LISEME JINA LANGU (4)

Zephiline F Ezekiel
0
Mwandishi: Pablo

SEHEMU YA NNE
Ni nyota tu ndizo nilizokuwa naziona katika wakati huo huku damu nyingi zilikuwa zinanitoka sehemu yote ya mwili wangu.kiza kinene ndicho kilichukua nafasi yake katika mboni ya macho yangu na taratibu usingizi wa kuzimia ukachukua Nafasi yake...........

SASA ENDELEA...
"oooooh aaaaaa"ni miguno ya maumivu niliyoyatoa baada ya kuamka na kujikuta nipo hospitali kichwa changu kilikua kimefungwa Bandeji kubwa iliyozunguka kichwa kizima nikajaribu kunyanyuka ili nikae kitako lakini nikazuiwa na nesi mmoja ambaye alionekana si muda mrefu alikuwa kashafisha kidonda changu kutokana na kuona baadhi ya bandeji iliyokuwa na damu damu na spirit katika chombo kama sinia flani hivi la plastic.kichwa changu kilikuwa kinauma sana huku kumbukumbu ya yote yaliotokea nikayakumbuka vizuri kabisa katika ubongo wangu.nilijikuta nikimuomba nesi japo niegeme mto kutokana nilikuwa nishachoka kulala ambapo bila ya kuchelewa alinisaidia bila ya hiyana kisha nikamuuliza.

"hivi dada kuna ndugu yangu yoyote amekuja??"
"ndio pablo hebu pumzika kidogo"ilipita kama nusu saa nikiwa nipo katika dimbwi la mawazo nikiwaza je moureen yupo katika hali gani kwa sababu mara ya mwisho ni mimi ndiye niliyemsukumiza nakulivaa mimi gari.nikiwa katika hali hiyo ya mawazo ghafla mlango ukafungulia ndani ya wodi ya chumba hicho kisha macho yangu yakatua kwa shangazi yangu ambaye ndiye mlezi wangu kutokana na wazazi wangu kufa kitambo na yeye ndiye aliyenilea akiambatana na nurse,steve,rafiki yake moureen suzan na moureen mwenyewe.furaha yangu ilichomoza baada ya moureen kuniangalia kisha akachia tabasamu jambo lililonifanya kama najisikia afadhali vile kumbe bado.kila mtu akaanza kunipa pole kisha baada ya wao kuondoka moureen akaja mpaka kwangu kitandani akanibusu shavuni na kuniambia

"Thanks"kisha akaondoka.siku zilizidi kukatika huku hali yangu ikarudi kama kawaida na kuruhusiwa kuondoka katika hospitali hiyo lakini katika siku zote hizo nilizokaa moureen alikuja siku moja jambo ambalo mimi nilipoteza japo shangazi aliliulizia juujuu.shangazi akanichukua na kukaa kwake kama siku tatu hizi kisha akaridhika na kuniacha niendelee na chuo kama kawaida.hamu ya kwenda chuo ndio ilichukua nafasi na kujikuta Asubuhi na Mapema nishaamka na kujiandaa huku hamu kubwa ilikuwa kwenda kumuangalia moureen Msichana aliyeteka sana mtima wa moyo wangu.kama kawaida nilifika chuo na kuanza kuzungukazunguka ili kupoteza mida kutokana na kipindi changu kuchelewa kidogo kuanza.Ghafla nikiwa katika zungukazunguka yangu nikashtuka nikikumbatiwa kumbatio la Nguvu sana na nilipomuangalia anaye nikumbatia alikuwa si mwingine bali ni moureen jambo ambalo sikuliamini kabisa nikajikuta moyo ukidunda baada ya kuona madimpoz yake karibu kabisa ya macho yangu huku tabasamu zuri liliambatana na macho malegevu kama mtu aliyekula kungwi

