LISEME JINA LANGU (2)

Zephiline F Ezekiel
0
Mwandishi: Pablo

SEHEMU YA PILI
Tulikuta hali ilikuwa mbaya sana kwa halima ambaye kwa wakati huo alikuwa chini huku jackline kamkalia juu na kushika glassi kwa lengo la kumbamiza nayo kichwani.john haraka akamdaka jackline na kumpokonya glassi na kumshika huku na mimi nikimshika halima ambaye baada ya kushikwa jackline yeye alisimama kwa lengo la kumvamia ili amrudishie.

SASA ENDELEA...
"Malaya wewe ningekuua kudandia mabwana za watu.."
"Halooo utajiju ndio nishamkamata bwana wako sasa pyeee..utajiju"
"ndio hivyo kantangaze na wewe niachie nikammalize malaya niachie na kwambia niachie..aaaa niachie.."Ilikuwa sauti ya jackline aliyesikiliwa na john kwa nguvu na kutaka kujaribu kutoka.Kama kawaida ya wasichana waliendelea kurushiana Maneno ya nguoni yaliosababisha umati wa watu kujaa huku wambeya ndio wakizidi kuita wenzao waje kushuhudia tibwili hilo la Maneno ambalo bado lilikuwa likiendelea.Hakika katika Maisha yangu sikuwahi kumuona jackline akiwa katika hali ile hasira zake zilikuwa hazishukiki kirahisi zilivyomfanya awe na nguvu ajabu.alifanikiwa kumporochoka john katika mikono yake na kumvaa tena halima aliyekuwa nimemshikilia mimi na kuanza kupigana tena na kusababisha miongoni mwa wasichana wambeya kushangiliaa kwa nguvu na huku miongoni mwa watu wengine wakiendelea kugombanizia ili hali itulie.

"Aisee kumbe Na huyu pablo Malaya eee kagonganisha haloooo" hakika ilikuwa siku ambayo nikiikumbuka huaga na cheka kwa masikitiko kuna watu walikuwa wananisema wengine wakinitetea kwa hali iliyotokea.Ugomvi uliisha baada ya Mapolisi kuwatawanyisha watu na kuwakamata Halima na jackline.Mimi na john tulirudi ndani na john akaanza kunisaidia kuweka vitu sawa huku na mimi kifuta futa damu na kufagia baadhi ya vyupa vya glassi na Bakuli vilivyofunjika.
"Mmh mbaba kumbe na wewe noma hadi umesababisha Mademu wapigane pablo'
"Daaah acha tu jamaa"
"ila kawaida Ndio uwanaume kama ukiwashughulikia vizuri lazima wakugombanie daa ila wewe mbaya.."
"Hahaha hamna kawaida...ka...." kabla hata sijamaliza sentensi Mlango wangu ukagongwa nikaenda kufungua na kuwaona Maaskari waliovaa sare zao wawili wakiwa katika wamesimama
"haloo sisi ni maaskari katika kituo cha kati unahitajika mara moja kituoni kwa maelezo" siku na hiyana mdogo mdogo Nikanyanyuka na kwenda Mpaka kituoni.Nilikuta Baadhi ya watu mtaani ambao Nao walieenda wakiwa wanawasubiria halima na jackline watoke.sikukaa sana kituoni waliniuliza Maswali kidogo na kuniruhusu nirudi nyumbani na kuwaacha Halima na jackline wakiwa bado wapo lupango.nilifika nyumbani na kumkuta bado john yupo huku akimaliza kila kitu nilimshukuru sana na haikupita hata dakika aliniaga Nakuondoka.Nilipanda zangu kitandani na kulala huku Msongamano wa Mawazo ukichukua nafasi yake iliyosababisha usingizi Mzito kuchukua Nafasi yake.Nilishtusha na Mlio wa simu yangu iliyoonekana ikiita sana.niliichukua na kuaangalia jina na kuiona Namba tu bila ya jina niliangalia saa kwanza ilionionyesha ilikuwa ni saa mbili usiku katika simu yangu kisha nikaipokea

"Halooo"
"Haloo wewe si ndio Pablo"
"yaah ndio Mimi"
"Basi mimi dada yake jackline na kutaarifu ya kwamba Jackline yupo hospitalini mwananyamala na hali yake mbaya kwa sababu alikunywa sumu.."
"Mungu wangu" nilijikuta nikisema kwa nguvu na kisha simu hiyo ikakatika nilianza kujiandaa kwa lengo la kwenda hospitalini lakini kabla hata sijatoka simu yangu iliita tena lakini Nilipoiangalia tena niliona ni namba ngeni ambayo haikuwa na jina kwa haraka haraka nikajikuta nikiipokea.
"Haloo"
"Nambie"
"Natumaini wewe ndio pablo Nakutaarifu tu kwamba halima amekunywa sumu ya Panya hapo tulipo tushampa maziwa lakini hali yake Bado mbaya ndio tunampeleka MwananyaMAla Hospitali..."........

