LISEME JINA LANGU (12)

Zephiline F Ezekiel
0
Mwandishi: Pablo

SEHEMU YA KUMI NA MBILI
Niliukabali msemo subira ya vuta kheri sikutaka nianzishe timbwili kwa muda huo nilisubiri kwanza misa kuu kabisa ya ndoa iishe ndio nianze kazi yangu iliyonipeleka pale...

SASA ENDELEA...
Macho na masikio ya watu wote waliokuwepo ndani ya kanisa hilo yalikuwa katika mchungaji alikuwa anafungisha ndoa hiyo huku akiambatana na Moureen na robertson mugalula waliokuwepo pembezoni kabisa mwa mchungaji kasolo mimi niliyekuwa nimeshashika mishale yangu miwili katika upinde kwa lengo la kuifyatua yote muda utapofika.Misa fupi ya mchungaji ilionyesha kuwakuna kabisa wasikilizaji ambao walikuwa makini kabisa kumsikiliza.Wakati huo shingo yangu ilikuwa ikicheza pande zote za kanisa huku nikiangalia ni nani na nani aliyekuwa ananiangalia na kukuta Hata wafuasi wote wa baba moureen na robertson Mugalula walikuwa Wameshakamatwa na Misa ya Mchungaji aliyekuwa Na maneno matamu yaliomkuna kila mtu.Baada ya kumaliza misa mchungaji aliwaambia moureen na robertson waangaliane huku na wapambe wa robertson na wa moureen wakiwa wanakazi ya kuwafuta futa majasho licha ya kuwa hawakuwa na majasho yoyote.

"Haya bwana robertson Mugalula shika hii Pete ya Ndoa Nitakachokisema ndicho utakachokifatisha kisha baada ya kumaliza utauchukua mkono wa kushoto wa bibie moureen na kumvalisha pete hii ninayokupa sasa hivi ya ndoa."
"Sawa mchungaji" yale maneno ya mchungaji yalinisababisha nikae tayari kabisa huku taratibu nikiaanza kupandisha taratibu upinde wangu wa mshale uliokuwa na mishale miwili juu Baada ya kuficha chini Huku nikiwa tayari kabisa nishajiandaa.
"Mimi robert Mugalula"
"Mimi robert Mugalula"
"Nafunga ndoa Mbele ya ushahidi wa kanisa na pete hii ya ndoa kwa kumuoa bibie moureen"
"Nafunga ndoa Mbele ya ushahidi wa kanisa na pete hii ya ndoa kwa kumuoa bibie moureen"
"Na kuwa mke wangu halali kabisa na kufunga naye pingu za maisha Mpaka kifo kitakapotutenganisha"
"Na kuwa mke wangu halali kabisa na kufunga naye pingu za maisha mpaka kifo kitakopotutenganisha" Baada ya robert mugalula kumaliza kuongea Akaipokea pete kutoka kwa mchungaji na kuchukua mkono wa kushoto wa moureen aliyekuwa analia wakati huo na kumnyoosha vidole ambavyo kwa mara ya kwanza alikuwa kavikunja kwa lengo la kumvalisha pete hiyo.Hapo ndio sehemu niliyekuwa naitaka mimi kuanzisha timbili.kabla hata robert mugalula ajamvalisha moureen pete ile anataka kumvalisha tu Nikafyatua mishale miwili ile haraka sana na mmoja kumpata robert mkononi iliyomfanya aidondoshe pete aliyoshika na kumuachia moureen kisha mwingine ukatua katika Paja lake la kulia hali iliyomfanya aruke kidogo na kudondoka chini huku akishikiria sehemu ile ya mguu niliyompiga huku akionekana kusahau kuugulia maumivu mengine ya mshale wa mkono uliomtoboa na kufanya mshale ubaki katika kiganja.Hali ya mshangaoo wenye kustaajabisha ndio ukachukua nafasi yake huku kelele za watu walizokuwanatoa kwa uoga huku wengine wakiwa katika harakati za kutaka kukimbia ndizo zilizoniwezesha mimi kwa kasi kufika katika jukwaa lile walilokuwepo Moureen na robertson.wakati ule moureen alibaki akishangaa tu naye pia alionyeshwa kushangazwa na tukio lile lililomfanya miguu yake ife ganzi.hata baba moureen na mama moureen nao walikuwa katika pia harakati za kutaka kukimbia.Baada ya kukanyaga katika jukwaa nikakutana na mabest man wa robertson waliokuwa wanajaribu kumpa msaada wa kwanza kwa kutaka kumchomoa mishale niliyomchoma.sikutaka kuwauliza bila ya kuchelewa nikajiachia Mateke Makali mawili yaliowapata wote wawili na kufanya kila mmoja aruke sehemu yake.nilisogea kwa haraka haraka na kukutana na mchungaji aliyekuwa ananiangalia kwa butwaa Nikamsogelea na kumtandika kichwa kikali cha kifua kilichomfanya atoe ukelele huku akimtaja yesu huku akidondoka kisha bila ya kupoteza muda nikamkunja roba Moureen na kumuekea bastola kichwani niliyoikuta katika suruali ya yule mfuasi ambaye niliyemuua chooni.Moureen hakusita kupiga kelele za kuomba msaada jambo lililozidi kufanya miongoni mwa watu wazidi kukimbia.Mapolisi wakiambatana na wafuasi wa robertson na baba moureen wakaanza kumiminika kwa wingi ndani ya kanisa hilo na kuanza kunisogelea mimi niliyekuwa nikitabasamu wakati huo huku nikizidi kuwaangalia kwa dharau.baba moureen alibaki akiwa anashangaa na kutojua cha kuwaamrisha wafuasi wake nini la kufanya kutokana na mimi kumshikiria Mrembo huyo na mkono wangu ulioshika bastola ulikuwa kichwani kwa moureen.Pembezoni mwangu kulikuwa na robertson mugalula ambaye Naye sumu ya mshale niliyompiga iliendeleaa kumtafuta na kubaki akiwa anagugumia kwa maumivu na kushindwa kabisa kutembea.

