LISEME JINA LANGU (5)

Zephiline F Ezekiel
0
Mwandishi: Pablo

SEHEMU YA TANO
Kisha akatoa picha yake mfukoni na kunionyesha.Macho yangu yalikuwa yanangalia kwa shida katika picha ile yalitua kwa mrembo mkali moureen ambaye alikuwepo katika picha hiyo jambo ambalo kwa namna moja ama nyingine yalinisangaza

SASA ENDELEA...
"unamjua huyu mwanamke"
"si.....m......ju..i"
"wewe ubishi wako ndio unakuponza hebu lete ile mashine ya shoti aruke ruke kidogo" hakupita hata dakika shoti ya umeme ikaletwa kisha ukachukuliwa waya miwili na kuchomekwa katika mbavu zangu kwa kutumia Aina fulani hivi ya kama vibanio na kisha yule jamaa akachukua rimoti na kukaa nayo.
"nakuuliza unamjua huyu mwanamke??"aliongea huku akinionyeshea picha ya moureen
"Nakwambia simjui msenge wewe!!"
"sawa bana"nilimsuhudia akabonyeza kitufe chekundu katika rimoti yake aliyoshika kisha nikaanza kutetemesha na shoti kali ya umeme huku nikipata maumivu makali sana.akaniacha na kuchukua na kuchukua bastola kisha akaiweka risasi na kuikoki akarekezea kichwani kwangu na kushababisha mimi nianze kutetemeka kutokana kuanzia nizaliwe sikuwahi kuonyeshewa bastola
"ni kwa mara ya mwisho na kuuliza unamjua huyu Mwanamke???"
"M..m....m...h..........."
"Paaaaaaaaaaaaaaaa".......

"Namjuaaaaaa"nilijikuta nikiropoka kwa nguvu baada ya yule jamaa kupiga risasi karibia kabisa na mguu wangu risasi ambayo haikunipata lakini kutokana na mlio wake niliousikia vizuri kabisa katika masikio nikajikuta nakubali kutaja mwanamke Ambaye nilikuwa namjua lakini sikutaka kumwambia moja kwa moja
"Hahaha sasa unavyoringa ringa kunijibu nitakufumua ubongo mimi haya anaitwa nani..??"
"Moureen"
"oooh kumbe kweli unamjua je ni nani yako huyu"
"aaaa ni rafiki yangu tu"
"anhaaa kumbe rafiki yako basi subiri."nilimshuhudia akikoki tena bunduki na safari alionekana yupo serias kisha akaelekeza katika kichwa changu kwa lengo la kuniuma
"Subiriiiii sio rafiki yangu ni msichana wangu"
"Aaaa mbona unanisumbua kijana unajua nitakuuuua."
"Hamna usifanye hivyo"
"Sasa sikia nikwambie huyo moureen ni mwanamke wangu ambaye nasubiri muda tu Amalize kusoma nimuoe nishatoa kiasi kikubwa sana cha pesa kwa baba yake jambo ambalo hata yeye analijua sasa basi kuanzia sasa sitaki kukuona tena na moureen na kama ukikaidi ukawa hata unaongeaa naye mimi nakufutilia sana basi nitakuuua umenisikia Mimi ndio Robertson Mugalula Nakuambia Nitakuuuua" hakika maneno yale yaliniingia kabisa katika nafsi yangu huku majonzi na simanzi yaliukumba moyo wangu ambao tayari ulishazama katika penzi zito la msichana huyo.uoga wa kuuwawa na robertson Mugalula jamaa ambaye mwili wake ulikuwa wa mazoezi sana licha ya kuwa na sura nzuri ambayo ilidhirisha kabisa yeye ni handsome boy na sura yake ya Baby face.Machozi yalianza kunitiririka taratibu jambo ambalo lilimfanya robertson kuniangalia kwa dharau kubwa kisha akamuita kijana wake mmoja ambaye alimnong'oneza kitu kisha jamaa huyo akanisogelea nakunitandika ngumi kali sana ya kichwa iliyopelekea kiza kizito kinitokee macho mwangu na kuzimia.

