
SEHEMU YA TATU
Nilitembea kwa haraka haraka na kufika nyumbani kisha nikaingia ndani na kujitupa kitandani huku nikiwa na mawazo.hakipita dakika mlango wangu ukagongwa hali ilinishtua na kujikuta nikajizoazoa taratibu na kwenda kuufungua.SASA ENDELEA...
"Vp anko mimi naitwa Alex nimetumwa na dada nije nikuletee mzigo wako."nilimuangalia kijana huyo aliyeonekana tunalingana kimakamo ambaye baada ya kusema hivyo alinipa bahasha ya kaki ambayo bila kusita nikaipokea kwa shauku kubwa
"Dada gani"
"Jackline".Baada ya kusikia jina la jackline nikajikuta furaha kubwa imeingia katika nafsi yangu nikamruhusu kijana yule ambaye bila kuchelewa akaondoka nikaingia ndani na kwa pupa nikaanza kuifungua bahasa hiyo na kukuta kadi ya mualiko kama wa sherehe fulani hizi na kukuta kikaratasi kilichoandikwa
"Baby nimekusamehe jamani nakupenda sana naomba usikose kuudhuria katika sherehe hiyo itakayoanza kanisani pale posta la Nathan church please wahi mpenzi kwa sababu nipo peke yangu nahitaji niwe nawe".Nilisoma barua hiyo ilionifanya nipate faraja kubwa katika Nafsi yangu hali ilionirudisha katika hali ya furaha.Mungu si Athumani jumapili ikafika lakini kuchelewa kwangu kuamka kulinifanya niingie na wasiwasi kidogo.nikavaa suti kali ambayo baada ya kujiangalia kwenye kioo nilijithibitishia kwamba nilitokelezea kisha nikatoka na kuchukua taxi ambayo nilikubali kutoa kiasi chochote ili nifike haraka.nilimpa dereva elfu hamsini ambapo bila ya kupoteza muda akaanza kulikimbiza taxi hiyo na kupitumia lisaa limoja tu kutoka mwananyamala komakoma mpaka posta ambapo ndipo kanisa lilipo.nilifika na kukuta umati wa watu wakizidi kuingia katika kanisa hilo ambalo hauingii bila ya kutoa kadi ambayo alinipatia jackline akimtuma Alex.nikaingia katika kanisa hilo na kukaa kwenye siti huku macho yangu yakimtamfuta jackline ambaye licha ya kumtafuta kwenye simu namba yake hakupatikana.nilibaki kwenye kiti nilichokaa na kumsikiliza padri aliyekuwa akiiendesha Misa huku bado nikiendelea kumtafuta jackline huku mawazo yakuchelewa kwake yalitawala katika fikra cha kichwa changu.Ghalfa Mtu alivaa suti kali nyeusi Akiambata na wapambe wake wakaingia hali iliyofanya watu wote kanisani kupiga vigelele vilivyozidi kunishangaza
"Mmh kwani vp??"nilijikuta nikijiuliza maswali kadha wa kadha huku nikiwa nipo katika kiza kinene kilichonifanya nitulie nikisubiri kitakachotokea.Kelele zingine za vigelele vilipita katika ngoma za masikio yangu kwa mara nyingine huku kwa macho yangu nikishuhudia mwanamke alivaa shela jeupe lililompendeza sana akitembea kwa hatua ndogo ndogo huku kashika mauwa akiambatana Na wapambe wanne wawili wakishika shela kwa nyuma lililokuwa likiburuzika huku wengine wakiwa wanamsindikiza kwa kutembea.nikajikuta nikisimama na kumuangalia bibi harusi huyo na Macho yangu yalimtambua kwa haraka sana hakuwa ni mwingine bali ni mrembo niliyotoka naye mbali alikuwa ni jackline.hali ya kuishiwa nguvu ilikuja mara moja na kujikuta nikaa katika kiti changu kama mgonjwa aliyepatwa na ebola.mboni ya macho yangu yalianza kubadilika huku hali ya majimaji yalitiririka kidogokidogo hali iliyonifanya nijifute ili kutoruhusu kuonekana.usingizi mzito ukanijia ghafla nikajikuta nikiegemea kwenye benchi la mwenzagu wa mbele aliyekuwa kasimama kwa kuweka kichwa changu.usingize ule hakuwa wa muda mrefu hakupita hata dakika kumi nikasikia maneno ya padri akimuuliza jackline ambaye alikuwa kafunikwa na kofia ya shela aliyovaa
"Bibie jackline umekubali kuolewa na bwana jackson Martin na kuwa mume wako wa ndoa kwa uthibitisho wa pete hii ya ndoa.."