"Wote wekeni silaha zote chini la sivyo mali ya kichwa cha huyu binti nitakipasua sasa hivi Nahesabu mpaka tano moja!!!,Mbili!!!,Tatu!!!,Nneeeeee!!!!,Ta......"
"Jamaani wekeni silaha chini" Nikiwa nakaribia kumaliza hesabu niliyowaambia baba Moureen akawaamuru wafuasi wake na mapolisi waweke silaha chini ambapo bila ya shuruti wote wakaachia na kuzidondosha silaha zao chini.Ile nafasi ya mapolisi wale na wafuasi wale kuachia zile silaha ziliziniwezesha mimi kutoka na moureen pale jukwaani nakuanza kutembea naye haraka haraka nikitoka naye nje huku bado bastola yangu nikielekezea kichwani kwake.kwa bahati nzuri nikafanikiwa kutoka naye nje moureen huku nikisindikizwa na mapolisi na wafuasi wa robertson na wa baba moureen akiambatana na yeye mwenyewe baba moureen aliyekuwa pia na mkewe huku wakiendelea kunisisitiza nisimuue.safari yangu ya kumkokota moureen iligota katika gari jeusi ambalo lililokuwa kabisa la wafuasi wa robertson kisha nikalifungua haraka na kumuingiza Moureen na kisha mimi pia nikaingia na kwa bahati nzuri nikakuta funguo ya gari ikiwa kabisa imeshachomekwa mahala pake sikutaka kufanya ajizi kwa haraka nikakwinya funguo na kuliwasha gari kisha kwa speed ya ajabu nikaling'oa pale na kilichozidi kunisaidia ni uwepo wa geti kuwa wazi ndio ulioniwezesha nipite kwa haraka.wakatu huo huo nikiwa katika harakati hizo mapolisi na wale wafuasi baada ya kushuhudia nikianza kuendesha gari Wao waliishia kulishambulia lile gari kwa risasi kibao ambazo kwa uwezo lile gari lililokuwa hali ruhusu risasi yoyote kupenya.Speed yangu ya gari ilimshangaza kabisa moureen aliyekuwa ananiangalia sana huku machozi meusi yaliokuwa yamechanganyika na wanja aliopaka zilinifanya nijisikie vibaya.sikutaka kuanza naye kuongea kwanza kwa sababu nilikuwa ndani ya speed kubwa ya kuendesha gari kwa lengo la kuwachenga wafuasi wa robertson wakisaidia na nguvu tosha kabisa ya mapolisi waliokuwa nao wanakimbiza gari yangu na kilichozidi kunisaidia ni uwepo wa kutokuwa na Magari siku hiyo katika maeneo ya barabara zenye magari mengi na kutokuwa na matraffic.