"unajua katika maisha yangu sijawahi kufanyia kitu kama ulichonifanyia wewe Aa sina cha kukulipa ikafikia thamani ya upendo wako ulionionyesha kwa kuniokoa pablo thanks"
"aa...aaa...mmm...h usij..ali bana mbona kawaida..."
"Yani sasa wewe ndio rafiki yangu wa ukweli kuliko wote" Moureen alisema maneno yale huku akizidisha mbwembwe za kunikombatia jambo ambalo lilizidisha furaha kisha mdogomdogo tukaanza kutembea kuelekea darasani huku mkono wa moureen akiupita kiuoni kwangu nikafatia na mimi huku nikijikuta hisia zangu zikienda mbali baada ya kushika kiuoni cha moureen kilichovutia zaidi hapo ndipo mwanzo kabisa ya urafiki wangu na moureen.urafiki wetu ulizidi kukomaa jambo ambalo lilimkera steve na kuona nimempeperushia ndege wake baada ya moureen kuwa na mimi muda wote akiwepo chuo.chat za hapa na pale katika simu ndizo zilishamiri na nakumbuka siku moja nilirushia vocha ya laki mbili katika simu jambo ambalo lilikuwa geni kabisa katika Maisha yangu.siku moja jumamosi nakumbuka Moureen akiwa na gari lake akaamua kunitoa out tukaelekea katika moja katia ya beach nzuri za kuvutia katika maeneo ya kunduchi na kubadilishana Mawazo.hapo ndipo moureen alipoitaji kujua historia ya maisha yangu ambapo bila ya kuficha nilimuadithia mpaka kufa kwa wazazi wangu kwa ajali ya meri.Alinirudisha nyumbani kwa kutumia gari lake kisha Akaondoka lakini hakupita hata dakika kumi messeji ikaita katika simu yangu na kuonyesha kuwa ni moureen aliyetuma bila ya hiyana nikaifungua na kukuta
"Pablo katika maisha yangu nimeona wanaume wengi tu lakini kwako nimeona kitu ambacho nahisi nikiwa na wewe nitafarijika sana.ukiachilia mbali kuwa si desturi kwa msichana wa kiafrika kumtamikia moja kwa moja mvulana the way unavyojisikia lakini mimi sina budi kukuambia "Nakupenda pablo Nataka uwe mume wangu"............

Nikajikuta mara kumi kumi nikisoma messeji hiyo huku akili yangu ikiwa haimini kabisa juu ya suala hilo.kutongozwa na msichana huyo niliona kitu cha ajabu na bahati kubwa niliyopata nilihisi kama nimeokota dhahabu chooni.kwa furaha nikamjibu Moureen na kumwambia nimekubali na huo ndio ukawa mwanzo wa mahusiano yetu matamu baina ya mimi na moureen

Kelele za mashibiki ndio zilinipa hamasa kubwa ya kuuanza mpira huo uliokuwa chini ya mguu wangu ambao kwa hamu na hamasa ulikuwa ukisubiria filimbi ya mwamuzi ambaye bado alikuwa anarekebisharekebisha saa yake ya mkononi aliyoiamini kwa kuendesha dakika katika mtanange huo wa kutaka na shoka ambao kurudi kwangu uwanjani kuliwafanya mashabiki wa team yetu kuongezeka kwa furaha ya hali ya juu baada ya kukumbuka mchango wangu mkubwa kutokana na mechi sita za nyuma walifungwa kutokana na kutokuwepo kwangu.ilikuwa kama kawaida timu yetu ya orlando ilikuwa inamenyana na timu ya young bozy ambapo mshindi atachukua kitita cha shilingi laki moja ikiambatana na seti nzima ya jezi na mipira miwili.mwamuzi akapuliza kipyenga na kawa kawaida mimi nikauwanzisha mpira ule kwa mwenzagu ambaye pia naye akaurudisha nyuma kwa mabeki wengine.hakika kurudi kwangu kuliwazuia sana timu pinzani kushambulia kutokana na kuniogopa wakajikuta muda mwingi wakikaba sana na kusita kwenda mbele na kujikuta wakiniruhusu mimi kupiga kichwa baada ya kuunganisha safi krosi iliyopingwa na mwenzagu ambapo kichwa kile kilizaa goli ya kwanza na kutufanya tuongoze.rafu za hapa na pale hazikutuzia kuendelea kumiliki na kutokana na kupata mawenge nikafanikiwa kufunga goli la baada ya kuwapiga chenga mabeki wawili na kubaki na kipa na kufunga kirahisi.mechi iliendelea mpaka mwisho wa mchezo tukawatume wafunga tatu bila huku magoli yote nikifunga mimi na kwa shukrani nikakabidhiwa mpira.hakika tulishereherekea sana lakini kabla ya kuondoka uwanjani hapo nikaja kuitwa na mchezaji mwenzangu ambaye aliniambia kwamba naitwa nilipoangalia niliona gari aina ya Altezza mpya ambayo baada ya kuisogelea nikamuona moureen bila ya kusita nikapanda kisha tukaondoka hapo na kuwaacha miongoni mwa watu wakiwa wanasema yao.kabla hata hajanifikisha nyumbani simu yake ikaita na kuipokea na kuanza kuongea baada ya kumaliza akanambia
"baby leo nilitaka nikae na wewe siku nzima but nimepigia na mama inabidi niwai"siku sita kumzuia nikamuacha aende huku hatukachana hivi hivi tukanyonyana ndimi kama dakika 15 hivi kisha nikashuka kwenye gari yake na kuanza kwenda getoni kwangu ila kabla sijafika magari mawili meusi yakaniovertaking bila ya kujua wapi yalipotokea kisha wakashuka watu sita ambao bila ya kuuliza mmoja wao akanipiga na kitu kizito kichwani na kusababisha nizimie.....

