona moureen akiwa anatembea kuelekea kwa robertson aliyekuwa tayari ameshapanda kwenye kajukwaa cha kufungia ndoa.Hakika moureen uzuri wake ulizidi maradufu na alikuwa akitembea akisindikizwa nyuma na wapambe wake waliokuwa wamemsaidia kushikilia shela lake alilovaa lililokuwa likiburuzika.macho yangu yakaanza kuangaza na kuwaangalia miongoni mwa wafuasi ambao wote walikuwa wanamuangalia bibi harusi moureen wakati huo kama kawaida nikatoa upinde wangu na kuchukua mishale kama miwili na kuanza kuiandaa huku nikiificha kwa kuelekezea chini.Niliukabali msemo subira ya vuta kheri sikutaka nianzishe timbwili kwa muda huo nilisubiri kwanza misa kuu kabisa ya ndoa iishe ndio nianze kazi yangu iliyonipeleka pale...

TAZAMA KICHEKESHO HIKI KISHA BONYEZA SUBSCRIBE ILIYOPO CHINI YAKE WAKATI TUKIELEKEA KWENYE MUENDELEZO



USIKOSE SEHEMU YA KUMI NA MBILI

Maoni, Ushauri na Chochote Share Namimi Katika Mawasiliano Haya:
+255 718 274 413 Ipo WhatsApp
+255 764 339 438
ZephilineEzekiel@Gmail.Com

Chapisha Maoni

0Maoni
Chapisha Maoni (0)