LISEME JINA LANGU (12)

Zephiline F Ezekiel
LISEME JINA LANGU (12)
JINA: LISEME JINA LANGU Mwandishi: Pablo SEHEMU YA KUMI NA MBILI ILIPOISHIA... Niliukabali msemo subira ya vuta kheri sikutaka nianzishe timbwili kwa muda huo nilisubiri kwanza misa kuu kabisa ya ndoa iishe ndio nianze kazi yangu iliyonipeleka pale... SASA ENDELEA... Macho na masikio ya watu wote waliokuwepo ndani ya kanisa hilo yalikuwa katika mchungaji alikuwa anafungisha ndoa hiyo huku akiambatana na Moureen na robertson mugalula waliokuwepo pembezoni kabisa mwa mchungaji kasolo mimi niliyekuwa nimeshashika mishale yangu miwili katika upinde kwa lengo la kuifyatua yote muda utapofika.Misa fupi ya mchungaji ilionyesha kuwakuna kabisa wasikilizaji ambao walikuwa makini kabisa kumsikiliza.Wakati huo shingo yangu ilikuwa ikicheza pande zote za kanisa huku nikiangalia ni nani na nani aliyekuwa ananiangalia na kukuta Hata wafuasi wote wa baba moureen na robertson Mugalula walikuwa Wameshakamatwa na Misa ya Mchungaji aliyekuwa Na maneno matamu yaliomkuna kila mtu.Baada ya kumaliza misa mchungaj…