"Ndiiio nimekubali"sauti nyororo iliyoambata na vigelegele ndivyo vilipenya kabisa katika masikio yangu huku macho yangu yakiona kabisa bwana harusi akimvisha pete ya ndoa ile mkononi mwa mwanamke niliyempenda sana jackline kisha bila hiyana wakaaanza kunyonyana denda mbele ya umati uliozidi kuongeza vigelele huku kila mtu ndani ya kanisa hilo akiwa na furaha sembuse mimi tu ambaye wakati huo Nilijitahidi kuzuia machozi yasinidondoke katika mashavu yangu.nilijikuta nikinyanyuka nakuwapita watu waliosimama huku wakipiga vigelele huku hakuna hata aliyejua maumivu yangu ya moyo ambayo katika maisha yangu nilisi kama nimepoteza kitu kikubwa.
"Wewe Fala utagongwa boya wewe chizi nini"ilikuwa sauti ya dereva wa gari aina ya costa ambaye kama isingekuwa breki baasi ningeshapelekwa Hospital baada ya kufungia breki karibia kabisa na mguu.hakika wakati huo nilikuwa sijielewi kabisa mawazo yalizidi kukuiandama kichwa changu hata nakumbuka siku hiyo usingizi haukuja kabisa kila nilipokuwa namkumbuka jackline nilikuwa nalia.hakika jackline ni msichana ambaye alinisaidia kwa vingi alijitahidi kujinyima yeye ili anipe mimi pale ninapopatwa na Matatizo alikuwa ni mwanamke mwenye kujitambua na alionyesha mapenzi ya dhati kabisa kwangu.Ndoto zangu za kumuoa ziliyayuka kabisa kwa umalaya ambao niliufanya bila hata ya msingi bali ni tamaa tu za kimwili.nilijikuta nawaza sana mwisho ilinibidi niukabali ukweli tu kwamba jackline nilimkosa.nakumbuka siku moja nilikutana naye Maeneo ya mwenge Aliiniita lakini nilimchunia si kwa sababu Aliolewa bali nilitaka nisimuone tena kwa sababu nampenda mno.
Ilikuwa siku ya jumatatu siku ambayo mimi na marafiki zangu tuliwahi chuo siku hiyo cha Ifm tukiwa tunajisomea kwa sababu mitihani ilikuwa inakaribia.Hakika haikuwa mimi na tu na marafiki zangu tuliowahi bali karibia wanafunzi wote darasani kwetu tuliwahi na kuanza kujisomea huku tukimsubiria lecture wa darasa letu aje kutufundisha.ghafla lecture akaingia darasani kwetu kisha akatuambia tumsikilize na kuanza kuongea
"Leo tutakuwa na Mgeni ambaye atakuja kuungana nasi kwa lengo la kusoma naombeni Mpeni ushiriki..."kabla hata ajamaliza mlio wa viatu vya skuna vilisikika ndani ya chuo kisha akaingia msichana Ambaye uzuri wake zikuweza kuufananisha Kwa kawaida alikuwa anafanana na nani lipsi zilizoambata na nywele ndefu huku mashavu yaliobonyea ambayo yalionyesha dimpoz kila wakati hata kama hajatabasamu huku kidevu kilichobonye pia ndio vilizidisha uzuri wa mrembo huyo ambaye Aliingia darasani kwa mwendo mdogomdogo na kuwaacha wote waliokuwa darasani kuwa mdogo wazi wakimshangaa mrembo huyo.Alifika na kukaa nyuma yetu ambapo alikaa na Msichana mwengine.kwa mbali nilisikia sauti yake ya kumtoa nyoka pangoni akimwambia msichana aliyekaa naye
"Hey do you have a pen(Eti una peni)"bila ya kuchelewa nikageuka na kunyoosha mkono wangu na kumpa peni ambayo alipookea kwa kusita sita huku akikwepesha macho yake yasiogongane na yangu jambo ambalo kwa mbali nikasikia sauti ya lecture iliyowafanya karibia wanafunzi wote darasini huo kucheka
"mmmmmhh vp baba usione chaka"..
