LISEME JINA LANGU (2)
JINA: LISEME JINA LANGU Mwandishi: Pablo SEHEMU YA PILI ILIPOISHIA... Tulikuta hali ilikuwa mbaya sana kwa halima ambaye kwa wakati huo alikuwa chini huku jackline kamkalia juu na kushika glassi kwa lengo la kumbamiza nayo kichwani.john haraka akamdaka jackline na kumpokonya glassi na kumshika huku na mimi nikimshika halima ambaye baada ya kushikwa jackline yeye alisimama kwa lengo la kumvamia ili amrudishie. SASA ENDELEA... "Malaya wewe ningekuua kudandia mabwana za watu.." "Halooo utajiju ndio nishamkamata bwana wako sasa pyeee..utajiju" "ndio hivyo kantangaze na wewe niachie nikammalize malaya niachie na kwambia niachie..aaaa niachie.."Ilikuwa sauti ya jackline aliyesikiliwa na john kwa nguvu na kutaka kujaribu kutoka.Kama kawaida ya wasichana waliendelea kurushiana Maneno ya nguoni yaliosababisha umati wa watu kujaa huku wambeya ndio wakizidi kuita wenzao waje kushuhudia tibwili hilo la Maneno ambalo bado lilikuwa likiendelea.Hakika katika Maisha yangu sikuwa…