"Moureeeen"
"Aa...b..eee"
"Sasa sikia Nielekeze Nyumbani kwenu haraka iwezekanavyo"
"Ni...mas..aki kata kushoto hapo ili tufike haraka" Hakika mipango yangu ilikuwa ipo kichwani kabisa na kwa kupita njia njia za shortcut zilifanikisha kabisa kupita bila ya wasi wasi.Bado moureen aliendelea kunishangaa na kuniuliza kwanini tunaelekea kwao lakini sikutaka kumjibu swali hilo kutokana na Mipango yangu ilikuwa inabadilika badilika kila wakati nipatapo wazo.katika kama majira ya saa sita hivi mchana saa iliyokuwa ndani ya gari ilitosha kabisa kunijulisha katika maswala ya wakati mkononi sikuwa na mshale wowote nilikuwa nimebaki na silaha tu huku nikiwa na moureen niliyejifanya kama nimemteka.Macho yangu yakatua katika lango kubwa la geti lililolembwa na vipande kama vya dhahabu dhahabu ambalo lilifanya geti hilo lipendeze Nikakanyaga breki baada ya Moureen kuniambia pale ndio palikuwa ni kwao kisha nikaanza kuendesha taratibu kuelekea katika geti hilo na kabla hata sijajiandaa kupiga honi lango lenye Automatic likajifungua na mimi nikaliingiza gari hilo.Ubaya wa gari hilo lilikuwa ni ni kioo cha nyuma tu ndio kulichokuwa kikionyesha lakini vilivyobaki vilikuwa ni tinted jambo lilinifanya niwe makini wakati wa kushuka kutokana na kuhisi nitapatwa na vizingiti kutokana na ulinzi niliohisi.Nikaanza kumtanguliza mouree aliyetoka kwa haraka na kisha kufuatia mimi lakini kabla hata sijajiandaa kutoka kabisa Ngumi nzito iliyonipata sawa sawa iliyonirudisha nyuma ikarushwa na kufanya niteme chembe chembe za damu hali ilinitia hasira kali iliyonifanya na mimi nitoke kwa style ya kurusha mateke yote mawili yaliompata yule aliyenipiga ngumi kifuani huku na mimi nikitoka kabisa nje ya gari hilo na kumfanya yule jamaa adondoke chini.wakati natoka nikakaribishwa vyema na walinzi kumi ambao kwa bahati nzuri kwa pale hawakuwa na silaha zaidi ya mikono yao iliyokuwa ishakunja ngumi tayari kabisa kupambana na mimi kutokana na wengine waliokuwa nyuma kuanza kunikimbilia.Hapo ndipo mafunzo yalioniingia kutoka kwa babu marehemu gardner ndio yalianza kutumika zoezi la kunifundisha kupambana na watu wengi ndio yalinipa hali ya kujiamini na kuanza kwenda nao sambamba.kazi hakuwa rahisi kwa sababu nao walikuwa na ujuzi kidogo ambao hakunitisha mimi ambaye niliendelea Kuwatandika mapigo makali yaliomnyong'onyesha kila aliyenisogelea na kufanikiwa kuwazimisha kama saba.huku watatu waliobaki niliishia kuwamiminia risasi za miguu kila mmoja na kufanya waanze kutoa makelele ya kuomba msaada.Baada ya kumaliza kupambana nao nikamshika moureen mkono moureen ambaye alizidi kunishangaa na kubaki akiniangalia tu na kutojua la kuniambia kutoka na kuwa na nguvu na kujiamini vya kutosha kuliko alivyonizoea.wote tukaingia ndani ya jumba hilo kubwa la kifahari ambalo lilikuwa na wafanyakazi wakike sita wa kazi za ndani.sikuwa na muda wa kuangalia angalia thamani ya vitu vya ndani na nilipofika katika sebure kubwa nikajibwaga katika kochi kubwa huku mbele yangu kukiwa na bonge la tv la flatscreen lilojaa katika ukuta wote pale.Moureen alikaa pembeni yangu akiniangalia na kutaka kuanza mazungumzo lakini alijikuta akishindwa kutokana na jicho kali nililokuwa namuangalia.

