LISEME JINA LANGU (6)
JINA: LISEME JINA LANGU Mwandishi: Pablo SEHEMU YA SITA ILIPOISHIA... Ilikuwa sauti ya moureen niliyosikia hakika nilivyochoka nilijikuta nikiikata simu hiyo kutokana na ukweli kwamba nilishajichokea na maisha lakini ile naikata tu messeji ikaingia kwa uvivu nikaiangalia na kukuta ni ile namba iliyonambia nisali sala zangu za mwisho na kunifanya moyo wangu tena uanze kudunda kwa kasi ya ajabu na kuchoka kabisa.kwa simanzi zito nikajikuta nikiifungua huku nikiwa na uoga kabisa wa kuisoma hiyo messeji iliyosomeka SASA ENDELEA... "PABLO PABLO,UNAVYOFIKIRIA UNAWEZA UKANIZIDI AKILI HATA MIMI SASA BASI NATAKA UCHAGUE MOJA KUUA WEWE AU SHANGAZI YAKO NA FAMILIA WASIO NA HATIA HAHAHAHA CHAGUO NI LAKO" hakika macho yangu hayakuweza kuamini messeji ile iliyotumwa niliendelea kuisoma kwa kuirudia kama mara kumi hivi huku akili yangu haukataka kuamini kabisa kwamba mtego uliobaki nilikuwa siponi kabisa.Kwa haraka haraka nikamlipa mwenye bajaj na kushuka kutokana na kufikia karibu na maeneo ya …