LISEME JINA LANGU (4)

Zephiline F Ezekiel
LISEME JINA LANGU (4)
JINA: LISEME JINA LANGU Mwandishi: Pablo SEHEMU YA NNE ILIPOISHIA... Ni nyota tu ndizo nilizokuwa naziona katika wakati huo huku damu nyingi zilikuwa zinanitoka sehemu yote ya mwili wangu.kiza kinene ndicho kilichukua nafasi yake katika mboni ya macho yangu na taratibu usingizi wa kuzimia ukachukua Nafasi yake........... SASA ENDELEA... "oooooh aaaaaa"ni miguno ya maumivu niliyoyatoa baada ya kuamka na kujikuta nipo hospitali kichwa changu kilikua kimefungwa Bandeji kubwa iliyozunguka kichwa kizima nikajaribu kunyanyuka ili nikae kitako lakini nikazuiwa na nesi mmoja ambaye alionekana si muda mrefu alikuwa kashafisha kidonda changu kutokana na kuona baadhi ya bandeji iliyokuwa na damu damu na spirit katika chombo kama sinia flani hivi la plastic.kichwa changu kilikuwa kinauma sana huku kumbukumbu ya yote yaliotokea nikayakumbuka vizuri kabisa katika ubongo wangu.nilijikuta nikimuomba nesi japo niegeme mto kutokana nilikuwa nishachoka kulala ambapo bila ya kuchelewa alinisaidia bil…