
SEHEMU YA KUMI NA TATU
Baada ya kutoa akarudishia vile vile kisha akanikabidhi vile vitu na mimi nikavipokea kisha akanisogelea karibu kabisa nakuanza kunipa mdomo wake kwa lengo la kunipa denda na mimi nikaupokea kwa ufundi wa hali ya juuSASA ENDELEA...
"Moureen!!,moureen,Si muda wake sasa subiria kama nitaweza kutoka salama"
"But..ba..by nimekumiss mpenzi ni kitambo sana ujue"
"No..sio muda wake" Nilimuambia moureen huku nikimtoa katika kifua changu alichokuwa ameegea baada ya denda la kama nusu dakika kisha nikamshika mkono na kutoka naye nje ambapo moja kwa moja tukarudi sebureni.Baada ya kufika sebereni Nikachukua dude la kuvutia sigara linaloitwa shisha na kukaa nalo karibu na kuanza kuwasha moto na kuanza kuvuta shisha hilo huku mikononi mwangu kukiwa na makaratasi yote.Nilimwambia moureen asogee karibu yangu kabisa kisha nikaitoa bastola yangu mfukoni na kumkombatia moureen kwa ule mkono uliokuwa na bunduki niliyomuelekezea kichwani na kumfanya moureen aanze kutetemeka kwa uoga huku akiniangalia kwa huruma
"So Pablo hivi ni kweli utaniua"
"Hapana sitakuua ila..."
"ila nini?? na mbona bado umekaa hapa hauoni kwamba ni hatari ambapo baba atakuja na watu wake na Mpango wako ni upi"
"Hey moureen hebu tulia kwanza usiwe na pupa subiri uone haka kamche........" Nikajikuta nashindwa kumalizia baada ya kusikia ving'ora vya magari ya polisi vilivyokuwa vikilia nje ya geti la jumba hilo vimilio vilivyopenya kabisa katika tundu zangu za masikio.Kwa madaha na utulivu nikatulia na kuvuta pumvi kwa nguvu na kumuweka moureen vizuri huku nikimuewekea bastola vizuri kichwani huku mkono mwingine nikishika makaratasi yale muhumi na kuishikilia shisa kwa wakati mmoja huku nikiendeleaa kuvuta.Haikupita hata dakika tano mlango wa pale sebureni ukafunguliwa kwa nguvu kwa kupigwa mateke na kuingia wafuasi wa baba moureen na wafuasi robert wakiambatana na mapolisi wasiokuwa na idadi ambao mikono yao ilikuwa imeshiba bunduki kali wakiongozana na baba moureen aliyekuwa na mkewe wakiwa wanahema juu juu
"Kabla hataujafanya chochote weka silaha chini na usimame juu huku ukimuachia binti kabla sheria haijachukua Mkondo wake" Moja kati ya polisi aliyekuwa mstari wa mbele huku akinionyeshea mimi bunduki aliongea na kunifanya mimi nitabasamu huku nikiendelea kutoa moshi mzito wa ile shisha Niliyokuwa Naivuta.
"Hahaha sheriaaa???,sheria gani unayozungumza wewe.Mpaka hapa Nilipo nipo tayari kwa lolote na kama mtanikamata sasa hivi basi kichwa cha huyu binti nitakipasua kwa bastola hii iliyokuwa na risasi nyingi tu."
"Hivi wewe Mbwa unataka nini??,Muachie Mwanangu kabla sijawaamrisha vibaraka wangu waanzishe vita."
"Hahaha baba moureen bado unaongea ukiwa ujui unachoongea" Nilimwambia baba moureen aliyekuwa amefura hasira kwa kuniangalia kwa jicho baya huku nikimuonyesha madocument yake ya Akiba zake za pesa huku nikimuonyesha na kadi zake za atm na kumuonyesha pia Hati miliki ya nyumba yake zilivyomfanya apate mshtuko mkubwa yeye na mke na kujikuta wote wakitumbua macho kwa mshangoo kutokana na kutoamini kabisa wanachokiona.
"Sasa basi kama unataka makaratasi haya yarudi mikononi mwako waambie wafuasi wako Pamoja na hao mapolisi watupishe kidogo watuachie tuyamaliza mimi na wewe sasa hivi" Nilimwambia baba moureen aliyekuwa kama kaduwaa na kufanya aanze kukuna kichwa na kutafakari kisha akaniangalia mimi ambaye kwa wakati huo Nilikuwa namtishia kuingiza makaratasi yale katika lile dude la kuvutia shisha ambalo lilikuwa linamoto mkali kidogo.