Nilijikuta nikijisikia aibu baada ya lecture kuniambia vile na kugeuka nyuma huku bado wanachuo wengine wakiwa wanacheka.ilichukua muda mrefu sana kumjua kutokana na yeye kuwa mkimya sana nilijaribu kila mbinu kujaribu kumuingia lakini Sikufanikiwa.Siku mimi tu hata wale wenye uwezo mkubwa wa fedha wenye magari hapo chuoni walijaribu kumuingia msichana lakini hata namba ya simu hawakupata.Ni steve tu ndiye mwanaume wa kwanza chuoni hapo kuongea na msichana huyo na kupewa namba ya msichana huyo jambo lililomfanya ajitape na kututambia huku akitangaza dau la Milioni mmoja ili kumpa mtu namba ya msichana huyo jambo ambalo lilishindwa na wengi.Mawazo juu ya msichana huyo yaliendelea kuandama kichwa changu nakujikuta muda mwingine nikimuota katika njozi zangu nikiwa nawe jambo ambalo lilinipa faraja kubwa katika Moyo.kutokana na kumpenda sana msichana huyo nikajikuta nikimsahau kabisa jackline na kuacha umalaya kwa wasichana wengine.nilidiriki kabisa kumpiga picha msichana huyo bila ya kujijua kisha nikaikuza na kuipamba katika geto langu huku nikiwa najiliwaza nayo kwa kuibusu kila nilipokuwa naiangalia.siku moja nikiwa Najiandaa kwenda nyumbani rafiki yangu Martin akaniita
"ooya pablo nimeshalijua jina la yule demu mwanangu"
"daa nambie anaitwa nani..??"
"Moureen"
"daa basi kesho"nilimuaga martin ambaye alionyesha kufurahishwa kwa kumjua jina msichana jambo ambalo hata mimi nilifurahi kwa sababu hata mimi sikuwa nalijua jina lake.Mdogomdogo nikajikokota na kutoka njee ya chuo ambapo macho yangu moja kwa moja yakatua kwa mrembo huyo moureen alikuwepo ng'ambo ya pili ya barabara nilitamani kuvuka ili nimfuate lakini nilisita kwa sababu nilimuona akiwa na steve jambo ambalo liliniumiza moyo.nikiwa katika dimbwi la msangao Huku nikiwa nipo pembezoni mwa barabara nikiwa nataka kuvuka ghafla moureen akamuacha steve na yeye kuja kuvuka aje nilipo mimi.ile anafuka gari aina ya Harrier lilokuja kwa kasi lilianza kumfuata moureen ambaye kutokana na kuwa muoga akijikuta akisimama huku akifumba macho yake akiwa hana la kufanya.
"Noooooo"sauti ya steve ndio ilinishtua aliyekuwa akilisuhudia tukio hilo.nikajikuta nikitupa begi langu na moja kwa moja nikaanza kumkumbilia moureen ambaye nilifanikiwa kumsukumiza yeye lakini gari hilo la harrier likanigonga mimi na kunirusha Mbali sana kisha likafunga breki.ni nyota tu ndizo nilizokuwa naziona katika wakati huo huku damu nyingi zilikuwa zinanitoka sehemu yote ya mwili wangu.kiza kinene ndicho kilichukua nafasi yake katika mboni ya macho yangu na taratibu usingizi wa kuzimia ukachukua Nafasi yake...........
TAZAMA KICHEKESHO HIKI KISHA BONYEZA SUBSCRIBE ILIYOPO CHINI YAKE WAKATI TUKIELEKEA KWENYE MUENDELEZO

USIKOSE SEHEMU YA NNE
Maoni, Ushauri na Chochote Share Namimi Katika Mawasiliano Haya:
+255 718 274 413 Ipo WhatsApp
+255 764 339 438
ZephilineEzekiel@Gmail.Com
Maoni, Ushauri na Chochote Share Namimi Katika Mawasiliano Haya:
+255 718 274 413 Ipo WhatsApp
+255 764 339 438
ZephilineEzekiel@Gmail.Com