"Oyaaaaaa Hebu Amka"ni sauti iliyoniamsha ikiambata na kofi zito la mgongo ambalo lilinipa maumivu kidogo.nilijikuta nipo katika gari ambalo vioo vyake vilionekana kama ni tinted ambavyo vilikuwa havionyeshi kabisa nje nilimuona jamaa aliyenipiga kofi akiwa kavaa miwani meusi na suti huku mwili wake ukiwa umejazia sana
"Tokaaa"
"eee...naa..aaam aya...aaa"nilijikuta nikijibu kwa kigugumizi kisha yule jamaa akafungua Mlango wa gari hilo kisha akanisukumiza kwa nguvu na kutoka katika gari hilo huku nikidondoka na kuumia mguu wangu wa kushoto kisha gari hilo haraka likaniacha mimi pale ambako baada ya kusimama nilipagundua mapema palikuwa ni pale pale waliponikamata jana yake ambapo palikuwa karibu kabisa na nyumbani.Nilifika nyumbani huku nikichechemea na kisha nikaingia haraka ndani kwangu bila mtu yoyote kuniona niliangalia saa iliyopo chumbani kwangu na kugundua ilikuwa kama saa kumi na mbili jioni.nilienda kuoga kisha nikajitupa kitandani na kuiwasha simu yangu iliyokuwa nimeiweka chini ya mto katika kitanda changu na kubonyeza kitufe cha kuwasha ambapo nikakuta missed call mia moja na messeji Themanini nikazifungua nakukuta nyingi zikiwa za moureen ambazo kwa utulivu nikaanza kuzisoma "vp baby mbona upoke na mbona ujaja chuo nimekumiss vp wewe"ilikuwa ni miongoni mwa messeji ambazo kabla hata sijaendelea simu tena ikaita na nilipoangalia nikaona jina la moureen mpenzi likitokea katika screen ya kioo cha simu yangu
"Haloo vp pablo jamani"
"Kesho nakuomba tuonane raha resort restaurant"
"lakin........"Nilikata simu kwa uchungu kisha nikamtumia sms saa ya mimi na yeye kuonana katika hotel hiyo ambayo mara nyingi tulipenda kwenda

Saa ziliyoyoma na giza likaachia mwanga uchomoze na kuashiria siku mpya inaanza.bila ya kupoteza muda mida ya saa nne nikiwa nimevaa nguo zangu zilizonipendezesha sana.Nikaiwasha simu yangu iliyokuwa nimeizima kutokana na moureen kunisumbua sana kisha Mdogo mdogo nikatoka na kuchukuwa bajaj ambayo hakuchukuwa hata dakika thelathini nilikuwa nimeshafika katika hotel hiyo raha resort ambayo baada kumlipa mwenye bajaji nikaingia na kuanza kumtafuta moureen ambaye alishanitumia messeji kwamba alishafika.Sura yangu ikagonga kwa mwanamke ambaye ilionyesha uzuni mkubwa katika sura yake huku mavazi aliyovaa yalimpendezesha sana nilienda na kumgusa bega ambapo bila ya hiyana akageuka na kunikombatia huku ajibenua na kupeleka mdomo wake katika mdomo wangu ambapo kwa uchungu na simanzi zito nikamtoa
"whats wrong(tatizo nini) mbona sikuelewi yani siku hizi mbili umetesa sana kwa sababu ya kukuwaza"
"oooh moureen nataka tuachane"
"sijakuelewa unasema???"
"na...taka tuach..anee"nilisema kwa shida baada ya kushuhudia kwa mara ya kwanza moureen akidondosha chozi na kuniangalia mimi hali ambayo ilipelekea na mimi chozi kunidondoka
"kisaaa...nini??"
"Ro..bert Mugalula Ndi..."nilijikuta nikisita huku jina hilo nililolitaja likamshtua kidogo moureen ambaye bado machozi yaliendelea kumtiririka huku akiniangalia
"Can i kiss you now(naweza kukubusu sasa)"moureen aliniuliza swali hilo katika hali ya sauti ya kudeka hali iliyosababisha nishindwe kujizuia na kumkombatia kwa nguvu moureen kisha wote tukaanza kudendeka huku kila moja kutojali watu ambao walionekana kushangazwa na tukio hilo lakini ghafla simu yangu ikaita jambo ambalo lilinishtua na kujikuta nikimtoa moureen ambaye hakuwa tayari kabisa kuniachia niliangalia kioo cha simu yangu na kuangalia namba inayonipigia na kukuta namba ngeni jambo ambalo lilinifanya nipokee simu kwa uoga
"Sali sala zako za Mwisho Bitch(malaya)"