"Sasa vijana chukueni cheki hii ya millioni tano na mkagawane muondoke haraka nilimalizane naye na nyie vibaraka wangu nisubirieni Nje" Baba moureen kwa kujikaza akaandika cheki ya kuchukua hela na kumkabidhi yule polisi aliyekuwa akiwaongoza wenzake ambao baada ya kuambia hivyo hawakuwa na hiyana wote pamoja na wafuasi wale wakatoka na kuniacha Mimi nikibakia Na baba moureen,mke wake na moureen mwenyewe ambao wao wote hawakuwa na neno lolote la kuongea.Baada ya kuhakikisha kwa macho kuwa wote wametoka Nikajikokota kwa kuinuka kisha nikaanza kupiga hatua za taratibu na kumfuata baba moureen aliyekuwa naye ananiangalia na kumfuta kwangu kulionyesha kumpa wasiwasi kutokana alikuwa ananiangalia kiuoga
mkono wangu ulikuwa umeshika document za mali zake zote.
"Kumbuka kuwa kila mtenda baya lazima hulipwa na baya lake alilofanya kutoka na ubaya aliomfanyia mwenzake,mzee umeua familia yangu kwa kuwanyonga mbele yangu jambo ambalo linaniuma mpaka sasa,na ninavyokuona mzee baba yake halali kabisa moureen kifo kinakukalibia na nitakuua mimi mwenyewe ila kama unatafata ninachokitaka basi nitakuachia.Sasa basi umeona haya makaratasi yako nataka uandike Jina langu kama mrithi wa mali hizi"
"Whaaaaaaat haiweze..k....." kabla hata baba moureen hajamaliza kuongea nikamsogelea na kumtandika kofi nzito la uso na kumfanya ayumbe yumbe na kabla hata hajakaa sawa nikamtandika kichwa kizito cha kichwa na kufanya atoke nundu papo hapo na kusababisha moureen na mama yake waanze kupiga makelele ambayo niliyanyamazisha kwa kuwakanya kuwa kama watapiga kelele basi sitakuwa na huruma na Mzee huyo.
"Sikia mzee sina muda wa kupoteza safari hii nakuua vp utaandika jina langu au hauandiki"
"fuck you niuee tu siandiki" jibu la baba moureen likanitia hasira na kujikuta nikimuweka sawa na kuvuta ngumi niliyoikunja kwa nguvu nikiwa na lengo la kumtandika katika mdomo wake.lakini nikiwa katika hali ya kupeleka ngumi ghafla kitu kama mshale ukapenya kwa haraka katika bega yangu ya kulia na kufanya nimuachia baba moureen niliyemkunja na kuanza kumuangalia aliyenipiga lakini kabla hata sijainua kichwa changu kumuangalia nani aliyenipiga nikazolewa kwa kupigwa kikumbo kikali mpaka katika kochi kisha zikafuatiwa na ngumi tano za nguvu zilizotuwa kifuani kwangu na kunifanya nitapike damu nzito na kunifanya nipate juhudi za kumsukumiza aliyekuwa ananishambulia jambo ambalo nilifanikiwa kumtoa.Macho yangu yakatua kwa robertson mugalula ambaye kwa Asubuhi yake nilikuwa nimempiga mishale miwili ambayo kwa hali niliyomuacha katika kanisa nilijua kabisa kwa namna moja ama nyingine sumu ya mshale ingekuwa ni silaha tosha ya kumfanya atungulie haraka mbele za haki.akiwa anachechemea mguu mmoja huku majasho mengi yaliokuwa yanamtiririka kwa kasi na kuzidi kulowesha shati akajikokota na kuchukua lile dude la shisha na kulinyanyua na kunielekezea mimi kwa lengo la kunitwanga nalo na kunifanya nibaki nimemtumbila macho huku Nikiwa najaribu kuinuka lakini maumivu ya mshale wa bega ulitosha kabisa kuniua nguvu na kubaki nikimuangalia tu Robertson aliyekuwa yupo tayari kabisa kunirushia dude lile.............................
TAZAMA KICHEKESHO HIKI KISHA BONYEZA SUBSCRIBE ILIYOPO CHINI YAKE WAKATI TUKIELEKEA KWENYE MUENDELEZO

USIKOSE SEHEMU YA KUMI NA NNE
Maoni, Ushauri na Chochote Share Namimi Katika Mawasiliano Haya:
+255 718 274 413 Ipo WhatsApp
+255 764 339 438
ZephilineEzekiel@Gmail.Com
Maoni, Ushauri na Chochote Share Namimi Katika Mawasiliano Haya:
+255 718 274 413 Ipo WhatsApp
+255 764 339 438
ZephilineEzekiel@Gmail.Com