LISEME JINA LANGU (5)

Zephiline F Ezekiel
LISEME JINA LANGU (5)
JINA: LISEME JINA LANGU Mwandishi: Pablo SEHEMU YA TANO ILIPOISHIA... Kisha akatoa picha yake mfukoni na kunionyesha.Macho yangu yalikuwa yanangalia kwa shida katika picha ile yalitua kwa mrembo mkali moureen ambaye alikuwepo katika picha hiyo jambo ambalo kwa namna moja ama nyingine yalinisangaza SASA ENDELEA... "unamjua huyu mwanamke" "si.....m......ju..i" "wewe ubishi wako ndio unakuponza hebu lete ile mashine ya shoti aruke ruke kidogo" hakupita hata dakika shoti ya umeme ikaletwa kisha ukachukuliwa waya miwili na kuchomekwa katika mbavu zangu kwa kutumia Aina fulani hivi ya kama vibanio na kisha yule jamaa akachukua rimoti na kukaa nayo. "nakuuliza unamjua huyu mwanamke??"aliongea huku akinionyeshea picha ya moureen "Nakwambia simjui msenge wewe!!" "sawa bana"nilimsuhudia akabonyeza kitufe chekundu katika rimoti yake aliyoshika kisha nikaanza kutetemesha na shoti kali ya umeme huku nikipata maumivu makali sana.akaniacha na kuchukua…