LISEME JINA LANGU (3)
JINA: LISEME JINA LANGU Mwandishi: Pablo SEHEMU YA TATU ILIPOISHIA... Nilitembea kwa haraka haraka na kufika nyumbani kisha nikaingia ndani na kujitupa kitandani huku nikiwa na mawazo.hakipita dakika mlango wangu ukagongwa hali ilinishtua na kujikuta nikajizoazoa taratibu na kwenda kuufungua. SASA ENDELEA... "Vp anko mimi naitwa Alex nimetumwa na dada nije nikuletee mzigo wako."nilimuangalia kijana huyo aliyeonekana tunalingana kimakamo ambaye baada ya kusema hivyo alinipa bahasha ya kaki ambayo bila kusita nikaipokea kwa shauku kubwa "Dada gani" "Jackline".Baada ya kusikia jina la jackline nikajikuta furaha kubwa imeingia katika nafsi yangu nikamruhusu kijana yule ambaye bila kuchelewa akaondoka nikaingia ndani na kwa pupa nikaanza kuifungua bahasa hiyo na kukuta kadi ya mualiko kama wa sherehe fulani hizi na kukuta kikaratasi kilichoandikwa "Baby nimekusamehe jamani nakupenda sana naomba usikose kuudhuria katika sherehe hiyo itakayoanza kanisani pale posta …