Hakika habari zile Mbili zilinichanganya kwa kiasi kikubwa Mno nikajikuta Mwanaume nikikurupuka Ndani huku tumbo wazi shati nimeliweka begani na kuchukua Ndala zangu huku safari ya mwananyama kuanza.Kutokana na kutokuwa na umbali kutoka nyumbani Mpaka hospitali nilifika kwa haraka huku nikiwa nashauku kubwa.Nilijikuta nikishusha pumzi ndefu baada ya kufika sehemu iliyoandikwa reception(Mapokezi) Ambapo nilikuta umati mwingi wa watu ambao walikuwa wanasubiri huku watu hao wakigawanyika kwa Makundi mawili.kwa tathimini tu nilizoanza kupiga niliweza kutambua kwamba Makundi yale Mawili ya watu moja lilikuwa la upande wa jackline lingine lilikuwa la Halima.Mdogo Mdogo nikaanza kulisogelea kundi la watu waliokusanyika ambalo kwa kuangalia niligundua ni la mama halima Ambalo Mama huyo wakati huo Machozi yalichukua nafasi yake.Nikasogea mpaka pale huku nikipigipa hatua chache lakini kabla hata sijamfikia kuna mtu ghafla akaropoka.

"Mama halima pablo mwenyewe si huyu hapa!!".Maneno yale yalionekana yalimshtusha sana mama huyo na kuacha kuliwa kisha akageuka nyuma na kuniangalia huku akiwa amefura kwa hasira ambazo wakati akiwa ananiangalia mimi alianza kuhema juujuu hali ambayo hata mimi taa ya hatari ikaanza kuniingia kichwani kwangu.
"we Malaya mwanahizaya kwa nini unataka kuniulia Mwanangu haujui kwamba ndio mziwanda wangu huyu."
"Unajua ni mama sikili...za yani...hi..vi.......Paaaaaaaaaaaa"Kabla hata sijamaliza kuongea nilishtukia kibao kikali kilichopigwa kwa ufundi na Mama halima kutua kabisa katika shavu langu ambalo nilisi nyota fulani ambazo nilijikuta nikawaona mama halima wawili wawili kutokana na Kibao hicho kilichonifanya nishike shavu langu.nikiwa katika maumizi yale ghafla mama yule akanikunja na mikono yake hali iliyosababisha ukelele wa umbeya ukianza kusikika katika hospitali hiyo ya Mwananyamala huku fujo vilivyosababishwa na kelele kuchukua nafasi yake.
"Oyooo!!!!.....mpige malaya anajifanya kidume.oyooo piga!!!,piga!!!piga!!!"sauti za watu ndizo zilizidi kumpa bichwa mama halima ambaye alinikunja na kusababisha Aongeze Majonjo kwa nitingisha tingisha kisha Akachia kichwa kikali kilichonipata sawa sawa kichwani na kunifanya Tena nianze kuona nyota.

"Mama ee kausha bana...kausha nisamehe..bana usifanye hivyo usifanye hivyo Mama..."
"Lazima nikufundishe Adabu" kutokana na kelele zilizokuwa zinampa kichwa Mama yule Ambaye bado aliendelea kunikunja ghalfa akanianisha mgongo na kuanza kunitandika Makonde mazito Ambayo yaliniiingia sawa sawa.nilijikuta Nikiingiwa na Hasira na kupata nguvu ya kumchomoa mama huyo kisha nikampa ngumi moja iliyomtia hasira na kuanza kuendelea kunirusha vichwa.hakika mama halima sijui alikuwa mkuria maana shukrani ziende kwa walinzi waliofanikiwa kugombelezea ugomvi kwa kufanikiwa kumtaiti Mama huyo ambaye muda si mrefu daktari akasema hali ya mwanae halima na kumwambia hali ilikuwa shwari na kumfanya aondoke hospitalini hapo.Mimi sikuondoka bali nilienda katika kundi lingine ambalo lilikuwa na Mama jackline ambaye kwa macho tu nilishamgundua kwa sababu ya kufanana mno na Mtoto wake jackline lakini kabla hata sijafika
"Wee kijana ukomi tu kule umepigwa unataka na huku wewe Nenda achana na Mwanangu ondoka baba uliomfanyia tu yanamtosha.."Maneno yale ya mama jackline yalinumiza na kujikuta nikimpiga Magoti Huku machozi yakinilenga lakini haikusaidia kwa sababu bado aliniambia niondoke kwa sauti ya juu iliyonifanya nitii na kuondoka bila ya kujua hali ya Msichana huyo jackline anaendeleaje.nilifika nyumbani huku nikiwa na mawazo kibao.siku ziliendelea kusonga Hali ya Jackline iliendelea vizuri na kupona kabisa licha ya kuwa mara nyingi nilipoenda Kumuangalia nilipigwa stop.sikuwa na hamu ya kwenda kumuangalia halima kutokana na mtiti wa Mama halima.Siku Moja Nikiwa katika pilika pilika za kununua nguo kutokana na sikukuu ya Pasaka kukaribia nilimuona mrembo.Mrembo ambaye kwa Kumuangalia vizuri alikuwa ni jackline msichana ambaye kipindi kifupi tu kutokuwa naye kulinifanya nikonde kwa kumuwaza niwe mpweke kwa ajili yake.nilimfuata na kumgusa bega ambaye hata yeye baada ya kuniona Aliachia tabasamu