Pwaaaaaaaaaaaaaa" sauti ya maji niliyomwagiwa usoni yalionishtusha kutoka katika usingizi mzito ulionikumba baada ya kuzimisha kwa kupigwa na kitu kizito ambacho kiukweli mpaka sasa sikuwa najua nini.nilifumbua macho na kujikuta nimekaa kwenye kiti huku mikono na miguu ikiwa imefungwa na kamba nzito zilizosababisha kutokuweza kufurukuta kabisa mdomo mwangu kulikuwa na plasta kubwa iliyokuwa imenizuia mimi kuongea jambo lilinifanya nianze kupata maumivu sana mdomo mwangu.maumivu ambayo pia hakusita kuniandama katika sehemu ya kichwa na mikono huku nikijikuta natamani niugulie kwa kutoa sauti lakini plasta niliyofungwa mdomo ndio ilinifanya niugulie tu kwa kuhema.kumbuku ya yaliotokea niliyakumbuka kwa haraka sana huku nikipata shauku kubwa kwa nini walikuwa wamenifanyia hivyo.macho yangu yalikuwa yakiangaza angaza sehemu hiyo niliyofungwa ambapo awali sikulitambua eneo hilo ambalo kwa kukisia tu niliona kama sehemu kama kiwandani hivi kutokana na ukubwa wa eneo hilo ambalo usafi wake kulitosha kabisa kusambaza hewa nzuri iliyonifanya Nijifariji sana kana kwamba nilikuwa tayari nina maumivu.Nikiwa bado naangaza angaza macho yangu katika eneo hilo ndipo nilipowaona watu kama saba hivi huku mmoja wao akionekana kama mtu mwenye pesa kutokana na suti yake kali aliyovaa viliambatana na viatu vyeusi vilivyong'aa na kofia safi uliyotulia kichwani kwake.Aliniangalia kisha akachia tabasamu pana na kuanza kunisogelea mpaka akanifikia akaniangalia kisha taratibu akaupeleka mkono wake katika mdomo wangu nakunifungua plasta iliyonifanya niugulie kutokana na maumivu makali sana.

"Kijana jisikie upo huru kwanza maana hapa upo mikono salama"
"we....we nani kwanza mnataka nini kwangu jamani mimi mnaniuonea tu jamani kwani nimefanya nini.."nilijikuta nikilalamika huku machozi yakinilenga hali ambayo ilimfanya yule jamaa acheke kisha akanisogelea kwa ukaribu na kunitandika kofi moja kali sana la uso lilisababisha nichanike shavuni kutokana na kucha ndefu mkononi mwake kisha akanishika mashauzi na kuniangalia kwa usoni na kunitemea mate jambo ambalo lilinitia hasira sana lakini kutokana na kufungwa nikaishia kudondosha chozi tu mashavuni kwangu
"We fala mimi sijawai kupandishiwa na mbwa kama wewe na ukiendelea nitakupoteza Malaya wewe sasa unajua kosa lako???" akaniuliza swali ambalo kutokana na hasira ya kunitemea mate nikajikuta nikinyamaza huku bado hasira zangu zikizidi kupanda jambo ambalo pia lilizidi kumkasirisha yule jamaa ambapo kwa mara nyingine akanitandika kofi tena zito.

"Nakuuliza swali Mbona unibu swali langu je unalijua kosa lako??"
"Silijui Msenge wewe" nilimjibu kwa hasira na safari hii nikajikuta nikimtemea mimi mate jambo ambalo lilinigharimu akawaamrisha moja kati ya wafuasi wake mmoja aje kunipa ambao bila ya kuchelewa alikuja kwa kasi na kufyatua teke kali moja la kichwa lililopelekea mimi kudondoka chini kisha akaendelea kunikanyanga kanyanga tumboni na kichwani na mabuti yake ya kijeshi bila ya huruma na kunisabisha anitoe damu nyingi sana za kichwa na mdomo.aliendeleza kasi ya kunipiga mpaka yule jamaa alimuamuru akamzuia kisha akaja akaniinua na kunigisha magoti na kwa mara nyingine akavuta makoozi yake na kunitemea tena usoni. kisha akatoa picha yake mfukoni na kunionyesha.Macho yangu yalikuwa yanangalia kwa shida katika picha ile yalitua kwa mrembo mkali moureen ambaye alikuwepo katika picha hiyo jambo ambalo kwa namna moja ama nyingine yalinisangaza

DOGO ANAHITAJI MAONI YAKO, NDIO ANAANZA HIVYO BONYEZA PLAY KISHA SUBSCRIBE CHINI YA VIDEO NA BAADA YA KUTAZAMA VIDEO MPE COMMENT YAKO KAMA USHAURI KWENYE SANAA



USIKOSE SEHEMU YA TANO

Maoni, Ushauri na Chochote Share Namimi Katika Mawasiliano Haya:
+255 718 274 413 Ipo WhatsApp
+255 764 339 438
ZephilineEzekiel@Gmail.Com

Chapisha Maoni

0Maoni
Chapisha Maoni (0)