"Kwa hiyo ulikuwa unakubali kuolewa na Mwanaume usiyempenda???"
"Pablo nilikuwa sina jinsi ya kufanya hivyo ilinibidi nikubali tu"
"Ouk hivi unanipenda kweli??"
"Yes mpenzi nakupenda sana"
"Ni kweli unataka kuishi na Mimi tukiwa Mume na mke"
"Kwanini isiwe hivyo pablo Nahitaji iwe hivyo katika maisha yangu sitaki mwanaume mwingine zaidi yako pablo"
"Ouk Najua wewe ndio mtoto pekee katika familia yako nataka tucheze mchezo leoleo sasa hivi Naomba niletee hati za nyumba hii kadi zote za Benki na karatasi zake zote."
"mmmh sawa..basi nifuate huku" Nikajikuta nikipata kama mshtuko wa moyo kudunda baada moureen kukubali mpango wangu kwa kutumia ishara ya kidole akaniamrisha nimfuate jambo ambalo sikulemba nikajizoazoa kwenye kochi na kuanza kumfuata kwa haraka haraka huku naye nikimshawishi atembee haraka haraka ili tufanye vitu kwa ushapu.Moja kwa moja tukaingia katika chumba kikubwa kilichokuwa na choo chumba ambacho Baada ya kuingia nikajikuta nizungusha zungusha kichwa changu na kuanza kuangalia thamani ya vitu vingi vilivyokuwepo humo.Nikamuona moureen akisogea mpaka kwenye dressing table kubwa iliyokuwa ina vikoro koro vingi kama maperfume, mafuta na marosheni ya kila aina kisha nikamuona akifungua kamlango cha kabati la dressing table hiyo na kutoa funguo kisha alipomaliza.Moja kwa moja akaenda katika kabati kubwa la nguo lilokuwepo humohumo na kufungua kisha akakuta sanduku na kulifungua na kukuta kisanduku kingine kilichomfanya hata yeye ashangae kidogo kisha akanyanyuka pale na kuanza kama kufikiria kitu kama dakika moja hivi na kuniomba nimsaidie kuinua godoro la kitanda kilichokuwepo humo na mimi bila ya kusita nikaenda kunyanyua godoro hilo kwa kupapasa moureen akakuta funguo nyingine ambayo alienda kufungua kisanduku kingine kilichobaki na kukuta madocument ya makaratasi ya benki zikiambatana na Atm kama nne za bank zilizokuwa na kikaratasi cha namba za siri za bank zilizoandikwa katika moja ya karatasi kisha na hati miliki kabisa ya Nyumba hiyo.baada ya kutoa akarudishia vile vile kisha akanikabidhi vile vitu na mimi nikavipokea kisha akanisogelea karibu kabisa nakuanza kunipa mdomo wake kwa lengo la kunipa denda na mimi nikaupokea kwa ufundi wa hali ya juu

TAZAMA KICHEKESHO HIKI KISHA BONYEZA SUBSCRIBE ILIYOPO CHINI YAKE WAKATI TUKIELEKEA KWENYE MUENDELEZO



USIKOSE SEHEMU YA KUMI NA TATU

Maoni, Ushauri na Chochote Share Namimi Katika Mawasiliano Haya:
+255 718 274 413 Ipo WhatsApp
+255 764 339 438
ZephilineEzekiel@Gmail.Com

Chapisha Maoni

0Maoni
Chapisha Maoni (0)