"Inakuaje jackline"
"pouwa"
"za masiku"
"Nzurii"
"Sasa jackline mbona umenichunia hivyo najua kwamba nilikukosea sana lakini mimi ni Binadamu kama binadamu wengine jackline ninakosea"
"Mmmh Mbona mimi nimeshakusamehe ilibaki mimi tu nikuombe msamaha kwa sababu nilikuja kuvuruga Mechi yenu kati ya wewe na malaya mwenzako"
"yaliopitwa si ndwele tugange yajayo nakuomba unisamehe turudiane jamani Jackline Please"
"Hahaha urudiane Na nani sasa"
"Aaaaaa na wewe jackline mpenzi"
"haloo kama ni jembe lishapata mlimaji, am sorry pablo tushachelewa jamvini karamu imeshaliwa" Alisema Maneno yale jackline huku akinionyesha kidole chake kilichokuwa na pete iliyoonekana kama ya uchumba hali ilinifanya nipigwe Na kama shoti ya umeme nilijukuta nikaangua kilio kama chizi huku nikipiga Magoti huku kwa Mbali Nilimshuhudia jackline akaiondoka pale kwa Madaha na Malingo na kuniacha pale nikilia huku miongoni mwa watu wakinicheka wengine wakinionea Huruma..........

Nilijikokota huku bado machozi yakichukua nafasi yake huku Nikiwaacha watu waliopo eneo hilo kusema kila wanachojisikia kuhusu tukio lililotokea kisha haraka haraka nikapanda gari la kuelekea nyumbani huku Bado nikiwa na simanzi ya hali ya juu.Nilifanikiwa kufika nyumbani mapema tu lakini kabla hata sijaingia ndani nilimsikia mtu kama ananiita na kunifanya nisimame Alikuwa ni john rafiki yangu ambaye kwa kiasi kikubwa alinisaidia kuwasuluhisha jackline na halima

"Kaka vp Pablo mbona umechoka choka"
"Hamna bana kawaida si unajua tena mihangaiko ya hapa na pale"
"Vp auendi kwenye harusi??"
"harusi ya nani"
"Si halima leo anaolewa kaka".Maneno ya John yalianza kuninyong'onyesha nikajikuta nikishika kichwa huku machozi yakinilengalenga nikajitutumua kumjibu huku nikijaribu kuficha hali ambayo ilinitokea ghafla kwa wakati huo
"Pouwa nisubiri basi nika...oge twende"
"Poua kaka"bila ya kupoteza muda nikaenda kuoga huku bado mawazo yakiendelea kutawala katika kichwa changu huku Nikijaribu kupoteza mawazo hayo kwa kuimba imba.nikamaliza kisha mimi na John tukaanza safari ya kwenda kwa Halima.Tulifika kwao na kukuta rusha roho la nguvu huku Baadhi watu wengine wakipiga vigelegele.Ghafla Gari kubwa likaja likiambatana na gari ndogo ambayo kwa kuangalia tu lilionekana lilikuwa la bwana harusi hali ilizidisha vegelele na kelele za furaha.bwana harusi akiwa ndani ya kanzu ndefu na kiremba alishuka kwenye gari ndogo kwa madaha huku akiwa na wapambe wake wakiwa wamfutamfuta majasho kamera nazo hazikuwa nyuma kumpiga picha hali iliozidi kuzidisha Harusi kunoga.bwana harusi akiingia ndani na hakupita hata nusu saa akatoka na bibi harusi ambaye kupendeza kwake kulimfanya hata asionekane halima niliyemzoa.uzalendo ukanishinda nikajikuta nikimtoroka john ambaye alikuwa kimya akiangalia mchezo mzima unavyoendelea.nilitembea kwa haraka haraka na kufika nyumbani kisha nikaingia ndani na kujitupa kitandani huku nikiwa na mawazo.hakipita dakika mlango wangu ukagongwa hali ilinishtua na kujikuta nikajizoazoa taratibu na kwenda kuufungua.

TAZAMA KICHEKESHO HIKI KISHA BONYEZA SUBSCRIBE ILIYOPO CHINI YAKE WAKATI TUKIELEKEA KWENYE MUENDELEZO



USIKOSE SEHEMU YA TATU

Maoni, Ushauri na Chochote Share Namimi Katika Mawasiliano Haya:
+255 718 274 413 Ipo WhatsApp
+255 764 339 438
ZephilineEzekiel@Gmail.Com

Chapisha Maoni

0Maoni
Chapisha Maoni (0)