Nilijikuta nikianza kutetemeka baada ya Namba hiyo kukata simu kabla hata sijaongea chochote.Macho yangu yalikuwa yamenitoka huku majasho yakianza kunitoka mwilini mwangu hali iliyosababisha Moureen aanze kunishangaa
"Whats wrong pablo??(tatizo nini)"moureen aliniuliza lakini sikumjibu nikaanza kurudi nyuma nyuma hali ambayo moureen bado alikuwa haelewi
"unaenda wapi sasa??"nilijikuta kama nimechanganyika na kuanza kukimbia na kuelekea nje jambo ambalo lilimfanya nae moureen naye kunikimbilia lakini kabla hata sijaufikia mlango wa kutokea Nje milio ya risasi ikanipitia karibu kabisa katika masikio yangu na kunikosa na kwenda kuwapata waliokuwa mbele yangu ambao papo hapo wakadondoka na kufa hapo hapo jambo ambalo lilishtua watu wote katika hotel na kusababisha watu kuanza kupiga makelele na kuanza kukimbia hovyo ndani ya hoteli bila ya kutojua risasi imetokea wapi.kukimbia hovyo hovyo kwa watu kulisaidia kwa kiasi kikubwa mimi kutoka nje lakini Nje ndipo kulikuwa Na magari mengi meusi ambayo baada ya kuyaona Nikajikuta nikirudi ndani na kupotezana kabisa na moureen aliyekuwa akinikimbilia lakini hakufanikiwa kunipa kutokana na hata yeye kuchanganyikiwa na milio ya risasi.niliingia ndani kabisa ya hoteli na kuelekea moja kwao moja katika Miongoni mwa meza kubwa na kujificha chini ya Meza hiyo.macho yangu yalishuhudia watu wote wakiambatana na Wafanyakazi wa hoteli hiyo wakikimbia na kuacha hoteli yote ikiwa tupu ni mimi tu ndio niliyebaki huku nikiwa nimejificha katika meza kubwa ambayo iliniwezesha kutoonekana na kuona yaliyokuwa yanaendelea.nikiwa katika hali ya kukodoa macho ghafla watu waliovaa suti kama kumi wakiongozana na Robertson mugalula wakiwa wameshika bunduki wakaingia katika hotel hiyo na kuanza kunitafuta kila pande na kilichozidi kuniogopesha walipoanza kuangalia pia chini ya meza zilizokuwa zimedondoka na kunipa hofu kubwa.nikiwa natetemeka huku Bado majasho yakiendelea kunitoka nikaanza kuomba dua ili Mungu aweze kufanya miujiza kutokana na hali kuwa Mbaya.kwa macho yangu niliona kiatu kikali aina ya foengo kikiwa kinakuja kabisa katika mezi niliyokuwa na kushababisha mimi nitulie na kujikunja tuli kama Nyoka na kuendelea kumuomba Mungu afanye miujiza yake.Alifika pale na kuianza kuishika meza hiyo ambayo mimi nikiwa chini ya meza hiyo akiwa na lengo la kuinyanyua.Akiwa katika harakati ya kuinyanyua ghafla king'ora cha mlio wa gari la polisi ulisikika kwa nguvu hali iliyomfanya aichie meza kisha kwa mwendo wa speed akanzaa kukimbia kwa kutoka nje akiambatana na wenzake.hapo ndipo na mimi nilipopata nafasi ya kutoka na kufanikiwa kuwachenga mapolisi ambao baada ya mimi kutoka ndipo walipoingia wakiwa wamejiandaa vya kutosha.hakika mihemo ya kunusurika ndio ilichukuwa nafasi yake katika mwili wangu huku nguo zangu nilizovaa zikiloa zote kutokana na majasho mengi yaliokuwa yakinitiririka.hakika ilikuwa ni jambo jipya kabisa katika maisha yangu kwa sababu sikuwahi kutokewa na msukosuko kama huu wakataka kabisa kuuliwa niliendelea kujilaumu sana kutokana na kukaidi onyo nililopewa lakini nguvu ya mapenzi ndio yalinifanya nishindwe kabisa kujihimili mwenyewe.hakika hata kwa muda huo kwenda nyumbani nilianza kupaogopa kwa sababu nilihisi kama watakuwa wanapajua.mawazo ya kwenda kwa shangazi yangu ndio yalichukua nafasi yake na kukata shauri ya kwenda kwa kuchukua bajaj ambayo nilitegemea kwa vyovyote itaweza kunifikisha haraka.nilienda kuchukua bajaj ambayo kwa haraka ikaanza kwenda huku nikiwa bado nawaza.nikiwa katika dibwi la mawazo ghalfa simu yangu ikaita nikajikuta nikiipokea bila hata ya kuangalia nani aliyekuwa anapiga.

"haloow baby vp upo salama??,upo wapi??" ilikuwa sauti ya moureen niliyosikia hakika nilivyochoka nilijikuta nikiikata simu hiyo kutokana na ukweli kwamba nilishajichokea na maisha lakini ile naikata tu messeji ikaingia kwa uvivu nikaiangalia na kukuta ni ile namba iliyonambia nisali sala zangu za mwisho na kunifanya moyo wangu tena uanze kudunda kwa kasi ya ajabu na kuchoka kabisa.kwa simanzi zito nikajikuta nikiifungua huku nikiwa na uoga kabisa wa kuisoma hiyo messeji iliyosomeka

DOGO ANAHITAJI MAONI YAKO, NDIO ANAANZA HIVYO BONYEZA PLAY KISHA SUBSCRIBE CHINI YA VIDEO NA BAADA YA KUTAZAMA VIDEO MPE COMMENT YAKO KAMA USHAURI KWENYE SANAA



USIKOSE SEHEMU YA SITA

Maoni, Ushauri na Chochote Share Namimi Katika Mawasiliano Haya:
+255 718 274 413 Ipo WhatsApp
+255 764 339 438
ZephilineEzekiel@Gmail.Com

Chapisha Maoni

0Maoni
Chapisha Maoni (0)